Huyu Melikizedek ni nani?

Introver

JF-Expert Member
Joined
Apr 6, 2019
Posts
565
Reaction score
655
Melkizedeki ni nani?


Neno la Mungu linatuambia katika 1Timotheo 3:16 kuwa “bila shaka siri ya utauwa ni kuu.” Au kwa lugha rahisi Neno hili tunaweza kusema “bila shaka siri ya Uungu ni kuu; Hii ikiwa na maana kuwa kuufahamu uungu wa Mungu, si kitu chepesi tu cha kufikirika kibinadamu, bali kipo katika Siri na Siri hiyo ni kubwa sana..Hivyo hiyo inatuhimiza sisi tumwombe Mungu atufunulie ili tuzidi kumjua yeye siku baada ya siku.


Kumbuka Hapa katika hii siri ndipo palipoleta mgawanyiko na mkanganyiko mkubwa kati ya Ukristo na Imani nyingine kama vile uislamu, Na hapa hapa ndipo palipoleta migawanyiko mingine mikubwa katikati ya wakristo wenyewe.


Lakini sisi hatutaingia huko leo, bali kwa ufupi tutamtazama huyu Melkizedeki ni nani, kwa kurejea baadhi ya vifungu vya maandiko. Sasa kumbuka biblia inaweka wazi kabisa, kwamba Kristo alikuwepo kabla hata kabla ya kitu chochote kuwepo duniani.


Yohana 8:57 “Basi Wayahudi wakamwambia, Wewe hujapata bado miaka hamsini, nawe umemwona Ibrahimu?


58 Yesu akawaambia, Amin, amin, nawaambia, Yeye Ibrahimu asijakuwako, mimi niko”.


Unaona Lakini swali tunajiuliza alikuwepoje? Hili ni swali ambalo hata wakristo wengi leo hii tunashindwa kulijibu ipasavyo. Tutasema Yohana 1:1 Inathibitisha hilo kuwa hapo mwanzo kulikuwepo na Neno naye Neno alikuwako kwa Mungu naye Neno alikuwa, ambaye ndio YESU. Hivyo Yesu alikuwepo tangu mwanzo mbinguni na baba yake mpaka ilipofika wakati wa yeye akashuka duniani kuja kutuokoa.


Lakini hatujui kuwa huyu YESU ambaye anaonekana kwa maumbile yale, hakuwepo tangu mwanzo. Safari yake ilianzia AD 1, tutaliona hilo tunavyozidi kusonga mbele.


Kama biblia inavyosema hapo mwanzo kulikuwako “Neno”, Hivyo kwa asili yake NENO sio mtu, Hili ni Neno la kigiriki Logos, likiwa na maana ya WAZO LA MUNGU, /KANUNI au NIA ya Mungu.


Sasa hili Neno kazi yake kubwa ilikuwa ni nini?


Tukisoma:


1Yohana 1:1 “Lile lililokuwako tangu mwanzo, tulilolisikia, tuliloliona kwa macho yetu, tulilolitazama, na mikono yetu ikalipapasa, kwa habari ya NENO LA UZIMA;


2 (na uzima huo ulidhihirika, nasi tumeona, tena twashuhudia, na kuwahubiri ninyi ule uzima wa milele, uliokuwa kwa Baba, ukadhihirika kwetu);


3 hilo tuliloliona na kulisikia, twawahubiri na ninyi; ili nanyi pia mpate kushirikiana nasi: na ushirika wetu ni pamoja na Baba, na pamoja na Mwana wake Yesu Kristo”.


Unaona hapo Hili Neno kumbe limebeba UZIMA ndani yake (Yohana 1:4), ambao uzima huo Mungu alitaka kuudhihirisha kwetu tangu zamani. Hapa mitume wanasema walikuwa wanalisikia tangu zamani, hivyo halikuwa jambo jipya katika masikio yao lakini baadaye sasa wakati ulipofika wakaja kupata neema ya kuliona kwa macho yao wenyewe na kulipapasa siku lilipokuja kufanyika mwili ndani ya YESU KRISTO.


Sasa tumeshaona uzima wowote ni Neno la Mungu (Wazo la Mungu) kwa mwanadamu, Kazi yake kubwa ni kurejesha kilichopotea na kukikomboa. Hivyo katika maandiko Neno hili la uzima halikuanzia kwenye Ule mwili wa YESU KRISTO pekee, hapana bali lilianzia tangu mbali sana, isipokuwa lilifichwa tu machoni pa watu wasilitambue kwasababu SIRI ya utauwa ilikuwa bado haijafichuliwa. Hivyo hili NENO Lilichukua maumbile mengi mengi tofauti kwa lengo tu la kutimiza kusudi lile lile kuleta uzima ndani ya watu.


➔Tunaona lilikuwepo kuanzia Edeni, mwanzoni kabisa mwa safari ya mwanadamu kama Ule mti wa Uzima katika bustani, Lile lilikuwa ni NENO LA MUNGU..lilikuwepo pale kuwapa uzima Adamu na hawa, kuwazuia na mauti, lakini walipoasi wakafukuzwa mbali nalo.


➜Baadaye likaja likachukua umbile lingine tena la MERIKEBU(SAFINA), Lilisimama pale ili kuwakomboa wanadamu na uzao wao usipotee kabisa katika uso wa dunia, akaokoka Nuhu na watu wengine 7.


➜Baadaye likaja kuchukua umbo la mnyama MWANAKONDOO, siku ile Ibrahimu alipokwenda kumtoa mwanawe wa pekee kuwa sadaka ya kuteketezwa likasimama kama dhabihu badala ya Isaka kama Yule kondoo aliyekuwa mlimani kichakani, vyote hivyo vilifanyika kwa mafumbo makubwa sana, kufunua UZIMA hasa udumuo utakaokuja huko mbeleni..


➜Ndio baadaye tunakuja kuona linachukua tena maumbile ya wanadamu likaonekana duniani kwa wakati mchache kutimiza kusudi Fulani ndio sasa hapo tunamwona mtu anayeitwa MELKIZEDEKI. Kama kuhani kumpatanisha Ibrahimu na Mungu kwa kitambo tu. Lakini ukuhani halisi ulikuwa bado haujafunuliwa.


Waebrania 7:1”Kwa maana Melkizedeki huyo, mfalme wa Salemu, kuhani wa Mungu aliye juu, aliyekutana na Ibrahimu alipokuwa akirudi katika kuwapiga hao wafalme, akambariki;


2 ambaye Ibrahimu alimgawia sehemu ya kumi ya vitu vyote; (tafsiri ya jina lake kwanza ni mfalme wa haki, tena, mfalme wa Salemu, maana yake, mfalme wa amani;


3 hana baba, hana mama, hana wazazi, hana mwanzo wa siku zake, wala mwisho wa uhai wake, bali amefananishwana Mwana wa Mungu); huyo adumu kuhani milele……………….


Waebrania 7:15 “Tena hayo tusemayo ni dhahiri sana zaidi, ikiwa ametokea kuhani mwingine mithili ya Melkizedeki;[anazungumziwa YESU KRISTO]


16 asiyekuwa kuhani kwa sheria ya amri iliyo ya jinsi ya mwili, bali kwa nguvu za uzima usio na ukomo;


17 maana ameshuhudiwa kwamba, Wewe u kuhani milele Kwa mfano wa Melkizedeki”.


Mahali pengine tena Neno lilipochukua umbile la kibinadamu, ni pale Shedraka, Meshaki na Abednego walivyotupwa kwenye tanuru la moto Likatokea kwa mfano wa mwana wa Mungu, likawa linazungumza nao kisha likaondoka..Kwasababu lilikuwa bado halijashuka rasmi duniani. Lakini utaona lengo lake ni lile lile kuleta uzima na kuokoa.


Sehemu nyingine lilitokea kama MWAMBA. Kule jangwani wana wa Israeli walipokuwa wanakaribia kufa na kiu lilisimama mbele yao ili kuwaokoa, Na Musa hakulifahamu hilo mpaka alipofanya uzembe ule wa kuupiga ule mwamba mara mbili ndipo alipojua kuwa kumbe alikuwa amesimama mbele ya uzima wenyewe, mbele ya mkombozi mwenyewe.


(1Wakorintho 10:4 “wote wakanywa kinywaji kile kile cha roho; kwa maana waliunywea mwamba wa roho uliowafuata; na mwamba ule ulikuwa ni Kristo”.)


