Ili Usitoe Pesa kwa trafick police fanya hivi!

Hii mada imenikumbusha vitu vingi.Huwa sitoi fedha ya aina yoyote kwa askari wa usalama Barabarani,Nina bahati huwa hawanisimamishi hovyo(kutokana na aina ya gari ninayoendesha).
Mara chache wale wanaokosea njia huwa nafanya yafuatayo

  • sifungui kioo
  • sifungui mlango
  • siweki gari pembeni y abarabara kusipo na parking
  • sisimami katikati ya barabara kuwasikiliza.
  • sisimami kama sina kosa,barabarani sio sehemu ya kuombana leseni(huu ni msimamo wangu)
  • Gari muda wote huwa locked,with radio on,eyes on the road,and sight mirrors.not on some shitty traffic(nimeshanote wanaosimamisha bila mie kuwapa attention)
ikitokea wametimiza 1,2,3,4 nikisimama nafungua kioo upana wa nchi 3,na kumsikiliza shida yake.nikishamsikiliza na kumuelewa namuomba jina lake kamili,namba yake ya askari pamoja na kituo chake cha kazi.
huwa siwaambii,lakini nina recorder kwenye gari,ninachofanya ni kurekodi kila upuuzi wanaosema.nikishaona haelewi,kang'ang'ania kuomba rushwa,na anaonesha muelekeo wa mie kumtimizia njaa yake huwa namuomba dakika 5 tu asikilize upuuzi woote alioungoea,ikishafikia stage hii,basi kinachofuata ni jamaa kutahayari,kuomba radhi,kunukuu vifungu visivyokuwepo,na kuondoka.

Kama nina kosa obvious (niko makini sana barabarani,gari ninayotumia ni mpya,haina makosa ya kipuuzi),huomba notification na humweleza waziwazi kuwa sitampa pesa ya aina yoyote pale barabarani kwani yeye sio muhasibu wa serikali.

Kwa stage hizo ninazopitia hapo juu napenda ku-declare kuwa sijawahi kutoa RUSHWA BARABARANI,EVER.
 

Teh teh hiii niliifanya hapo Mombo mzeee maaskali walitaka kulia na wakaniachia tuuu kwa hurum nikawapa ten ili wasinune zaidi ila kweli hiyo ndo dawa watu hawajajua notiofication hulipwa within seven days na sio lazima pale.

Ila watakapo tukamatia ni mfumo huu wa Electronic License wakuuu iki swapiwa kwa kamtambo kao na hujalipa madeni itakula kwako haina budi ila ndio maendeleo yaendako nasi tutaya tii tuu.

Nakuunga mkono kwa hoja yako nzuri

 
ebu someni masharti ya notification tena mkumbuke iyo sio receipt na wakati ela ya serikali ikitolewa lazima upewe receipt watu wanaishia kupewa notification.wizi mtupu
 
Kabla ya uchaguzi nilienda K/Koo,kule huwa hakuna parking kwa hiyo alternative pekee ni kuweka gari pembeni ya barabara.
Basi siku hiyo wakaja vijana wawili,wakajitambulisha kama askari wa jiji,wakati wamevaa nguo za kiraia.
mazungumzo yalikuwa hivi.

kijana1"mzee umefanya kosa la ku-park sehemu isiyoruhusiwaunatakiwa utoe faini ya laki moja."akasema kijana yule huku akinionesha karatasi yenye orodha ya faini.

Mimi"kunakoruhusiwa kuna alama yoyote?mbona watu wameweka magari yao mbele na nyuma yangu?"

kijana2"hao tumeshawatoza faini?"

Mimi"mbona bado wameweka magari yao sehemu zenye makosa?"

Kijana1"si unajua mzee wameondoka,ila wamelipa faini"

Mimi"Ebo!!sasa kama hakuna tatizo wao kuweka gari pale,na mmeshawatoza faini,inamaanisha nia yenu sio kuondoa magari yaliyokaa vibaya bali kuyatoza faini,si nidivyo?"

wote kwa pamoja" unajua mzee sisi ni askari wa jiji,na vitambulisho tunavyo".
There i thought something is wrong,they produced some fishy laminated paper with the list of all possible mistakes.

