Ikulu kesho: Ngoma maua vigelegele kuendeleza dhana ya "WAMEULA"

KALABASH

JF-Expert Member
Jan 26, 2011
493
206
Mh. ZITTO kanena na mimi nanena kuwa hakuna kukusanyika ikulu kesho jumatatu tarehe 7 kwa madhumuni ya kushangilia walioteuliwa kuwa mawaziri. Kama kweli tunaamini hawa tumewabebesha mzigo mzito wa kumsaidia rais kutatua matatizo mazito yanayowakabili watanzania basi sehemu muafaka ni makanisani na misikitini kuwaombea ili wafanikishe hayo. Watu hupongezwa wanapofaulu mitihani au wanapooa au kuolewa na mengineyo kama hayo.Lakini hatupongezi makamanda wanapoteuliwa kwenda frontline vitani kwenye mapambano. Tunapoendekeza utamaduni huu ulioanza hivi karibuni wa mikukusanyiko ya ndugu jamaa na marafiki pale Ikulu kuimba na kusema hongera "UMEULA" tusianze tena kulalamika wateule hao wanapofanya kweli na kuanza "KULA" Nawasilisha.
 
Back
Top Bottom