➜Baadaye likaja kujidhihirisha katika maumbile mengi tofauti tofauti mfano kama Hekalu, Sehemu nyingine kama malaika, sehemu nyingine kama nguzo ya moto. Sehemu nyingine kama NYOKA WA SHABA.


(Yohana 3:14 “Na kama vile Musa alivyomwinua yule nyoka jangwani, vivyohivyo Mwana wa Adamu hana budi kuinuliwa;

15 ili kila mtu aaminiye awe na uzima wa milele katika yeye”.)


➜Sehemu nyingine likajidhihirisha kama HEKIMA Ambayo aliwavaa waamuzi na wafalme wa Israeli akianziwa na Sulemani na wengineo waliomfuata, ili tu kutimiza lengo la kuwaokoa na kuwatunza watu wake kupita wafalme wale Mungu aliowachagua hekima yake ikae ndani yao.


Ukisoma Mithali sura ya 8 na ya 9 utaona kabisa jinsi Sulemani anavyoilezea hekima kama kitu chenye uhai na kinazungumza, Pia soma (1Wakorintho 1:24) utaona inamtaja KRISTO kama yeye ndio hiyo Hekima ya Mungu yenyewe.


Sehemu hizo hatuna muda wa kuzielezea moja moja, Lakini nataka uone picha Fulani hapo, NENO LA MUNGU jinsi lilivyopana, Na jinsi lilivyokuwepo tangu mwanzo. Hivyo baadaye sasa wakati ulipofika, Mungu kuufunua utimilifu wote, Mungu kuweka wazi WAZO lake lote kwa mwanadamu, Mungu kuufunua uzima wote na Ukombozi wote, akaona ni vyema sasa aunde mwili maalumu, mahususi, uzaliwe na mwanamke bikira, uitwe jina la YESU (Maana yake YEHOVA-MWOKOZI) ili sasa liweze kukaa na wanadamu milele, lizungumze nao, liwajibu maswali yao, liwafundishe, walipapase, walitegemee hilo, liwaongoze katika njia ya kweli na ya haki na ya uzima hata milele. Hapo ndipo tunaona Lile Neno ndani ya mwili unaoitwa Yesu…ambaye kwa ujumla sasa ndio tunamwita BWANA YESU KRISTO HALELUYA! HALELUYA!.


Yohana 1:14 “Naye Neno alifanyika mwili, akakaa kwetu; nasi tukauona utukufu wake, utukufu kama wa Mwana pekee atokaye kwa Baba; amejaa neema na kweli”.


Ndio maana mtume Yohana alikuwa anaoujasiri kabisa kusema maneno haya…


1Yohana 1:1 “Lile lililokuwako tangu mwanzo, tulilolisikia, tuliloliona kwa macho yetu, tulilolitazama, na mikono yetu ikalipapasa, kwa habari ya Neno la uzima;

2 (na uzima huo ulidhihirika, nasi tumeona, tena twashuhudia, na kuwahubiri ninyi ule uzima wa milele, uliokuwa kwa Baba, ukadhihirika kwetu);”


Sasa tukirudi kwenye zile kauli za Yesu anaposema kabla Ibrahimu hajawapo mimi nipo, hapo tunaona alikuwa hauongelei ule mwili uliozaliwa na bikira, bali alikuwa anaongelea lile Neno la Mungu ndani yake. Ukilijua hilo hutasema kuwa Mungu anazo nafsi tatu. Wewe na MAWAZO yako au NIA yako hamwezi kuwa vitu viwili tofauti vinavyojitegemea, ni kitu kimoja.Lile Neno ndio Mungu mwenyewe, Yesu Kristo ni Mungu ndani ya Mwili.


Hivyo ndugu tukirudi kwenye kichwa cha Somo je! Huyu Melkizedeki ni nani?. Jibu ni kuwa Huyu Melkizedeki ni Neno la Mungu lililojidhihirisha katika mwili kutimiza kusudi fulani kabla ya wakati wake mtimilifu. Lakini baadaye ndilo liliokuja rasmi kuitwa YESU KRISTO.Hata sasa tunaposema mkaribishe YESU Kristo ndani ya maisha yako, tunamaanisha likaribishe Neno la UZIMA la Mungu ndani ya maisha yako, Kwasababu Neno hilo sasa limefunuliwa ndani ya Kristo Yesu Bwana katika utimilifu wote. Kwahiyo unavyolisikia hili Neno na kulipokea, ni sawa umempokea Yesu Kristo mwenyewe ndani ya maisha yako…


