Huzuni: Uzuri hauzai

kukukakara

JF-Expert Member
Joined
Jul 31, 2012
Posts
496
Reaction score
164
''Ni mzuri sana najijua. Nimeenea kila idara.'' Alisikika binti akiwasimulia rafiki zake; mtanashati ambaye kwa kweli asingeweza kuachwa kutongozwa na mwanaume yeyote popote akitokezea.

Ila sasa hivi naiona dunia chungu, chungu kama shubiri, aliendelea.. nililala kitandani miezi kadhaa bila ya uwezo wa kutembea baada ya kutoa mimba ya kijana aliyenitongoza nikamkubalia kwa maelewano tutakuwa mke na mme maishani. Kumbe la; hakuwa na wala hakudhamiria. Kwa kudhamiria kuolewa na kuishi na mme niliamua nikutwe na mtoto. Hivyo niliamua kuitoa mimba. Alisikika akilalama.

Matokeo yake hata baada ya kupata uwezo wa kutembea na kurudia haiba yangu ya kawaida, najiona sina maana tena duniani. Kwanza kabisa baada ya kama miezi kadhaa baada ya kupona nilishawishika na bwana moja tuanze mnahusiano. Nilisita lakini baada ya ahadi nyingi na ukaribu wa huyo bwana kimahusiano nilimkubalia. Ghafla nilijikuta kufanya nae tendo la ndoa na siku hiyo niliamsha maumivu ambayo yalinifanya nilale kitandani wiki nzima.

Doctor akaniambia mimba yako ilitoka vibaya na kuna viungo vimeumia. Hautaweza kufanya mapenzi tena kwa muda mrefu pengine sio chini ya miaka mitatu na huku ukiendelea na matibabu ya hali ya juu.

Sikuwa na jinsi bali kuufuata ushauri huu hasa nikikumbuka maumivu yaliyoweza kunisibu.

Jambo gumu: Baada ya kuendelea na maisha yangu ya kujihami na upweke wa kulazimika mara baba moja mtu mzima katokea kunipenda. Huyu kanipenda kikweli japo alinitongoza na mimi nikamkubalia bila ya kumweleza hali niliyonayo. Huyu baba akaanza kuwajibika kikweli kunihudumia, sio tu mimi hata nikimweleza matatizo ya nyumbani kwetu.

Kila akiniomba kukutana kimapenzi nilimwongopea sababu mbali mbali na hakuwa na hasira na mimi. Ila sasa hivi ameanza kuwa na mashaka na mimi na mimi sina uwongo tena wa kumdanganya. Kiukweli maumivu ninayoyapata nikirudia kitendo hiki siwezi kurudia. Ila kwa jinsi huyu baba anavyonihudumia najawa na dhamira ya ukosefu wa hali ya juu. Najuta kumpenda, najuta kumdanganya.

Je wapendwa msiniseme sana haya yanawakuta binadamu na binadamu ndio sisi. Nishaurini natamani kumwambia huyu baba ukweli. Nifanyeje kwani najua hataniamini na atajua nilikuwa namwibia tuu.

Nisaidieni mwenzenu mimi nimebaki picha tu ya msichana mrembo.

Wadogo zangu, msitoe mimba. Msijaribu kabisa. Uzuri hauzai!
 
Kweli kutoa mimba sio swala zuri hata kidogo ila wanaume pia ifike wakati mjue wajibu,msijue kufurahia sex tu bila kutathmini matokeo ya baada ya hapo
 
Nadhani wote wawili wawe Makini. Labda kama kuna swala la ubakaji. Ni mbaya sana kwa kweli
 
kwanza pole sana kwa yanayokusibu.Pili umshukuru Mungu bado ni mzima wa afya japo una matatitizo ya hapa na pale.Tatu nakushauri uombe toba kwa kitendo chako cha kutoa mimba.Mwenyezi Mungu hapendi.Nne nakwa kuwa umesema huyu Mzee anakupenda na wewe unaamin kwa dhati kwamba anakupenda na wewe unampenda,basi kaa naye kwa mahaba mueleze kwa undani kisa chako ,usifiche kitu na ikibidi muambie mfanye "medical check up".Kama ana dhamira nzuri na wewe ataelewa na atakupa jibu zuri la kukufariji kwa maisha yanayofuata.Sku zote ukweli unauma lakin unasaidia kimahusiano.Kumbuka ukiendelea kunyamaza na huku unamushawasha wa kupenda utajiletea matatizo mengine ikiwemo mgandamizo wa mawazo,kutoaminiwa na kuachika .
 
Itabidi ukachukue yatima uwalee mpaka hapo utakapojaaliwa wa kwako
 
Mwambie ukweli tu, coz kama kaweza kuhudumia family czani kama hilo tatizo ni kubwa kwake
 
he Dr alikwambia baada ya miaka 3 utaweza kubebe ujauzito?

huyo baba una malengo nae au unapita?

kama una malengo nae mwambie ukweli afu mwende hospital muongee na Dr mda ukifika mfanye pole pole na kama ni mzee na bahati nzuri ukute ana kibamia basi utamshukuru mungu
 
Matron bado unanichukia jamani?[emoji53][emoji53][emoji53]
 
Pole sana mamii... Ni vema ukamwambia huyo baba ukweli tena anaweza kukupa full support juu ya hili kama kweli anakupenda
 
Pole sana aisee,lkn ukweli humuweka MTU huru andaa mazingira yakufunguka kumueleza Mzee ukweli ukishindwa nenda nae hosp unakopata tiba
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…