Imetosha: Suala la Jina bandia la Mh Paul Makonda Vs Askofu Jose Gwanjima

Vugu-Vugu

JF-Expert Member
Feb 24, 2017
1,344
1,531
Wanajamii”
Amani iwe pamoja nanyi”
Nitakribani mwezi mmoja sasa tangu kuibuka kwa sekeseke la madawa ya kulevya kulikozua taharuki na hofu kubwa ndani na inje ya mipaka ya Tanzania.

Hii ni baada ya mkuu wa mkoa wa Dar-es saaalam Mh Paul Makonda kutaja majina kadhaa hadharani ya aliowaita washukiwa wa madawa ya kulevya wa mkoa wake wa Dar-es salaam, Huku majina hayo akiyataja kwa awamu mbili katika siku na saa tofautitofauti ofisini kwake Jijini Dar-es salaam.

Awamu ya kwanza haikuwa na blust/mshituko wala manung`uniko yoyote kwani waliotajwa kwa kiasi fulani walitia shaka huenda ni kweli wanahusika na kadhia hiyo yamadawa ya kulevya.

Tatizo liko awamu ya pili yenye majina sitini na matano (65) huku yakiwemo majina kadhaa ya watu mashuhuri sana ndani na inje ya mipaka ya Tanzania, Wenye wafuasi na wategemezi mamia kwa maelfu.

Wa kwanza ni Mh Freeman Alkael Mbowe ambaye ni Mbunge wa Hai,Kiongozi wa wapinzani Bungeni, Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo( CHADEMA) Mgombea Uraisi Kupitia chadema mwaka 2005,,Mmiliki wa makampuni ya Freemedia(Tanzania Daima) na iliyokuwa Bilcanas.

Wa pili ni Yusuph Hussein Manji tajiri namba 5 Tanzania ,Diwani wa kata ya Mbagala jijini Dar-es salaam, Mdhamini mkuu ya timu ya ‘The Young African-Yanga’ na CEO wa makampuni ya Quality Group LTD.

Wa Tatu ni Askofu Josephate Gwajima wa Makanisa ya “UFUFUO NA UZIMA” ambayo yako zaidi ya 400 dunia kote na niwamiliki wa kanisa linalosadikiwa kuwa ni kubwa zaidi Africa.

Wanne Ni Miss Tanzania staafu na Mwigizaji maarufu duniani na aliyekuwa kada maarufu wa chama cha mapinduzi ambaye hata hivyo ametimkia CHADEMA anajulikana kama Wema Sepetu.Inasemekana mwana dada huyu alikisaidia kwa kiasi kikubwa Chama cha Mapinduzi katika ushindi wake wa 2015 japo anadai hawakuwahi kumlipa chochote mpaka anang`atuka.

Hawa watakuwa sample study yetu kwa leo.
Tunaelewa wote madawa ya kulevywa ni kitu kibaya kabisa kuwahi kutokea Duniani na yanapashwa kupingwa kwa nguvu zote na kila binadamu mwenye nia njema, Inchi nyingi zimetunga adhabu kali sana kwa watumiaji na wasambazaji wake, mfano Jimbo la Hong Kong inchini China adhabu yake ni kunyongwa mpaka kufa.

CHA AJABU NI BAADA YA MTUHUMIWA MMOJA (ASKOFU JOSEPHAT) NAYE KUITUHUMU SOURCE “The stretching principle”. Hapa pakamwibua Mh Raisi na kuunda haraka kamisheni ya kupambana na madawa ya kulevya ikiwa ni baada pia ya wabunge wa JMT kuhoji uhalali wa Makonda kutuhumu na kuwataja watu hadharani.

Binafsi nampongeze sana Mh Dr . John Pombe Joseph Magufuli kwa kumteua Sin`ga kuwa kamishna wa kuzuia Madawa ya kulevya inchini. Kama kuna mtu Serious serikali hii imepata ni huyu jamaa hana chembechembe za ukada hata kidogo is about Justice tu. Mungu atakuongoza kaka yangu ila kamwe usimwonee mtu Watanzania tukonyuma yako.

Imetosha ,Sitaki kumtetea Makonda wala Gwajima , Sitaki kumwamini Makonda wala Gwajima ila MASHAKA YANGU ni juu ya "kamakweli hivi ndivyo ilivyo kwanini iwe hivi "

1. Kama kweli Gwajima alijua tangu awali Paul Christian Makonda anaitwa Daud Albert Bashite kwanini alikuwa kimya mpaka Makonda alipomtaja kuwa ni miongoni mwa watuhumiwa wa madawa ya kulevya.