Je! Leo hii bado Upo katika dhambi?, Na hali Tumesharahisishiwa wokovu namna hii bado unauona ni mgumu kuupokea?. Watu wa Agano la Kale japo walilifahamu hili Neno la Mungu kwa sehemu tu kwa kupapasapasa lakini walitii kwa utimilifu wote wakapata wokovu sisi je! Tutapataje kupona tusipouthamini wokovu mkuu namna hii?(Waebrania 2:3). YESU KRISTO ndio wazo la Mungu, ndio NIA ya Mungu, ndio MUNGU MWENYEWE katika Mwili. Tumfuate yeye tupate kuwa salama, katika safari yetu hii fupi hapa duniani.


Ubarikiwe sana.
 
Swali fupi maelezo mareeeefu, ntakuja kuyasoma nikipata muda
 

"ILIMU AL LADUNNI"...

Jamii mbalimbali hapa Duniani zimekuwa na visa vya mapokeo kwa yale yaliyo ni mafumbo ya Uzima--Kwa sura moja ama ingine: Yale ambayo kwenye siku hizi zetu za leo, tungalikadirisha kama mambo ya 'Wasafiri Kiwakati'...

Melkizedek, Khidr, Yesu, Eliya, Shiva, Khrishna, Babaji, n.k

Ingalikuwa ngumu kiasi gani kuwaambia watu wa zamani kuhusu mawezekanano ya Kusafiri Kiwakati--na hali kusafiri kiwakati daima kumewepo--Hapa Duniani na hata kwenye Sayari zingine?

Ingalikuwa ni vigumu kiasi gani kuwaambia watu wa sasa, 2025, kuhusu mawezekano ya Kusafiri Kiwakati ( ! )


Kile ambacho Mzee Trump na serikali yake wamekidhamiria kuhusu MRADI STARGATE si chochote bali 'ingilio' la mawezekano haya ya 'Kiunishati Habari'--Neno la Uzima: (1) Akilibandia katika Steroidi, (2) Ungamuzi wa Kikwantumu na (3) Umeme Mkubwa; ni tekinolojia za milango/teminali za 'Kutobozea/kupindisha Supasha-Wakati'...

Kusafiri Kiwakati kunawezekana kitekinolojia za unnje, na pia tekinolojia za uundani wa 'Utu wa Kimiili'...

Wakati mmoja, kadiri wanajamii wanafaulu kujisahihisha na mitego ya 'Vita vya Kumbukumbu'; TORATI 2.0 inaangazwa kwenye 'Vituo vya Utamaduni' -- kote Duniani; waja wema watayajua na kuyaweza haya yote ya 'Kusafiri Kiwakati'...

Hmmm


Hmmm


View: https://www.youtube.com/watch?v=_D8aNRwK8vM
 
KWAHIYO MELKIZEDEKI NINNANI?
naona Kama ni Yesu labda alikuja kwa mission nyingine na hakutaka wamjue au?
 
KWAHIYO MELKIZEDEKI NINNANI?
naona Kama ni Yesu labda alikuja kwa mission nyingine na hakutaka wamjue au?​
FUMBO LA MIILI NA KUMBUKUMBU...

Kiakili na Utambuzi, sisi watu wa Dunia tunalotatizo la kiufundi kuhusiana na fahamu na mafahamu...

Tuna utambuzi mushkeli kuhusu kila kitu ikiwemo 'Sisi ni Nani' na 'Tunaishi katika Dude Gani(?)'...

Kuanzia sasa, tuseme, 2025, ili kulishughulikia tatizo hili--lugha mpya itaanza kuzungumzwa miongoni mwetu; hiii inakuwa ni lugha kwa ajili ya maandalizi ya kujijengea 'Maarifa na Maarifu' ya 'Ukweli uliostirika wa Mambo'...

Hili, kiuono na ufikirifu mifumo, ni sawa na muktadha akilifu wa kukadirisha vina vya tafsiri ya kwamba kuishi Duniani ni Kupoteza Kumbukumbu...

