Ndano
Member
- Jan 8, 2017
- 17
- 18
*IJUE (MAANA YA) NOTIFICATION (TAARIFA YA KOSA)*
Madereva wengi sana wamekuwa wakiandikiwa notification, lakini bila kujua notification ni nini.
Leo tutazungumzia notification, na kinachotakiwa kufanywa baada ya kuandikiwa notification
*Notification* ni taarifa ya kosa na ndio maana kichwa chake cha habari kimeandikwa *NOTIFICATION OF TRAFFIC OFFENCES.*
(Yaani taarifa ya makossa ya barabarani.)
Karatasi au fomu ya notification imetengenezwa chini ya kifungu cha 95(10) cha Sheria ya Usalama Barabarani(RTA), Sura ya 168, na hutolewa na askari wa usalama barabarani chini ya kifungu cha 95(3) cha sheria tajwa hapo juu.
Fomu hii ni waraka wa serikali ambao umechapishwa kwenye gazeti la serikali nambari 257 la mwaka 2011.
Katika fomu za polisi fomu hii ni nambari 101, yaani PF101 (kama ambavyo mmezizoea fomu nyingine kama PF3-Police form no.3. Kithibitisho kingine kinachoonesha kuwa notification ni taarifa ya kosa ni maneno *"To…"* yanayoanza mwanzo kabisa baada tu ya kichwa cha habari kuonesha kwamba taarifa inatolewa *"Kw..."* (jina la mtuhumiwa)
Hii inamaana fomu hii unaweza kutumiwa nyumbani kwako kupitia anwani yako ya posta, au kwa mtu kuileta, au kupewa mkononi au kuikuta imebandikwa kwenye gari lako (kama wanavyofanya watu wa parking) na askari kaondoka.
Kilichomo kwenye notification (Content)
*1*. Notification yoyote itakuwa na jina na anwani ya mtuhumiwa aliyefanya kosa.
*2*. Itataja aina ya kosa na maelezo ya kosa hilo kwa ufupi pamoja na kifungu cha sheria kilichovunjwa.
Aina ya kosa lililofanywa ipo nyuma ya ile form na.101, lakini pale juu askari ataandika tu, mfano, kosa na.23. *Ukitaka kujua kosa namba 23 ni lipi na linaangukia kifungu kipi cha sheria geuza nyuma ile fomu*
*3*. Askari anatakiwa si tu aandike namba ya kosa bali pia ataje kosa husika,mf. Kupita kwenye taa nyekundu, kuovateki vibaya nk. Bahati mbaya sana askari wetu ni au hawajui au ni wavivu kusoma makossa wakayajua. Maana mara nyingi hukimbilia tu kuandika kosa na.23. Kosa namba 23 ni kifungu cha 113 cha RTA.
Katika RTA kifungu na. 113 kinahusu adhabu za jumla kwa makossa ya barabarani. Adhabu hizi ni zile ambazo hazina kifungu maalumu cha sheria.
Kwa mfano kosa la speed huwezi kuandika No.23 ukimaanisha ni kosa dhidi ya kif.113, kosa la speed lina kifungu chake na.51, na adhabu zake kif.63 cha sheria.
Kwa nini nasema askari wanafanya makossa, wanafanya makossa kwakuwa ukiandika kif.23 halafu mtuhumiwa akachagua kwenda mahakamani, unampa shida mwendesha mashataka namna ya kutengeneza mashataka kwani form na.101 itakuwa sehemu ya ushahidi. Matokeo yake mtuhumiwa anaweza kupata adhabu ndogo kuliko anavyostahili au akashinda kesi.
*4*. Itakuwa na sehemu ya mtuhumiwa kukubali kosa.
Iwapo mtuhumiwa atakubali kosa basi anatakiwa kujaza sehemu B ya fomu na kisha ndani ya siku 10 (tangu ulipoletwewa au kupewa hiyo fomu)kuipeleka fomu hiyo pamoja na faini yake kwa askari aliyemuandikia hiyo notification na kisha askari kuipeleka kwa Mkuu wa Polisi Wilaya (OCD) au Mkuu wa Kituo cha Polisi(OCS).
*5*. Itakuwa na sehemu ya mtuhumiwa kukataa kosa.
Ikiwa mtuhumiwa atakataa kosa basi atajaza sehemu A ya fomu na kisha ndani ya siku zilizotajwa kuituma kwa OCD au OCS.
*6*. Faini kwa makossa ya sehemu ya kwanza(nyuma ya notification) ni shilingi 30,000
Hivyo basi, ukisimamishwa na askari barabarani na akataka kukuandikia notification kwa kosa, iwe unakubali au unakataa kosa kubali kusaini, cha msingi tu angalia unasaini wapi.
Ukisaini part A maana yake unakataa kosa, na ukisaini part B ambako ni kule chini kabisa ya fomu maana yake unakubali kosa, na unatakiwa ulipe.
Hata hivyo kuna utata kuhusu muda wa kufanya malipo.
Wakati sheria katika kifungu cha 95 inatoa siku 28, notification inatoa siku saba(7) tu.
*Notification* ni sheria ndogo ya sheria mama(RTA) na kwa mujibu wa sheria sheria ndogo haipaswi kukinzana na sheria mama, na kukitokea ukinzano huo sheria ndogo inakuwa batili (Void) kwenye kile kisehemu inachokinzana.