IMF names Tanzania as 7th leading African economy

Kwani wewe shida yako ni Kenya? Mbona husemi Nigeria ambayo inatupita mara tisa? Jamani tukubali kuwa tuko kwenye right track kwani miaka si mingi tulikuwa nafasi ya pili mwisho kwa nchi masikini duniani wakati huo Kenya ikiwa na uchumi wa kati. At this pace mwaka 2025 tutegemee kuwa juu zaidi.
Tulikuwa nafasi hiyo kwa vile tulikuwa hatupiki data tunasema ukweli.
Na pengine ingekuwa wakati ule wa kusema ukweli kwa hali ya sasa tungekuwa wa kwanza toka kuleee!
 
Mkuu unaweza kutusaidia kuchambua hiyo GDP ya Tanzania per components yaani tueleze investments,Net exports,expenditure n.k zimekaaje isije ikawa tunashabikia GDP kubwa huku component ya expenditure imepanda kuliko investment

Nasubiri darasa
Hawatakuelewa wale wavimba macho, wanaosifia kila kitu.
 
Hizi takwimu za kwenye makaratasi tuliishachoka nazo sisi. GDP sio kigezo cha kupima ubora wa maisha ya watu ktk nchi husika.

Hata GDP ya Marekani imekuwa ikiizidi ile ya ulaya nzima kwa muda sasa lkn still wananchi wa Sweden, Denmark, Norway, Luxembourg nk wana maisha mazuri kushinda wa US.

Haya mambo ya GDP hayatatupeleka popote tupigane kuondoa umasikini kwa kuachana na miradi ya kutafutia "Kicks" na tuwekeze ktk kilimo. Period.
 
Tanzania - $56.66 billion

Tanzania holds the eight position with a total of $56.66 billion as the country’s GDP. Tanzania is largely dependent on agriculture for employment, accounting for about half of the employed workforce.


Source: www.thecitizen.co.tz


So uchumi unategemea KILIMO na hatutaki kuweka hela huko kwenye kilimo.
[HASHTAG]#weareinrighttrack[/HASHTAG]
 
Tulikuwa nafasi hiyo kwa vile tulikuwa hatupiki data tunasema ukweli.
Na pengine ingekuwa wakati ule wa kusema ukweli kwa hali ya sasa tungekuwa wa kwanza toka kuleee!
Hizi ni data za World Bank na IMF. Hawa hukusanya data zao wenyewe pote duniani. Ingalikuwa ni kila nchi kupika data zake kwani Tanzania ndiye bingwa wa kupika data kuliko Nigeria, Kenya na nchi zingine zote hapa duniani? Wakati ule IMF ilikuwa inatuweka wa pili au tatu kutoka mwisho kwenye LDCs duniani (Least Developed Countries) tulikuwa hatujui kupika data?
 
Hizi ni data za World Bank na IMF. Hawa hukusanya data zao wenyewe pote duniani. Ingalikuwa ni kila nchi kupika data zake kwani Tanzania ndiye bingwa wa kupika data kuliko Nigeria, Kenya na nchi zingine zote hapa duniani? Wakati ule IMF ilikuwa inatuweka wa pili au tatu kutoka mwisho kwenye LDCs duniani (lowest development countries) tulikuwa hatujui kupika data?
"Least Developed Countries" na sio "Lowest Development Countries" hii ya mwisho sio kiingereza fasaha.
 
Takwimu za kipu.mbavu ambazo hazina msaada wowote kwa mlala hoi... Ya saba so what???
 
Mkuu samahani, habari yako imenichanganya haijaniuma,kwani shuleni nimefundiswa kuna tafauti kati ya 7th na 8th
IMF imetu rank wa 7. Business Insider Sub Sahara Africa yenye makao makuu Nairobi imetu rank wa nane kwa kutumia kigezo cha GDP pekee na kuipendelea Kenya!
So uchumi unategemea KILIMO na hatutaki kuweka hela huko kwenye kilimo.
[HASHTAG]#weareinrighttrack[/HASHTAG]
Serikali hailimi. Kazi ya serikali ni kuweka mazingira mazuri kwa shughuli za kilimo. Kazi ya serikali ni kuhamasisha kilimo, upatikanaji wa mbolea na mbolea, dawa, zana za kilimo pamoja na masoko. Serikali inapojenga miundombinu za barabara, reli ya SGR na umeme ni kumjengea mazingira wezeshi wa kilimo chetu. Serikali inapohamasisha ujenzi wa viwanda, inachochea wakulima wetu walime zaidi. Inapojenga zahanati na vituo vya afya maana yake inaweka mazingira mazuri kwa wakulima wetu.
Kwa maneno mengine serikali huwa haipeleki direct money kwenye kilimo ili wakulima walime zaidi.
 
Back
Top Bottom