2. Kama kweli Magufuli hakumtuma Makonda amtaje Gwajima,Mbowe na Manji kwanini akae kimya hata pale watu wake(wananchi) wanapopiga kelele kwa sauti za juu kwenye Mashua waliopanda nyoka kaingia ndani kwanini yeye kama dereva anaendelea na Safari!


3. Kama kweli Magufuli hafahamu kuwa Paul Makonda si jina lake halisi kwanini hajashtuka kama anavyoshtuka pindi apatapo taarifa mbaya toka kwa Makonda.( Rejea aliyekuwa Mkurugenzi wa Jiji la Dar-es salaama Hayati Wilson Kabwe Mungu amrehemu mzee huyu na apumzike kwa amani-Amen )


4. Kama kweli Makonda jina lake ni Paul Christian Muyeke(Makonda) tatizo liko wapi kuthibitisha hata kwa kumtumia Baba yake . Aje na vyeti/vitambulisho vya Christian Muyeke ili wale wauza unga wadhalilike, naupate legitimate uendelee na legacy yako kwa kasi ya ushindi thidi yao ( Vyeti [HASHTAG]#Madawa[/HASHTAG] ya kulevya)

5. Kama kweli Magufuli amelisikia sakata hili la Makonda,Je ameridhika watu kumshambulia kwenye mitandao ya kijamii kisa ndugu yake Paul Christian Makonda.

6. Kama kweli Makonda Yeyey ni mteule tu kwanini tunamzonga Yeye badala ya aliyemteua( Raisi).

7. Kama kweli Magufuli hana mutual benefit na Makonda kwanini anamwogopa kiasi cha kushindwa kuhoji uhalali wavyeti vyake na ukwasi alionao kwa kipindi cha mwaka mmoja.

8. Kama kweli Magufuli halei na kupendelea ndugu zake wasukuma kwanini asichukue hatua za haraka kama ilivyo kawaida ya huyu Msemakweli mpenzi wa Mungu!

9. Kama kweli Magufuli anakumbukumbu ya aliyoyasema juu ya wenye vyeti fake watakimbia inchi wenyewe mbona mambo ni tofauti kwa Makonda, Mpaka sasa yupo kazini au alimaanisha wale tu wasio wake hasahasa watu wa upinzani.

10. Kama kweli waliogushi majina na Vyeti walishafukuzwa kazi je si zaidi ya huyu mmoja.


# Mungu ibariki Tanzania na watu wake#

"Msema kweli mpenzi wa Mungu."

Na Sasa Arusha kumchagua Lissu​
 
What motivate you to write all this? I just have one Question that need answer
 
mkuu nchi yetu ni ngumu kuelewa nani mkwel nani muongo ........

kiufupi tuna rais muongo na watendaji mazwazwa asilimia kubwa.......

Gwajima yupo sahihi watu tunajua siri nyingi mno ila tunanyamaza..........
 
1. Kama kweli Gwajima alijua tangu awali Paul Christian Makonda anaitwa Daud Albert Bashite kwanini alikuwa kimya mpaka Makonda alipomtaja kuwa ni miongoni mwa watuhumiwa wa madawa ya kulevya.
Hapo kabla, Gwajima hakufahamu suala la Bashite! Lakini kama ilivyo kwa yeyote yule, baada ya Gwajima kutajwa na Makonda akalazimika kutafuta the motive behind!

Katika kutafuta huko ndipo akafahamu kwamba kumbe Makonda anatokea Kolomije!! Na katika kutafuta zaidi, ndipo akaja kugundua hilo la Daudi Bashite!!!

Hapa mara kadhaa nimeshasema... jina la Daudi Bashite alikuibuliwa kwa mara ya kwanza na Gwajima! Kwa mara ya kwanza hilo jina hapa JF lilitajwa December 15, 2015 kabla ya the called vita dhidi ya dawa za kulevya!!!

Member mmoja alionesha kushangazwa kwake Daudi Bashite kuitwa Paul Christian Makonda!! Na ukimsoma huyu member, wala haoneshi kwamba ni mtu mwenye ile tabia za minyukano ya kisiasa au kitu chochote sawa na hicho!!!
Nilikutana naye Koromije Misungwi Mwanza miaka ya 2000 enzi hizo akiitwa DAUDI Bashite. Sifahamu kivipi anaitwa Paul Makonda. Namfahamu in and out
Halafu msome hapa
Yes you are very correct. Baba yake alikuwa kamanda wa Sungusungu enzi hizo wanakijiji walikoma. Mnazifahamu mboko za Sungusungu?
Kisha oanisha na habari za Mwanahalisi hivi majuzi kwamba Mzee Albert Bashite hapo kabla alikuwa mwanajeshi Tabora kabla hajastaafu na kurudi Kolomije!!!
 
mkuu nchi yetu ni ngumu kuelewa nani mkwel nani muongo ........

kiufupi tuna rais muongo na watendaji mazwazwa asilimia kubwa.......