Sifa na Hadhi ya kuishi na kupoteza kumbukumbu ndiyo 'tamu chungu' ya kuyaishi maisha ya Dunia--walionje ya Sayari yetu wakati mmoja hata mwingine hutamani 'Kuingia Kuicheza Ngoma' ya maisha na Dunia na basi miongoni mwetu, na tena wengi wetu, ni watu tunaoucheza huu mchezo kwa muda--kuzaliwa, kuishi na kufa/kuondoka Duniani...

Kwa mintarafu ya hivi, maisha ya Dunia ni mithili ya Kuishi kwenye 'Ulimwengu wa Kufikirika' --ulimwengu ambao wanaoshiriki ndani yake huridhia kuingia kuucheza wakiwa 'Wamejisahau ama/na kusahau' ukweli wa jambo/mambo yenyewe.

Basi ndiyo yawa; kuishi Duniani kuna kukutana na mengi ambayo mwenyekuishi ataishi nayo kwa raha ama karaha; na huku akijaribu sana 'kuitafuta maana ya kuishi'--anaweza kudhani (1) ulimwengu wote mzima una maana kwa maisha yake ama (2) maisha yake ndiyo yenye maana kwa ulimwengu wote mzima; kutegemeana na Roho ya Utambuzi na nasibu ya 'Kujitambua'...

SASA, ulimwengu wa Dunia, kiukweli wa mambo ni 'Matriksi'...

Matriksi ni 'Mwili wa Kumbukumbu na Mafumbo ya Uzima'--wote tunaoishi katika huu ulimwengu tunashiriki jukwaa moja la 'Muona ni Muonwa'...

Katika hali ya kushangaza, tunachosadiki na kuamini--sehemu ya hayo tunauthibitisha ukweli wa kutengenezeka katika 'Matriksi'... Kwa mfano, ikiwa tunaishi na kuanza kujiuliza mimi ni nani--je, ninafanya nini hapa Duniani? Hili linaanza kuwa ingilio la kuanza 'kuichokonoa Matriksi'...

Katika Matriksi, kuna mengi ya 'kianzio' cha ufahamu na mafahamu kwa ajili ya Usentienti, Konsayansi na Nuru ya Ufahamu; haya Kiuono na Ufikirifu Mifumo yanakuja na Shauri na Mashauri kuhusu 'Akili Jinetifu'... Namna fulani ya Roho ya Utambuzi inayofungana na fahamu zetu za nje--fahamu za kimiili--miili ya nyama.

Kwenye Matriksi kuna 'Sheria na Kanuni' za kutawala dhahiri ya mambo na 'Ontolojia ya Taasisi'; hii ina maana ya kwamba vile vyote tunavyoishi kuvifahamu kwa uwezo na vipawa vya akili jinetifu ndiyo msingi wa 'Elimu'; jambo ambalo kiuno na Ufikirifu Mifumo, tulitambue hili kwa muktadha akilifu kama 'Elimu 1.0'...

SASA, Matriksi ni 'UHANDISI WA MAWANDA YA KIUFAHAMU' ambavyo 'CHANZO CHA UZIMA' kinakadirika 'PUMZI YA UZIMA'--Uzima wa mambo wenye kuakisi WAKATI kama umbali kati ya 'MUONA NA MUONWA' katika Ugani wa nasibu ya 'UZIMA WA MILELE'.

Kiufundi, dhana ya kupoteza kumbukumbu ndicho kile kile kwenye mapokeo ya Ukristo huja kwa khabari za 'Kutenda Dhambi/Dhambi ya Asili/Kupungukiwa na Utukufu wa Mungu'...

Kiufundi, dhana ya kurejesha kumbukumbu ndicho kile kile kwenye mapokeo ya Ukristo huja kwa khabari za 'Kukomboka/Kuukomboa Wakati/Kufufuka/Kupaa Mbinguni'...

Kiufundi, kisa cha Yesu 'Kufufuka/Kuwatokea Wafuasi huku na Kule/Kupaa Mbinguni' ni asili ya 'Kutoboa hii Matriksi ya Dunia...

Basi ndivyo yawa, kisa cha kusema Yesu 'amekufa na kufufuka', ameishinda 'Mauti', ni fumbo la imani kwa Ukweli wa Kushinda adha kuu ya Matriksi ambayo ni kuogopa mauti na hali haujui 'Umetokea wapi ama Utakwenda wapi baada ya Mauti ya Mwili'...

Kisa cha kusema Yesu aliwatokea wanafunzi wake baada ya 'