Ile ndoa nimeihairisha rasmi, nitaoa 2035

Nebuchadinezzer

JF-Expert Member
Oct 1, 2018
1,403
2,545
Poleni sana kwa usumbufu niliowapatiena hasahasa wale mliokuwa na nia ya dhati kuchangia ili kufanikisha sherehe yetu ya ndoa kati yangu Nebuchadinezzar na Bi. (Jina Kapuni ili kulinda heshima yake hapa JF).

SABABU: Nimegundua mchumba wangu hatuendani vitu vingi hasahasa misimamo ya kisiasa. Hili lichumba langu kumbe niliuaji kabisa! Nimegundua hili baada ya kulala kwa shujaa wa Afrika-JPM.

Nimegundua lichumba langu lilifurahia kufa kwa JPM. Nimegundua hili baada ya kusoma komenti zake kadhaa kwenye uzi rasmi uliotoa taarifa ya kifo cha JPM.

Nimekuja kugundua kuwa kuna mjomba wake alitumbuliwa kipindi kile cha vyeti feki ndio sababu limefurahi.

Just imagine, kama mtu kweli alikuwa na cheti ambacho sio halali kwanini asitolewe alipokuwa?

Baadhi ya ndugu zangu na washikaji wamenishauri kuwa niachane nae na mimi nimekubali kwa moyo mmoja maana huyu manzi ana sapoti mambo ya kijinga kuna siku ntaletewa mtoto feki nisipokuwa makini.

Bora nimeepuka balaa!

FUNZO: Oa mtu mnayeendana naye katika kila nyanja.

Wenu ktk JF,
King Nebu.
Bwana Harusi Mtarajiwa 2035.
 
Back
Top Bottom