Zak Malang
JF-Expert Member
- Dec 30, 2008
- 5,404
- 242
Ilani ya CCM yadanganya
Ilami ya uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi (CCM) ya mwaka 2010 imesheheni takwimu zinazoikinzana, imegundulika.
Katika ilani hiyo, ambayo anatumia mgombea Jakaya Mrisho Kikwete kuomba ridhaa ya kuendelea na urais, inaelezwa kuwa uchumi umekua kutoka asilimia 4.5 mwaka 2005 hadi asilimia 6.7 mwaka huu.
Lakini takwimu za serikali na washirika wake – Benki ya Dunia (WB) na Shirika la Fedha Duniani (IMF) zinaonyesha kuwa kiwango cha asilimia 6.7 kilifikiwa mwaka 2005 na siyo mwaka huu.
Hata kiwango cha asilimia 4.5 ambacho inadaiwa ndicho utawala wa kikwete ulianza nacho mwaka 2005, hakipo, kwani tayari wakati huo, serikali iliyokuwa inamaliza ngwe yake ilikuwa tayari imefikia asilimia 6.7.
Kwa hiyo, ilani ya uchaguzi ya CCM mwaka huu ilipaswa kuonyesha utendaji wa serikali – kufaulu au kushindwa – kuanzia asilimia 6.7 kwenda juu au kurudi chini. Haifanyi hivyo.
Ripoti ya WB ya mwaka 2007 kuhusu biashara na uchumi nchini ilisema, "…..uchumi wa Tanzania ulikuwqa ukikua kwa wastani wa asilimia tano hadi sita katika kipindi cha kuanzia mwaka 1995 hadi 2005.
Basil Mramba, aliyekuwa waziri wa Fedha katika serikali ya Mkapa, aliuambia mkutano wa mwisho wa Bunge la bajeti (2005) mjini Dodoma, kwamba "uchumi wa Taifa umekua kwa asilimia 6.7."
Alisema, "mheshimiwa Spika, utawala wa Awamu ya Tatu umepata mafanikio makubwa ya kiuchumi. Kwa mfano, uchumi umekua kutoka asilimia 4.2 mwaka 1996 hadi asilimia 6.7 mwaka 2005."
Kwa mantiki hii, miaka mitano ya utawala wa Kikwete imekuwa ya makitaimu; bado uchumi uko palepale alipouacha rais mstaafu Benjamin Mkapa. Hii ina maana Kikwete ameshindwa kuinua uchumi wan chi……..
Habri zaidi katika Mwanahalisi la leo.
Anajua fika mamilioni ya mambumbumbu anaotaka wamrudishe mjengoni hawajui chochote -- kitu cha uongo au cha kweli. Wao wamepumbazwa na sura tu!!!!!!
Ilani ya CCM yadanganya
Ilami ya uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi (CCM) ya mwaka 2010 imesheheni takwimu zinazoikinzana, imegundulika.
Katika ilani hiyo, ambayo anatumia mgombea Jakaya Mrisho Kikwete kuomba ridhaa ya kuendelea na urais, inaelezwa kuwa uchumi umekua kutoka asilimia 4.5 mwaka 2005 hadi asilimia 6.7 mwaka huu.
Lakini takwimu za serikali na washirika wake Benki ya Dunia (WB) na Shirika la Fedha Duniani (IMF) zinaonyesha kuwa kiwango cha asilimia 6.7 kilifikiwa mwaka 2005 na siyo mwaka huu.
Hata kiwango cha asilimia 4.5 ambacho inadaiwa ndicho utawala wa kikwete ulianza nacho mwaka 2005, hakipo, kwani tayari wakati huo, serikali iliyokuwa inamaliza ngwe yake ilikuwa tayari imefikia asilimia 6.7.
Kwa hiyo, ilani ya uchaguzi ya CCM mwaka huu ilipaswa kuonyesha utendaji wa serikali kufaulu au kushindwa kuanzia asilimia 6.7 kwenda juu au kurudi chini. Haifanyi hivyo.
Ripoti ya WB ya mwaka 2007 kuhusu biashara na uchumi nchini ilisema, ..uchumi wa Tanzania ulikuwqa ukikua kwa wastani wa asilimia tano hadi sita katika kipindi cha kuanzia mwaka 1995 hadi 2005.
Basil Mramba, aliyekuwa waziri wa Fedha katika serikali ya Mkapa, aliuambia mkutano wa mwisho wa Bunge la bajeti (2005) mjini Dodoma, kwamba uchumi wa Taifa umekua kwa asilimia 6.7.
Alisema, mheshimiwa Spika, utawala wa Awamu ya Tatu umepata mafanikio makubwa ya kiuchumi. Kwa mfano, uchumi umekua kutoka asilimia 4.2 mwaka 1996 hadi asilimia 6.7 mwaka 2005.
Kwa mantiki hii, miaka mitano ya utawala wa Kikwete imekuwa ya makitaimu; bado uchumi uko palepale alipouacha rais mstaafu Benjamin Mkapa. Hii ina maana Kikwete ameshindwa kuinua uchumi wan chi ..
Habri zaidi katika Mwanahalisi la leo.
Kikwete anadanywa katika mambo madogo tu ambayo hayahitaji kutumia nguvu nyingi ya kufikiri, itakuwa haya ya kuchambua kwa kina ukuaji wa uchumi wa Nchi! Japo hata katika hili hatumsamehe kwa sababu ana wataalamu wa sekta zote wanalipwa na kodi za wananchi maskini ambao inawabidi wakaze mikanda ili waweze kulipa kodi.
Hata mzee wa kijijini ambaye hajasoma hata darasa moja hadanywi mara nyingi namna hii katika masuala yahusuyo familia yake na vitegemezi vyake. Nina mashaka na elimu ya JK, hivi kweli alifika Chuo Kikuu na kufuzu kwa kichwa chake au alibwewa bwebwa.
Lakini inawezekana hili la ukuaji wa uchumi amegeuza namba hizo makusudi ili asiabike. Kama ukuuji wa uchumi 2005 aliukuta 6.7, na kaurudisha hadi 4, atajiteteaje? Tuna bahati mbaya sana kuwa na kiongozi wa ngazi ya juu wa namna yake. Kwa vyovyote wajanja walimsoma ndo maana rasilimali za nchi zinaibwa mchana kweupe.
Mwaka huu inafaa kuondokana na mzigo wa viongozi wasio na 'akili', ambao wanaweza kutuletea matatizo makubwa sio kwa vile wanataka bali kwa vile ni wajinga na hudanganyika kirahisi. JK, simtukani, ila ni mjinga. Mtu mzima mwenye akili zako huwezi kudanganywa mara nyingi namna hii kama sio mjinga.
Kwa kwakeli wanaJF, tusaidiane kuwahamasisha watanzania ili waelewe hatari kubwa inayoinyemelea nchi yetu ikiwa tutaendelea kuufumbia Macho ujinga wa viongozi wetu unaoendelea kuifilisi nchi.
Itakuwa baraka kwa nchi yetu ikiwa baada ya 31.10 JK ataitwa rais mstaafishwa kwa 'kura' za wananchi wa awamu ya Nne.
Kura zote za Rais kwa Dr. W. P. Slaa, na wagombea wa Chadema kwa Ubunge na Udiwani.