Impact ya EPL baada ya UK kujiotoa EU

esc343

JF-Expert Member
Apr 17, 2014
354
580
Baada ya UK kupiga kura na kuamua kujitoa kwenye umoja wa nchi za ulaya. Hii ina athari gani kwenye ligi yetu pendwa ya EPL?
Ikumbukwe moja ya sababu kuu ya hawa waingireza kujitoa ni swala zima la kazi, ilikuwa kama una EU passport basi ni rahisi kufanya kazi popote, hii inakuja mpaka kwa wachezaji. Sheria ya mchezaji ambae hayuko kwenye EU, ili aweze kupata kibali cha kufanya kazi( ina maana kucheza);
1. Mchezaji alietoka timu ya Taifa iliyopo kwenye 10 bora za FIFA. Awe amecheza michezo isiopungua 30% kwenye timu yake ya taifa ndani ya miaka miwili kipindi cha maombi
2. Mchezaji kutokea taifa 11-20 kwenye FIFA ranking, awe amecheza mechi za kimataifa zisizopungua 45%
3. 75% kwa timu za Taifa 30-50 kwenye FIFA rankings

Hzo ni baadhi za sheria kwa ambao hawakuwa EU yaani Africans,Asians,Americans, Wengi mtakumbuka sakata la Wanyama pindi alipokataliwa permit. Kwa vigezo hvyo, wachezaji wakubwa tu kama ANTONIAL MARTIAL, Ngolo KANTE, PAYET hawa ambao wamecheza mechi chache sana na timu zao za taifa maana waliitwa majuzi tu, hawata weza kupata kibali

Pia itakuja sheria ya wachezaji wa kigeni per team, ikumbukwe UK ilipokuwa ndani ya EU, wale wachezaji wanaotokea nchi za EU hawakuwa considered kama wachezaji wa kigeni, sasa pata picha wakiweka sheria ya wachezaji 6 au 5. Timu kwa United, City zitakuwa wapi

Swala la mauzo ya wachezaji nalo litakuwa na changamoto, kwanza kushuka kwa thamani ya pound. Pia sasa hv kununua young stars( biashara ya wenger) ili kuwakuza itakuwa ngumu maana kuna sheria kali sana ya kibali cha kazi kwa mtu below 18.

Ndoto ya watanzania kuchezea EPL ndio inazidi kupotea

Ila tuombee kwenye mazungumzo yao pindi watakapoanza, wata jaribu kupunguza makali( kuweka exemption) kwenye maswala ya wachezaji wa mpira.
 
Back
Top Bottom