MotoYaMbongo
JF-Expert Member
- Jan 7, 2008
- 2,146
- 886
Walimu wanateseka, wananyanyasika, Wamepanda madaraja tokea 2014 hadi leo hii naandika uzi huu bado hawajabadilishiwa mshahara, wamefatilia hadi wamechoka, kila siku wanaambiwa wapeleke nyaraka, wanapeleka halafu wanasubiri ikifika mwisho wa mwezi hola! Imefika mahali sasa wengine wanafatilia Dar Utumishi, huko wanaambiwa taarifa hazijatumwa, Walimu Urambo wanapaza sauti Waziri husika okoa jahazi, Urambo inakufa kielimu kwa uzembe wa Ofisi ya Utumishi, Tumbua majipu yameiva.