Ijue tofauti kati ya HESLB na TCU

Ijue tofauti kati ya HESLB na TCU

madede jr

Member
Joined
Aug 10, 2016
Posts
10
Reaction score
1
IJUE TOFAUTI KATI YA BODI YA MIKOPO YA WANAFUNZI WA ELIMU YA YUU (HESLB) NA TUME YA VYUO VIKUU TANZANIA (TCU)

Waungwana nawasalimu

Kumekua na mkanganyiko mkubwa kwa baadhi ya watu /wanafunzi kushidwa kutofautisha kati ya Bodi ya Mikopo wa Wanafunzi wa Elimu ya Juu (heslb) Na Tume ya VVyuo Vikuu Tanzania (TCU) Nakufikia tatua ya kupeleka malalamiko /matatizo ya TCU- HESLB na ya HESLB –TCU. Kwa ufupi ni hivi;

Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu ni chombo cha serkalii kilicho anzishwa kwa sheria Na. 9 ya mwaka 2004 ambayo malengo yake ni kutoa mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu na kukusanyamadeni kwaajili ya kukopesha wanafunzi wengine wahitaji.Baadhi ya majukumu ya Bodi ni pamoja nahaya;

  • Kuandaa mpango sahihi wa utambuzi wa wanafunzi wahitaji wa mikopo ya wanafunzi wa elimu ya juu

  • Kumshauri waziri katika mambo yahusuyo sera ya utoaji na ureshaji wa mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu

  • Kutunza kukumbukumbu za wanafunzi walio nufaikana mkopo/kopeshwa na bodi

  • Kusimamia na kuendesha taratibu zote za utoaji na urejeshaji wa mikopo iliyotolewa kwa wanufaika
Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) ni shirika lililoanzishwa tarehe 1, Julai, 2005 chini ya Sheria ya Vyuo Vikuu Na. 7 ya mwaka 2005 kwa madhumuni ya kuhakikisha elimu ya juu bora nchini Tanzania. TCU iliyochukua majukumu ya Baraza la Ufumbuzi Rasmi wa elimu ya juu (lililoanzishwa mwaka 1995) pia hufuatilia na kusimamia usimamizi wa jumla na utendaji wa taasisi za elimu ya juu. Kwa ufupi, majukumu ya TCU yanaelezwa kwa muhtasari kama yafuatayo:

•Uhimizaji wa kubadilisha maarifa/elimu kwa njia ya kuunganisha kimtandao Vyuo Vikuu na Vyuo vya Vyuo Vikuu;

•Usajili na utambuzi rasmi wa Vyuo Vikuu na Vyuo vya Vyuo Vikuu;

•Uthibitishaji wa programu za kitaaluma, uthibitishaji na uratibu wa udhahili wa wanafunzi;

•Ufuatiliaji na udhibiti wa elimu bora Vyuo Vikuu na Vyuo vya Vyuo Vikuu;

•Ukusanyaji na usambazaji wa taarifa/data kuhusu elimu ya juu.



Na wasilisha.
 
Back
Top Bottom