ManiTek TV
JF-Expert Member
- Jun 3, 2011
- 410
- 159
[h=2]12/03/2013
Dijit: App itakayobadili iPhone Yako[/h]
Dijit si app mpya kwenye AppStore lakini ni app ambayo itaifanya iPhone, iPad au iPod Touch yako iwe ni zaidi ya simu. Dijit ni app ya rimoti, ambapo hufanya kazi badala ya rimoti zote za gajeti mbali mbali zinazotumia rimoti. Utahitaji kutumia pesa ya ziada japokuwa app hii ni bure, pesa ya ziada inatokana na ukweli kwamba unahitaji kununua kifaa kinachojulikana kama Beacon kilichotengenezwa na kampuni ya Griffin Technology.
Beacon inauzwa kama laki moja hivi, lakini utakaponunua, rimoti zote unafungia kwenye kabati iwapo unatumia gajeti yoyote ya iOS yaani iPad, iPhone au iPod Touch. Gajeti yako ya iOS huunganishwa na Beacon kwa teknolojia ya bluetooth kisha unaweza kuitafuta remoti yako katika database ya Dijit ambayo ina maelfu ya rimoti. Hivyo inafanya matumizi kuwa rahisi kabisa na utaratibu wa kutafuta ni rahisi kwa vile unachotakiwa ni kuingiza jina gajeti yako (brand) aina ya gajeti (TV, DVD, Receiver n.k) kisha unafuata maelekezo kui-programu.
Ikiwa unatumia kifaa cha kichina ambacho hakina hata brand upo uwezekano kuwa hakitakuwepo kwenye database ya Dijit, hata hivyo bado utaweza kuitumia gajeti yako kwa kuisomasha Dijit kifungo kimoja kimoja kwa kutumia rimoti yako ya asili, lakini ukishai-programu mara moja tu huna haja ya kurudia tena kazi hiyo kwa vile inahifadhiwa kwenye kumbu kumbu ya dijit yako. Gharama nyingine ambayo ni ndogo tu ni kwamba Griffin inatumia betri mbili aina ya AA za kawaida tu, lakini ni vyema kuwa na betri za reachargeable kwani griffin humaliza betri haraka kwa uzoefu wetu labda uwe unatoa betri kila baada ya kuitumia.
Tahadari ni kwamba kama rimoti imepotea na kifaa chako hakimo kwenye database ya dijit basi rimoti hii si suluhisho kwa sababu ili ifanye kazi na kifaa (TV, box, DVD n.k) chako ni lazima ama kifaa chako kiwe kwenye database yao au uwe na rimoti original ili u-programme dijit yako angalau mara moja kwenye kila kifaa cha iOS utakachokitumia.
Pia Dijit inakuruhusu kupanga mwenyewe ni gajeti gani unatumia na hivyo kukuunganishia gajeti hizo kwenye rimoti moja katika kile wanachokiita activity. Yaani kwa mfano kama unatazama DVD basi unapanga activity ya DVD na hivyo Dijit inakupa rimoti ambayo inakuwa na DVD, TV pamoja na Home Theatre yako, na kama unataza TV kwa kutumia dishi, basi unaweka activity itakayokuwa na rimoti ya TV na Receiver yako.
Pia unaweza kupanga kwenye chumba fulani kuna vifaa gani na hivyo unapochagua chumba, kama vile chumba cha kulala au sebleni digit inakupa rimoti za chumba kinachohusika tu.
Dijit pia inapatikana kwenye Android lakini mnunuaji awe na tahadhari kwenye suala la Beacon, kwa vile beacon ya iOS haiingiliani na Beacon ya Android. Vile vile kuna app nyingi zinazoweza kuifanya simu yako iwe rimoti kamili, lakini zote huwa lazima ziambatane na gajeti (kifaa) nyingine kama ilivyo Beacon kwa dijit.
Source: Gajetek - Gajet na Teknolojia
Twitter: gajetek