Idadi ya watumishi hewa yafikia 248, Mkuu wa Mkoa Paul Makonda amsimamisha kazi Afisa Utumishi Ilala

Donatila

JF-Expert Member
Oct 23, 2014
7,563
21,665
Mkuu wa Mkoa Dar, Paul Makonda amemsimamisha kazi Afisa Utumishi wa Manispaa ya Ilala kwa kutowagundua watumishi hewa 11.

Hadi leo katika Mkoa wa Dar wamefikia watumishi hewa 248 wamebainika Dar, waleta hasara ya Shilingi bilioni 3.7.

Tarehe 2 Mei Mkuu wa Mkoa wa Dar, Paul Makonda aliwapa kiapo cha kazi wakuu wa Idara zote za jiji la Dar pamoja na maafisa Utumishi wa halmashauri za jiji wasaini kiapo cha kazi mbele ya Mkuu wa mkoa na wakuu wa wilaya baada ya kubainika kutoa taarifa zisizo za kweli dhidi ya kuwepo kwa watumishi hewa katika idara zao baada ya kubainika watumishi hewa wengine 209 katika Uchunguzi wa Siku chache zilizopita.

Miongoni mwa masharti yaliokuwapo katika kiapo hicho ni kwamba iwapo ikigundulika kuwapo kwa watumishi hewa katika idara husika baada wiki moja, Afisa utumishi au mkuu wa idara hiyo atalipa gharama za mishahara iliyopotea, kushitakiwa kwa uhujumu uchumi, kuachishwa kazi lakini pia kufikishwa mahakamani.

Hatua ya kusaini na kula kiapo inatokana na baadhi ya wakuu wa idara pamoja na maafisa Utumishi katika jiji la DSM kudaiwa kutoa taarifa za uongo kwa Mkuu wa mkoa Paul Makonda na wakuu wa wilaya za jiji hilo baada ya kutoa idadi ndogo ya watumishi hewa kwa mkoa wa dsm ambao walikuwa 74 tu, huku uhakiki wa sasa uliofanywa na tume maalum ukibaini watumishi hewa 209 ambao wametafuna kiasi cha takribani shilingi bilion 2.7
 
Mkuu wa Mkoa Dar, Paul Makonda amemsimamisha kazi Afisa Utumishi wa Manispaa ya Ilala kwa kutowagundua watumishi hewa 11
Anaacha kupambana na Afisa Ugavi wa Jiji ambaye ni bonge la fisadi anashobokea hivyo vidagaa. Huyo afisa ugavi alikuwa anakusanya mapato ya vyoo vya ubungo kupitia mume wake wanakula pamoja na sehemu nyingine za maegesho lakini anadanganya watu anafanya biashara ya nguo nyambaf
 
Mkuu wa Mkoa Dar, Paul Makonda amemsimamisha kazi Afisa Utumishi wa Manispaa ya Ilala kwa kutowagundua watumishi hewa 11.

Tarehe 2 Mei Mkuu wa Mkoa wa Dar, Paul Makonda aliwapa kiapo cha kazi wakuu wa Idara zote za jiji la Dar pamoja na maafisa Utumishi wa halmashauri za jiji wasaini kiapo cha kazi mbele ya Mkuu wa mkoa na wakuu wa wilaya baada ya kubainika kutoa taarifa zisizo za kweli dhidi ya kuwepo kwa watumishi hewa katika idara zao baada ya kubainika watumishi hewa wengine 209 katika Uchunguzi wa Siku chache zilizopita.

Miongoni mwa masharti yaliokuwapo katika kiapo hicho ni kwamba iwapo ikigundulika kuwapo kwa watumishi hewa katika idara husika baada wiki moja, Afisa utumishi au mkuu wa idara hiyo atalipa gharama za mishahara iliyopotea, kushitakiwa kwa uhujumu uchumi, kuachishwa kazi lakini pia kufikishwa mahakamani.

Hatua ya kusaini na kula kiapo inatokana na baadhi ya wakuu wa idara pamoja na maafisa Utumishi katika jiji la DSM kudaiwa kutoa taarifa za uongo kwa Mkuu wa mkoa Paul Makonda na wakuu wa wilaya za jiji hilo baada ya kutoa idadi ndogo ya watumishi hewa kwa mkoa wa dsm ambao walikuwa 74 tu, huku uhakiki wa sasa uliofanywa na tume maalum ukibaini watumishi hewa 209 ambao wametafuna kiasi cha takribani shilingi bilion 2.7

Anaitwa nani huyo Afisa?
 
RC wa mkoa wa dar amemsimamisha kazi Afisa utumishi wa manispaa ya ilala kwa kueleza kuwa wafanyikazi 11 hawafahamiki,
Mytake :hii fukuza fukuza ya watumishi wa Serikali itageuka kuwa tatizo sasa Serikali kwani Serikali inaendelea kulipa mshahara watumishi wengi waliosimamishwa kwa muda mrefu. Hebu niwape kwa ufupi orodha ya maafisa waliosimamishwa kazi toka mwaka juzi ambao sanaendelea kulipwa mshahara bila kazi :
1.afisa utumishi aliyesimamishwa mwaka juzi kwa kisingizio ati amevuruga uvhaguzi wa mitaa.
2. Mhandisi kwa tuhuma za gorofa kuanguka.
3.afisa mipango miji kwa tuhuma za viwanja.
4. Afisa mifugo.
5..........
Endeleza orodha
 
Habari ndo hiyo
 
Attachments

  • IMG-20160509-WA0006.jpg
    IMG-20160509-WA0006.jpg
    46.7 KB · Views: 83
It is a good idea ya kupambana na wafanyakazi hewa, hili nawaunga mkono wote ila aproach yake kwa baadhi wa wakuu wa mikoa itatuingizia taifa hasara.

