IMF: Uchumi wa Tanzania waongoza Afrika Mashariki

RUCCI

JF-Expert Member
Oct 6, 2011
1,701
1,714
Tanzania inatarajiwa kusajili kiwango cha juu zaidi cha ukuaji wa uchumi wake mwaka huu katika kanda ya Afrika Mashariki na kati.

Hii ni kwa mujibu wa ripoti ya shirika la fedha la kimataifa - IMF.

Katika ripoti yake iliyotolewa hii leo Tanzania inatarajiwa kusajili kiwango cha juu cha ukuaji wa uchumi wake wa asilimia 6.9% mwaka wa 2016.

Kasi hiyo ya ukuaji wa uchumi wa Tanzania ni ya pili tu nyuma ya Ivory Coast baina ya mataifa ya Kusini mwa jangwa la Sahara .

Ivory Coast inatarajiwa kukuwa kwa kasi ya asilimia 8.5%.

Katika kanda ya Afrika Mashariki ,uchumi wa Kenya ndio wa pili kwa kasi ya ukuaji kwa asilimia 6%.

IMF hata hivyo inasema kuwa kasi ya ukuaji wa uchumi kusini mwa jangwa la Sahara unatarajiwa kupungua kwa mwaka wa pili mfululizo kutokana na kudorora kwa viwango vya uzalishaji na hivyo uwekezaji.

Kwa mujibu wa shirika la fedha la kimataifa - IMF, eneo hilo linakadiria kushuka kwa ukuwaji wa uchumi kwa asilimia 3 mwaka huu.

Kiwango hicho ni cha chini kabisa kuwahi kushuhudiwa katika miaka 15.

Mataifa yanayotegemea mapato yanayotokana na mafuta ndiyo yalioathirika zaidi kama vile Nigeria na Angola.

Aidha Zambia pia imeathirika vibaya kutokana na ukosefu wa soko la kimataifa la shaba yake.

Ripoti hiyo inaitaja Afrika Kusini kama moja ya mataifa ambayo kiwango chake cha ukuaji kimedorora kwa kiasi kikubwa mno.

Katika orodha ya mataifa yanayotarajiwa kuwa na kiwango cha juu cha ukuaji Kusini mwa jangwa la sahara Ivory Coast ndio inayoongoza.
Orodha ya mataifa ya kanda ya Kusini mwa Jangwa la Sahara na viwango vya kasi ya ukuaji wa uchumi 2016.

Ivory Coast 8.5%
Tanzania 6.9%
Senegal 6.6%
Kenya 6%
Zambia 3.4%
Nigeria 2.3%
Afrika Kusini 0.6%


Chanzo: BBC Swahili
 
Chini ya jemedali Magufuli na CCM uchumi utaendelea kukua kwa kasi zaidi kuliko nchi zote za Afrika...
 
hapo ndo wazungu wanatuona mazuzu! basi utaona vichwa nazi wanaanza kujisifia eti nchi imeendeleea wakati wananchi wake wanakula viwavi wanakufa kwa kukosa madawa hosipitalini watoto bado wanakaa chini mashuleni oooho eti uchumi unakuwa kwa kasi nyambafuu
 
Huo uchumi unakua kwenye Makaratasi 2 ila hali ya Mtanzania wa kawaida ni mby sana hasa maeneo ya Vijijini
 
Back
Top Bottom