Huyu Ndiye Kocha Mpya wa AZAM (WANA 4G) Iddi Cheche Nae Ala Shavu!

PROSPER 05

JF-Expert Member
Oct 14, 2013
226
217
KLABU Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati, Azam FC, mchana huu imemtangaza, Aristica Cioaba, kuwa Kocha Mkuu wa kikosi hicho.

Cioaba, 45, anakuja Azam FC kurithi mikoba ya Mhispania Zeben Hernandez, aliyesitishiwa mkataba pamoja na benchi lake zima la ufundi.

Kocha huyo atasaidiana na makocha wazawa, Idd Nassor Cheche na Kocha wa Makipa Idd Abubakar, walioiongoza timu hiyo kutinga hatua ya nusu fainali ya michuano ya Kombe la Mapinduzi, ambapo saa 10.15 jioni ya leo itasaka fainali kwa kukipiga na Taifa ya Jang’ombe.

Akizungumza na mtandao rasmi wa klabu www.azamfc.co.tz Ofisa Mtendaji Mkuu wa timu hiyo, Saad Kawemba, tayari wamefanikiwa kumpata kocha huyo na wameingia naye mkataba wa muda wa miezi sita wenye kipengele cha kuongezwa.

Alisema Cioaba ana uzoefu mkubwa wa soka la Afrika na ataiongoza Azam FC kwa kipindi hiki hadi mwishoni mwa mwa msimu, ambapo baada ya kuisha watakaa tena mezani kufanya tathimini ya mafanikio yake na wapi wanaweza kuendelea kutokana na kazi iliyofanyika.

“Bodi ya Wakurugenzi ya Azam FC inapenda wadau wote wa mpira na wapenzi na mashabiki wa Azam kwamba klabu imempata mwalimu, ambaye ndiye ataiongoza klabu kwa kipindi hiki hadi mwishoni mwa msimu.

“Kwa hiyo kwa mashabiki wetu maana yake ni kwamba tukiingia kwenye mechi inayofuata ya ligi, kocha atakuwa ameanza kazi na Cheche (Idd Nassor) atakuwa msaidizi wake na benchi lake zima alilokuwa nalo hivi sasa litaendelea,” alisema.

Kawemba aliongeza kuwa hivi sasa kocha huyo atakuwa na kikosi visiwani Zanzibar kufuatilia mwenendo wa timu ulivyo na ataendelea kutoa ushauri panapohitajika na ataanza rasmi kukaa kwenye benchi mpaka pale vibali vyake vya kufanya kazi nchini vitakapokamilika.

“Taratibu hizo zitakwenda kwa mujibu wa sheria za nchi, ambapo tutaziheshimu na kuona ya kwamba tutazifanya kwa haraka zaidi ili mwalimu aweze kupata kibali cha kufanya kazi hapa nchini, kwa hayo machache tunawaomba mashabiki wetu wawe watulivu wampe sapoti kocha na wadau wote wa mpira waone ya kwamba tumefanya jambo la kheri,” alisema.
kocha Azam.jpg
kocha Azam 2.jpg
 
Mtu keshapiga dili tena.

Kocha mpya naye atataka wachezaji wake wa kigeni. Dili nyingine hiyo.

Mpaka Azam washtuke, jamaa atakuwa yupo vizuri sana. Dili baada ya dili. Mungu akupoe nini?
 
Saad kawemba moja ya CEOs wapuuzi kabisa katika soka .. Huyu ni jipu pale azam
Tumewaza pamoja,nilitegemea huku Azam mambo yataenda kisasa sana,sababu hakuna zile vulugu za wanachama kama kule Simba na Yanga lakini wapi,yule Mhisispaniola alilalamika kuingoliwa kiutendaji na huyu jamaa...
 
Tumewaza pamoja,nilitegemea huku Azam mambo yataenda kisasa sana,sababu hakuna zile vulugu za wanachama kama kule Simba na Yanga lakini wapi,yule Mhisispaniola alilalamika kuingoliwa kiutendaji na huyu jamaa...
Point. Wenye Timu inabidi waangalie Tena Safu ya Uongozi na Mfumo wa Uongozi, Pia waangalie Wachezaji Hasa wale wa Wazamani Kama bado wanafaa kuitumikia AZam fc
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom