Hvi tujiulize sasa hivi kuwepo ushindani usiopendelea upande wowote nafasi ya CCM iaweza kuwaje?

bendaki

JF-Expert Member
Feb 5, 2013
952
346
Ndugu wana JF,

Habari za asubuhi.

Jana niliangalia mkutano mkuu wa CCM kiukweli walijitanua kikweli kweli.

Nilimsikia Mwenyekiti wao akiagiza washinde kila uchaguzi na waongeze wanachama ili wawe wengi.

Nilijiuliza hawa CCM wanazuia wapinazani wasipige siasa kuongeza wanachama wao. Wana wawekea kila vipingamizi ili turudi chama kimoja.

Lakini nimeangalia kero za watanzania kama zina kabiliwa, hasha maisha ni magumu kweli kweli huku pesa zinakusanywa lakini wanajipendelea kwenye matumizi. Hakuna anaye wafikiria wakulima ambao ni maskini na ni 80% ya Watanzania wote.

Sasa itokee uchaguzi uwe wa haki kuanzia kampaini hadi kupiga kura na kutangazwa mshindi, CCM nafasi yake mnaiona inaweza ikawaje?
 
Kumbuka kuwa enzi za mwalimu kura za ccm zilikuwa zinapatikana huko vijijini hivyo kushinda kirahisi lakini enzi hizi za kina chakubanga kura zinapatikana kwa wingi polisi,usalama pamoja na jeshini
 
Kila wakati ni kulia lia tu, kwa nini tusijiulize maswali ya msingi pia kuwa... hivi kungekuwepo na wapinzani ambao hawakubali kununulika hali ya kisiasa saa hizi ingekuwaje hapa nchini?
 
Siyo wajibu wa CCM kulea wapinzani ingawa wapinzani ndiyo wanavyotamani. Inabidi wajizatiti wapambane ili waishi,lakini kama ni !kutegemea huruma ya green/yellow part! Mtakufa kweli.

Sent from my TECNO 7C using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom