asante kwa ushauri sababu mwenyewe huwa nakosa raha nakujiulza kwanini akatae kupima ina maana ananiamini mimi sana kuliko maisha thank for your advice!Jiulize, ana sababu gani ya kuogopa kupima UKIMWI kama kweli anakupenda kwa dhati na yeye pia anaipenda afya yake? Kuna kitu hapa. Fungua akili, usikubali kuingia kwenye shimo kizembe hivyo. Hataki kupima, achape lapa!
kiukwel sijawahi kufanya mapenzi ata siku 1 na yeye analijua hilo na siyo kwamba nilikuwa nambania tatizo ata kwa mda huu naweza fanya naye ila kupima ataki kabisa.
Mahusiano ni makubaliano ya watu wawili
Kama unaona amekiuka makubaliano hili ni suala la wewe either kukubaliana nae au ukatae kukubaliana nae,hata tukikupa ushauri wowote ule bado maamuzi ni yako
Hapa jiulize ni kwanini usubiri hadi ndoa?
Kwanini msipime sasahivi?
Kwanini anakataa kupima?
Kupima kuna faida gani nawewe?
Je mkishapima ndo mtakuwa waaminifu?
Baada ya kupima tutakuwa na msimamo kiasi gani?
Kusubiri hadi ndoa kuna maana gani?
Mtu akisubiri hadi ndoa ndio anakuwa muaminifu?
Pia kuna mambo ya kujiuliza kuhusu future yenu usiangalie tu kwenye ngono
Je,ana hadhi ya kuwa baba?
Je anajua ni kwanini anakuoa?
Je anajua umuhimu wa mwanamke?
Je anajua maana ya ndoa?
Je anajua uzito wa kuwa baba?
Mambo ya kujiuliza ni mengi sana cha msingi ni wewe tu kuchukua muda wa kujiuliza kama unaijua ndoa na masuala mazima yanayohusu familia!!!!!
Sipati picha wakati unaandaika haya maneno ulikuwaje he he he he ndo maana naipenda jf
Zipo story zinazomtatisha kuhusu nyie kina dada. Wapo wenye k zenye harufu kali! So unataka kumuuzia mbuzi kwenye gunia?mimi ni binti wa miaka 23 ninasoma chuo kiukweli kuna mvulana ambaye nilikuwa na mahusiano naye tangu mwaka 2007 kwenye mahusiano yetu hatukuwahi kufanya mapenzi ata siku moja hata hivyo alikuwa akiniambia tufanye ila mimi nilikuwa namzungusha nikimwambia anisubiri ila kiukweli alinivumilia na mimi niya ilikuwa kutokufanya naye mapenzi mpaka anioe ila kwasasa mwenzangu ananilazimisha sana kufanya naye wakati tulishaongea tangu hapo awali kabla ya kufanya mapenzi tupime ukimwi kwanza ndo tutafanya mapenzi lakini mwenzangu anasema hawezi kufanya katika maisha yake hilo suala la kupima kwani halina maana kwake na yeye haonyeshi suala lolote la kutaka labda kunioa.
Je huyu mwanaume ana nia gani na mimi????