1000 digits
JF-Expert Member
- Oct 16, 2012
- 6,865
- 9,053
Nimekua nikijiuliza hivi wenzetu wazungu wanatuonaje sisi waafrika pale wanapoona hata mambo madogo na ya muhimu yanawashinda kabisa wataalam wetu walioaminiwa na serikali na kupewa majukumu muhimu kwenye jamii?
Bila shaka kabisa yale yaliyopo kwenye mji mdogo wa Mambo ni kati ya mambo yanayosababisha wazungu watudharau na kutuona kama watu wasio na akili au wasioweza kutumia akili zao sawasawa.
Ni ajabu kabisa kuona wananchi zaidi ya 10,000 wakisambaziwa maji machafu kabisa kama yale ya mifereji wakati wa mvua.
Hivi ni kweli kama wataalam wa maji wamekosekana wa kuweza kubuni namana rahisi ya kuyasafisha maji yanayosambazwa katika mji wa Mombo?
Kwa nini Mtaalam aliyeaminiwa na serikali awasambazie binadamu maji machafu?
Hivi ni nani kati ya hao wakuu wa idara hiyo kuanzia mameneja wao anayeweza kuwapa hata ng'ombe wake maji kama yale yanayotoka bombani na uchafu na matope yale?
Juzi nimeshindwa kula hata embe baada ya muuzaji kunionyesha maji aliyokua anayatumia kuoshea maembe na kudai eti amechota bombani.
Bila kuchelewa nilikwenda sehemu yenye bomba na kujaribu kufungua bomba na kushuhudia maji machafu na meusi kama maji ya mitaroni yakitoka.
Nilijiuliza maswali mengi lakini nikapata jibu moja tu kuwa sisi wa afrika hatuthamini kazi za ubunifu. Ifikie mahali mtu akiomba kazi ajieleze kuwa ataifanyia nini jamii na sio jamii itamfanyia nini!! Bili za maji kila mwezi halafu mtu anapewa maji machafu. Sio jambo jema kabisa kwa mamlaka husika.
Wasisubiri mpaka waziri mkuu afike hapo awatumbue ndipo waanze kusema kuwa wanaonewa.
Kwa nini awaache watu walioajiriwa na serikali lakini hawana ubunifu wa kukabiliana na changamoto ndogo kabisa kama hizo?
Nadhani kazi ya idara ya maji ni pamoja na kuhakikisha wananchi wanapata maji safi na salama.
Karne hii lakini bado wataalam wetu kwenye idara ya maji wanashindwa kuja na mbinu rahisi za kusafisha maji ya mito au hata ya mvua ili binadam wapate maji yanayofaa kwa matumizi ya majumbani mwao?
Sasa ni wakati wa idara ya maji kuwa wabunifu na kuanzisha miradi mingi midogo midogo ya maji safi na salama na kuwasambazia wananchi kama huduma na pia kama miradi ya kuongeza pato la nchi na idara hizo.