Ijue kampuni ya simu ya Tecno, ondoa shaka kuhusu simu feki

Eric Mkomoya

Member
Oct 10, 2014
55
56
834317620_5_644x461_brand-newfactory-sealed-original-tecno-camon-c8-smart-phone-nairobi.jpg


Kampuni ya simu ya Tecno ni moto mkubwa katika kampuni kubwa mama ya Transsion Holdings ambayo makao yake makuu yapo nchini Uchina, kampuni hii ilianzishwa ikiwa July 2006.

Kampuni ya simu ya Tecno imekua na kusambaa katika nchi mbali mbali duniani ikiwemo India, Bangladeshi, Dubai, Nigeria, Misri Kenya hata kuweza kutengeneza kiwanda katika Nchi ya Ethiopia ambacho kinasaidia bidhaa za kampuni hiyo katika nchi za barani afrika.

Kampuni ya simu ya Tecno imeweza kufanya vizuri katika soko la simu janja (smartphone) na simu za kawaida (feature phones) katika nchi za Afrika kwasababu inajali soko la afrika kwa kuweza kutengeneza simu zenye uwezo mzuri katika mazingira ya nchi za afrika simu zenye uwezo wa kukaa na umeme muda mrefu, rahisi kutumia kwa watu vwa aina zote, na kwa upande wa simu janja (smartphone) kampuni hii ya TECNO MOBILE imeweza kuleta mapinduzi ya bei za simu janja kwa kuuuza bei kwa bei inayoendana na kipato cha waafrika wengi lakini zikiwa na mahitaji yote yanayotakiwa katika simu janja.

Baada kuijua Kampuni hii ya simu ni kubwa, unaweza jiuliza kwanini wauze simu feki? Jibu ni HAPANA TECNO MOBILE hawauzi simu feki ila wanauza simu kwa bei rahis mara nyingi watu hudhani cha bei rahisi ni kibaya la hasha, hii imekuja kutokana ana mipango ya kampuni yenyewe kuuza bidhaa zao kwa bei inayoendana na kipato cha wateja wao.

Kampuni hii ambayo ina undugu wa karibu na simu za Itel, Infinix na kampuni ya kutoa huduma baadaa ya mauzo kwa wateja ya CARLCARE International, inawatoa hofu wateja wake kwamba simu zao zitafungiwa na mamlaka ya mawasiliano Tanzania (TCRA) , ifikapo mwezi wa sita 2016 kwamba simu za kampuni ya TECNO MOBILE zitakua salama na watumiaji wake wawe na Amani tu na kuimini kampuni hii inayowajali wateja wake.
 
Back
Top Bottom