Nkuruvi
JF-Expert Member
- Dec 1, 2014
- 624
- 649
Wandugu,
Kipindi tulichopo ni muhimu sana kuhakikisha afya zetu zinakuwa imara. Magonjwa hasa hii UVIKO-19 inatishia amani ya Dunia.
NEWSTART ni mfumo wa maisha ambao umesaidia wengi kuimarisha afya zao na kuwawezesha kukabiliana na magonjwa kwa kutumia kanuni nane- NEWSTART
NEWSART ni Kama ifuatavyo"
1. N- NUTRITION- LISHE
Lishe ni jambo muhimu katika kuujenga mwili ili uweze kupambana na maradhi. Hakikisha mlo wako unakuwa kamili ili kuupa mwili wako uwezo wa kupambana na maradhi
2. E- EXERCISE- MAZOEZI
Fanya mazoezi ya mwili. Waweza kukimbia, kurukaruka au kucheza mpira. Mwili wa mwanadamu unakuwa imara unapofanya mazoezi. Kumbuka kama haikulazimu kwenda mailli moja kutafuta chakula, basi inakulazimu kwenda maili moja kumeng’enya chakula mwilini mwako. Hii ni kanuni ya maisha
3. W- WATER- MAJI
Kunywa maji safi na salama kwa angalau glasi 8 kwa siku. Hii itawezesha mifumo yako ya mwili kufanya kazi kwa usahihi kwa kuwa maji ni muhimu kwa ufanisi za mifumo ya mwili. Kumbuka 70% ya mwili wako ni Maji.
4. S- SUNLIGHT- MWANGA WA JUA
Pata mwanga wa jua kwa afya hasa jua la asubuhi. Hii husaidia utendaji mzuri wa mifumo ya mwili na homoni.
5. T- TEMPERENCE- KIASI
Uwe na kiasi katika kila jambo unalofanya. Iwe ni chakula, kufanya kazi, kusoma au shughuli yeyote, fanya kwa kiasi.
6. A- AIR- HEWA SAFI
Rasilimali muhimu kabisa kwenye mwili ni hewa. Pata hewa safi. Mazingira unayoishi au unayofanya kazi hakikisha ni mazingira yenye hewa safi
7. R-REST- PUMZIKA
Pumzika. Pata usingizi wa kutosha. Uwe na siku maalumu ya kupumzika, siku ambayo hufanyi kazi yoyote. Hapa ni vizuri kama Mungu alivyoagiza Kutoka 20:8 “Siku sita fanya kazi, ya saba ni Sabato”. Mungu anatutaka tupumzike
8. T- TRUST IN DIVINE POWER- TEGEMEA UWEZO WA MUNGU
Mtegemee Mungu katika maisha yako yote. Kama Mheshimiwa Rais anavyotusihi, maisha haya tuliyonayo yapo mikononi mwa Mungu, tumtegemee yeye.
Nawasilisha