Huyu ndiye mwanadamu

yuzazifu

JF-Expert Member
Oct 6, 2018
5,109
9,407
Akiwa na matatizo atahitaji aonewe huruma na kila mtu bt matatizo yakiwa kwa wengine atacheka na kukejeli.

Akiiba/kudhulumu atasema shetani alimpitia bt wengine wakiiba/kudhulumu atahukumu kua yule ni mwizi.

Akizaa mtoto ana kasoro atasema ni mipango ya Mungu bt akimuona kwa wengine atacheka na kudhihaki as if yule mtu kajiumba mwenyewe.

Mwanaye akibeba mimba yupo shule atasema maisha sio shule tu bt kwa watoto wa wengine atasema watoto hawana malezi wale au ni malaya sana watoto wale

Ukifukuzwa kazi atasema ngoja akome bt kama ni yeye atahitaji aonewe huruma na wote.

Ukimweleza shida yako ataitembeza kila kona bt yeye akikueleza atataka umtunzie siri.

Ukimuamini atakivunja kiapo cha uaminifu bt wewe akikuamini anataka ukidumishe kiapo cha uaminifu

Binadamu hasomeki kabisa hivo chukua tahadhari mapema
 
Huu ni mwaka wa uchaguzi! Hivyo tuchukue pia tahadhari ya kutowaamini Wanasiasa kwa 100%
 
Akikufanyia ubaya na kukuumiza hakimsumbui, ila ukimlipizia kisasi na kumfanyia kama alivyokufanyia yeye atalalamika. Sasa sijui kuna binadamu wenye mioyo ya nyama na wengine yao ya chuma 🤷‍♀️
 
Binadamu ubaya akutendee yeye, ukimtendea yeye analalamika 🤷‍♀️🤷‍♀️🤷‍♀️‍♀️
 
ubinadam kazi mkuu
Akikufanyia ubaya na kukuumiza hakimsumbui, ila ukimlipizia kisasi na kumfanyia kama alivyokufanyia yeye atalalamika. Sasa sijui kuna binadamu wenye mioyo ya nyama na wengine yao ya chuma
 
Back
Top Bottom