Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 22,454
- 32,980
Abuu,
Wazee wetu waliona balaa lililoikumba India kwa kuingia katika kudai uhuru vyama vyao viwili Congress Party kikiwa chama cha Wahindu na Islamic League kikiwa chama cha Waislam.
Kila chama kinamtazama mwengine kama adui mkubwa.
Usiku 1947 wanashusha bendera ya Muingereza wanapandisha bendera ya India huru asubuhi vita vya wenyewe kwa wenyewe vinaanza.
Vikamalizika kwa kugawana ardhi kila mtu na kwao.
Ilikuwa Abdulwahid Sykes achukue uongozi wa TAA kama President 1953 na 1954 waunde TANU na wadai uhuru.
Hamza Mwapachu akamwambia Abdul chama cha TANU kitakuwa kama Al Jamiatul Islammiya fi Tanganyika (Umoja wa Waislam wa Tanganyika) kwani Waislam tumejazana katika siasa Wakristo wako pembeni.
Njia ya kuwavuta Wakristo watuunge mkono ni Julius Nyerere atiwe kwenye uongozi wa juu wa TAA 1953 na 1954 TANU inaundwa na Nyerere anaongoza harakati za kudai uhuru.
Wakristo wataingia TANU kwani hawataiona TANU kama chama cha Waislam.
Kinyume cha hivi Waingereza watawaambia Wakristo waunde chama chao kupambana na TANU chama cha Waislam.
Tanganyika ingeingia kudai uhuru ikiwa na vyama viwili hasimu vilivyojikita kwenye dini.
Bahati mbaya mno Nyerere akiogopa sana kueleza ukweli vipi juu ya ugeni wake Abdul Sykes alimshika mkono hadi kuwa kiongozi wa TAA 1953 na TANU 1954 na 1955 akazungumza UNO.
Leo Tanzania hali ndiyo hii ingekuwaje kama tungeingia kudai uhuru tumegawanyika kwa misingi ya Uislam na Ukrist
Mwezi June, 1953 Makao Makuu ya TAA, New Street ilitangaza Kamati yake ya Utendaji: J. K. Nyerere, Rais, Abdulwahid Sykes, Makamu wa Rais; J. P. Kasella Bantu, Katibu Mkuu; Alexander M. Tobias na Waziri Dossa Aziz, Katibu wa muhtasari; Wajumbe wa kamati: Dr Michael Lugazia, Hamisi Diwani, Tewa Said Tewa, Denis Phombeah, Z. James, Dome Okochi, C. Ongalo na Patrick Aoko.