Huyu ndio "Rodrigo Duterte" Rais wa Ufilipino

CONTROLA

JF-Expert Member
Sep 15, 2019
6,939
22,985
Rais wa Ufilipino, Rodrigo Duterte amewaruhusu wananchi kumpiga risasi kiongozi yeyote wa serikali atakayewaomba rushwa.

Akihutubia mamia ya wananchi wiki iliyopita katika Jimbo la Bataan, Kaskazini mwa Jiji la Manila, Duterte amesema kuwa rushwa ndio kikwazo kikubwa cha maendeleo ya taifa hilo.

Durtete amesema kuwa mwananchi yeyote anayemiliki silaha, Anamruhusu kumtwanga risasi kiongozi yeyote atakayeomba rushwa lakini sio kumuua bali kumjeruhi.

Kiongozi huyo anayetajwa kuwa ni Dikteta, Amesema kuwa mwananchi akimjeruhi kiongozi aliyeomba rushwa yeye atasimamia kesi yake mahakamani.

Kiongozi wa serikali yangu kama atakuomba rushwa, Mpige risasi ila usimuue wewe mjeruhi tu. Mimi najua hili taifa linakwamishwa na rushwa, Hivyo mkiwajeruhi hawawezi kurudia na mimi nitawafukuza serikalini. Narudia mwananchi unayemiliki bunduki, usimchekee kiongozi anayekuomba rushwa, Mimi nitakusimamia mahakamani na huwezi kufungwa.” amesema Duterte.

Rais Duterte ni moja ya viongozi duniani wanaotajwa kuvunja haki za binadamu kwa asilimia kubwa zaidi duniani. Hii ni baada ya mwaka juzi kufanya msako wa kuvunja magenge ya wahalifu na wauza madawa ya kulevya na kisha kuwaua.

Mwaka jana pia Rais Durtete aligonga vichwa vya habari duniani, Baada ya kumtukana Mwenyezi Mungu ‘Mpumbavu’ kwa kitendo cha kumuumba Eva na kumuweka na Adam katika bustani ya Edeni huku akiwakataza wasile tunda la katikati huku akijua kitu hicho hakiwezekani.
ssas.jpg
 
Magufuli na sisi aturuhusu maana hizi vitu tunazilipia kila mwaka na hatuna matumizi nayo,tangu tuzichukue ndio hata kukabwa hatukabwi tena

Kukerwa na watu ovyo hawakeri yani hamna anae hangaika na wewe,Juzi hapa nimejitembeza kwa mguu makusudi ili wanikabe ila WAPI.

Ruhusa za namna hiii tupewe wamiliki yani Na uhakika muhimbili ntaijaza matrafic ndani ya wiki 1 tu
 
Nenda maeneo ya Tandika uone kama ukabwi,
 
Back
Top Bottom