Mimi"naomba vitambulisho vyenu"


waliponipa nikavipiga picha na kuwarudishia,kisha nikawaambia sidhani kama wao ni askari/wafanyakazi wa jiji,kwani vitambulisho vya vinatofauti ya uchapaji na FONT(sikuwaeleza haya).Na nikawaambia sijafanya kosa lolote la kuwapa wao fedha.Na kama wanadhani nahitaji kulipia faini kwao basi wanipe notification ya kwenda kulipia manispaa.kuona vile wakaanza kunilaumu kuwa mie mbishi sana na sijawathamini kama wao ni askari na kuondoka zao.

ushahidi upo kwenye picha hapa chini.


Je,hawa kina Thobias W.Mgaya na Wilson R.Mongi(Kama hayo ni majina yao halisi) wako wangapi?
Muwe waangalifu kwani muda mwingine mnaweza mkatoa fedha/fine/rushwa kwa watoto wa mjini.
 


Ayaaaaaaa. Hii post si ingekuja zamani kidogo. Mi wiki iliyopita traffic kachukua leseni yangu na akaniandikia notification (Road licence imeisha) na akasema nikishalipa nimpelekee risiti anipe leseni yangu. Mnanishaurije hapo wana jamvi. sikuwa na hela ya raod licence nasubiri mwisho wa mwezi huu ndo nikakate.
 

Mkuu, hao si wazoefu.

Wale mazoefu atakwambia, twende Kituoni. Mkifika huko unaambiwa subiri. You can spend even the whole day . . . .
 
Mkuu, hao si wazoefu.

Wale mazoefu atakwambia, twende Kituoni. Mkifika huko unaambiwa subiri. You can spend even the whole day . . . .

Hiyo itawezekana kama tu utamuachia aingie kwenye gari.au atakupelekaje kituoni?
 
Mkuu, hao si wazoefu.

Wale mazoefu atakwambia, twende Kituoni. Mkifika huko unaambiwa subiri. You can spend even the whole day . . . .

Mwenzenu mie kama gari yangu inamakosa huwa sisimami kabisaa yaani bora shari kamili kuliko usumbufu wao barabarani
 
Hapo juu mengine ni makosa unayafanya, uyafanye tu kwakuwa unaendeshea Bongo. Na mengine ya kutofungua mlango au vinginevyo, baadhi ya sehem utatolewa kwenye gari na kuwekwa kwenye gari la polisi kisha gari lako litakufuata huko. Naongelea kule wanakofuata sheria.
 
Nawapongeza wana JF kwa kujadili mada hii ambayo kwakweli dereva yeyote lazima anajua tamu na chungu yake. Cha muhimu unapokutana na traffic kwanza lazima uthamini kazi yake kinyume na madereva wengi ambao ni mabosi kwa namna nyingine. Kuwajibu kwa jeuri hata kama unatambua kuwa una makosa. Pili ni vema hawa polisi wakajua kuwa madereva nao ni binadamu mapungufu lazima yatakuwepo ndo mana waliweka kifungu cha kumpa onyo dereva. lakini sidhani kama kinatumika kwani kila kosa ni faini tu. Asanteni na hongereni nafikiri tutaendelea kujadili masuala muhimu na kuelekezana namna ya kuyatatua. JF fagilia:mod::mod::mod::mod:
 
Alafu kitu kingine jamani kama ulilipa iyo 20000 badala ya receipt wakakupa notification sasa huoni kuwa huo ni uhuni?
Hawa matrafic huwa wananikera sana nkiwaga na muda huwa nakomaaga nao sana

Inatakiwa kuwekwa wazi kuwa, Traffic hatakiwi kupokea pesa ya faini toka kwa mvunja sheria, walichotakiwa kuwa wanafanya ni kukupa notification na wewe kwenda lipa TRA ambao nao wanatakiwa kuwa na mfumo wa kielectronic wa kupelekeana taarifa kwamba gari gani limepigwa faini na kiasi gani then fine imelipwa au la kwa TRA. Mfumo huu ulitakiwa kuwa na incentive kwa traffic kwamba at the end of the year wanapata bonus ya 1% ya notification alizotoa. Sasa hapa pia panaweza kuwa na kosa maana wanaweza kuwa wanatoa notification kama njugu. Ila kama mtu hujaridhishwa unaomba kupelekwa mahakamani ili haki itendeke.

Tanzania tukitaka kuondoa rushwa za barabarani tunaweza kwa watu kuacha burgain na traffic, na ikiwa traffic atatumia vibaya cheo chake kumpotezea muda dereva bila sababu anaadhibiwa kwa kumlipa dereva. hapo tutashuhudia uadilifu wa hali ya juu.
 

Pdidy vyoote hivyo mimi nilikua navyo na akakuta sina kosa lakini nilichompendea Trafiki huyo aliyenishika akaniambia kwa upole ASIEE FANYA HATA BUKU MBILI NIKAZIMUE HALI NI MBAYA! NIKAMKATIA HALAFU NIKAENDELEA NA:car:
 
mimi gari yangu natembelea cheses no wananikamata kila saa wanasema hairuhusiwi kutembea mpk ipate no jana mmoja kanikamata saa mbili usiku ananiambia hayaruhusiwi kuonekana brbrni usiku nisaidieni sheria inasemaje
 

Mdau umesahau hapo kwenye list ongezea copy ya kadi ya gari -iwe Certified na ilipiwe stamp duty ya sh 500/=

BY the way weekend moja jamaa waliwahi kunisimamisha , kisa eti waliona nimevalia kivest na miwani tinted wakafikiri mimi mhuni hivyo lazima wanipate tu. basi walichoka walipoulizia vitu vyote hapo juu nikatoa kimoja baada ya kingine...guess what wakaniambia " naona umejipanga mno hadi stamp duty kwenye copy ya kadi ya gari !!! duuu kweli hatukupati" kisha wakamalizia " tunaomba basi walau jero ya chai" NIKAHAMAKI kama vile sikujua shida yao kisha nikawaambia- kama msingalinipotezea muda mkaenda straight to the point tangu mwanzo ningeweza kuwapatia out of courtesy lakini nisha tumia 4 minutes hapa then mnaomba na chai??? Basi haooo wakanywea . Next time nikapita maeneo hayo hayo weekend, this time alikuwepo mmojawapo wa wale wa siku ya mwanzo na wengine wawili... basi one of those new faces akanisimamisha , ile kusimama tu yule veteran akaniona ..akacheka akawaambia wenzake huyo mwacheni msijisumbue hampati kitu hapo maana jamaa amejipanga kupita maelezo...Basi huyooo nikaondoka in less than 30 seconds. So wadau ukiwa umetimiza sheria zote ni saafi sana unakuwa huru kiuhakika
 

Hairuhusiwi kuchukua reseni ya mtu.Notification inaruhusiwa kulipwa ndani ya siku 7
 
Cha msingi ni kuwakumbusha watumiaji wa magari ni kukatia magari yao bima ya garil ako, japo thirdy party, huwezi kuamini watu wengi sana hawakatii magari yao bima, sijui kwa kusahau au nini hadi wakamatwe na trafic.

One day trafic alinikamata hapo kwenye mataa ya maktaba (nakata kona toka posta), baada ya kuuliza leseni, tra licence, bima, triangle, fire ext, washa taa na etc na kujionea kila kitu kipo sawa, akaanza kuniambia pale kwenye mataa umepita na taa nyekundu, nikamkatalia na kumuomba anipe ushahidi wa anachonishitakia, maana nilipita na taa ya kijani hata ya njano ilikuwa bado haiijawaka na nyuma yangu yalipita magari kama 7 hivi, alivyoona najua nachofanya akasonya tu na kuniachia niende, yaani alitaka kunichomoa hela kilazima hivi hivi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…