Gwajima yupo sahihi watu tunajua siri nyingi mno ila tunanyamaza..........
Nina siku sikuoni mkuu technically!!!!
 
Hapo kabla, Gwajima hakufahamu suala la Bashite! Lakini kama ilivyo kwa yeyote yule, baada ya Gwajima kutajwa na Makonda akalazimika kutafuta the motive behind!

Katika kutafuta huko ndipo akafahamu kwamba kumbe Makonda anatokea Kolomije!! Na katika kutafuta zaidi, ndipo akaja kugundua hilo la Daudi Bashite!!!

Hapa mara kadhaa nimeshasema... jina la Daudi Bashite alikuibuliwa kwa mara ya kwanza na Gwajima! Kwa mara ya kwanza hilo jina hapa JF lilitajwa December 15, 2015 kabla ya the called vita dhidi ya dawa za kulevya!!!

Member mmoja alionesha kushangazwa kwake Daudi Bashite kuitwa Paul Christian Makonda!! Na ukimsoma huyu member, wala haoneshi kwamba ni mtu mwenye ile tabia za minyukano ya kisiasa au kitu chochote sawa na hicho!!!

Unaboa kweli ku- quote thread nzima.

weka link
 
Ungemsikiliza Gwajima toka mwanzo anaanza kufichua siri za Bashite usingeuliza ulichouliza na pia ungefuatilia jinsi vita hii ilivyoenda mpaka sasa impacts zake ni -ve or +ve basi usingeuliza swali kwa Bashite zaidi ya kumkosoa
 
sifuri haina cheti kwa hiyo kampeni ya kuonyesha cheti haina mashiko.......nimesikia kuna mtu amejitoa mhanga kufungua kesi hili jambo sasa tutaona je taaluma itaingizwa siasa....(najaribu kupata picha mshua wa mungu wa dar apeleke memo pale necta mh aprintiwe mnyama kwa jina lake duh tutaumbuka mbaya)....
 
Alikuwepo January Makamba kipindi cha J.K amefifia kama mshumaa,hata bashite atafifia tu hamna marefu yasiyokuwa ncha.
 
Mkuu mleta uzi....Inawezekana kweli MAKONDA ana HATIA juu ya hili la vyeti....LAKINI SWALI LA MSINGI hili la vyeti vya MAKONDA limekuja wakati upi?????.....Ni wakati ambao MAKONDA anafanya kitu ambacho kiongozi yoyote,mwananchi yoyote mwenye mapenzi na NCHI HII angemsapoti kwa vyovyote vile....Kilicho haribu hapa kuhusu hizi TUHUMA ZA MAKONDA juu ya VYETI vyake ni haya yafuatayo.....
1...Ni kipindi ambacho hili suala la vyeti vya MAKONDA limevamiwa na kuvaliwa njuga na WAOVU wa MADAWA YA KULEVYA.....hivyo kumwajibisha MAKONDA ni sawa na kudhoofisha hii VITA ya madawa ya KULEVYA na itakuwa ni USHINDI MKUBWA kwa hawa waovu wa madawa ya kulevya.....HATA ANGEKUWA RAIS NI NANI hili la MAKONDA asingethubutu kumgusa.....
2..Kingne ni uchapa kazi wa HUYU kijana.....Honest MAKONDA anapiga kazi vilivyo anawazidi hata hao WENYE VYETI...hili nalo ni moja ya SABABU kubwa sana linalozuia MAGUFULI asimwajibishe MAKONDA...naamini kabsa asilimia 90 ya member wa JF mmoja tu angekuwa RAIS kamwe asinge thubutu kumwajibisha KIJANA mchapa kazi anaendana IDEOLOGY ZAKO IPASAVYO.....
3..Mkubali mkatae MAKONDA naitendea HAKI JIJI la DSM kiuongozi na kuyafikia ipasavyo MAISHA ya watu wa hali ya CHINI ili HAKI zao zipatikane...
Kwa hayo machache hapo JUU NI RAIS/KIONGOZI yupi ataweza muwajibisha kiongozi aina ya MAKONDA japokuwa ana yake makosa......na hayo MAKOSA si ya kuhatarisha MAISHA YA WATANZIA???.hell no
 
Nimeshaweka post husika hapo juu... ifuate hiyo na utaona ni mwaka gani!!![/QUOTE

Sijakuelewa wewe unatakaje, kama swala linazungumziwa ni moja yawezekana baadhi hoja zikarandana.
 
Back
Top Bottom