Haya ndio anayasema Lissu ukomo wa wakuu wa mikoa kisheria, mkuu wa mkoa hana mamlaka ya kisheria kusimamisha au kufukuza watumishi wa umma lakini kwa kutafya sifa wakuu wa mikoa na wilaya hujipa mamlaka yasiyo yao kisheria na watuhumiwa wakienda mahakamani wanashinda kesi alafu tunaanza kusema mahakamani kumejaa rushwa kwa nini kila kesi ya serikali tunashindwa.

Wakuu wa mikoa na wateule wengine wa rais wafuate sheria wasije kutuingiza matatizoni kuliko hata hao watumishi hewa.
 
RC wa mkoa wa dar amemsimamisha kazi Afisa utumishi wa manispaa ya ilala kwa kueleza kuwa wafanyikazi 11 hawafahamiki,
Mytake :hii fukuza fukuza ya watumishi wa Serikali itageuka kuwa tatizo sasa Serikali kwani Serikali inaendelea kulipa mshahara watumishi wengi waliosimamishwa kwa muda mrefu. Hebu niwape kwa ufupi orodha ya maafisa waliosimamishwa kazi toka mwaka juzi ambao sanaendelea kulipwa mshahara bila kazi :
1.afisa utumishi aliyesimamishwa mwaka juzi kwa kisingizio ati amevuruga uvhaguzi wa mitaa.
2. Mhandisi kwa tuhuma za gorofa kuanguka.
3.afisa mipango miji kwa tuhuma za viwanja.
4. Afisa mifugo.
5..........
Endeleza orodha

Si ungemalizia tu!
 
It is a good idea ya kupambana na wafanyakazi hewa, hili nawaunga mkono wote ila aproach yake kwa baadhi wa wakuu wa mikoa itatuingizia taifa hasara.

Haya ndio anayasema Lissu ukomo wa wakuu wa mikoa kisheria, mkuu wa mkoa hana mamlaka ya kisheria kusimamisha au kufukuza watumishi wa umma lakini kwa kutafya sifa wakuu wa mikoa na wilaya hujipa mamlaka yasiyo yao kisheria na watuhumiwa wakienda mahakamani wanashinda kesi alafu tunaanza kusema mahakamani kumejaa rushwa kwa nini kila kesi ya serikali tunashindwa.

Wakuu wa mikoa na wateule wengine wa rais wafuate sheria wasije kutuingiza matatizoni kuliko hata hao watumishi hewa.
Kusimamishwa Kazi Na Kufutwa Kazi Ni Vitu Viwili Tofauti.
RC Anaweza Kumtumia Mwenye Mamlaka Ya Kumsimamisha Kazi Muhusika Lakn Kwa Shinikizo Lake Lililojaa Ushahidi.

Mh.Lissu Anaongea Tu Ili Kuvuta Umakini Wa Watz Ili Chama Chake Kionekane Makini Lakn Si Rahisi Umfukuze Kazi Mfanyakaz Wa Serikali Kienyeji, Vivyo Hivyo Kusimamishwa Kaz Naweza Kutamka Mimi Nisiye Na Mamlaka Lakn Barua Ya Kusimamishwa Ikaandikwa Na Mwenye Mamlaka.

Wanasiasa Wanatupotosha Kwa Mengi Jaman, Ebu Tupime Kauli Zao Maana Yote Walokuwa Wanayaongea JPM Kajaribu Kuyafanya Kwa Vitendo Tena Kwa Muda Mfupi, Sasa Hivi Wanahaha Nini Waseme So Wamejikuta Wanatafuta Hoja Zisizo Na Mashiko Kukuza Chama Chao.

Juzi Namsikia Mh.Zitto Anasema Mawaziri Hawajapewa Instrument Ambayo Ndiyo Power.
Hivi Kuna Nguvu Kubwa Tofauti Na Ile Iloandikwa Kikatiba Kwamba Waziri Lazima Awe Mbunge Na Atateuliwa Na Rais Kisha Ataapishwa.

Jaman Mimi Nawapenda Wapinzani Lakn Huku Waendako Kupingana Na JPM Kwa Misingi Isiyo Ya Kizalendo, Wananifanya Niwaone Hawana Nia Ya Kuje Nchi Bali Kushindana Kisiasa.
 
Nimegundua una uelewa mfinyu wa mambo ya kisheria.
 
yeye mwenye uelewa ameingia chaka akikujibu nami niite nijifunze kwake
Mimi Mtu Akinidharau Huwa Nafurahi Lakn Namwona Hana Uwezo Kama Haji Kwa Hoja Badala Yake anakuja Kwa Maneno Ya Mtaani.

Aje Hapa Na Hoja Wapi Mimi Mfinyu Ili Twende Sawa.

Mkuu Wa Mkoa Au Mfanyakaz Mwingine Anaweza Kutoa Mapendekezo Ufukuzwe Au Usimamishwe Kazi Lakn Atakayeandika Hiyo Barua Ya Kufukuzwa Au Kusimamishwa Si Yeye Kama Sheria Haijampa Mamlaka.

Lakn Pia Sheria Inaweza Kumpa Nguvu Ya Kumsimamisha Kazi Fulani Lakn Isimpe Nguvu Ya Kumfukuza.

Tz Tunashindwa Kutofautisha Kati Ya Kusimamishwa Kazi Na Kufukuzwa Kazi.

Presdential Apointee Wote Wanafukuzwa Kazi Na Rais Kuhusu Kusimamishwa Siwez Kulionelea Ila Najua Rais Anateua Jaji Lakn Hawez Kumfukuza, Tofauti Kabisa Na Mawaziri, Wakurugenz, Wakuu Wa Mikoa Na Wengine Kama Hao.
 
Back
Top Bottom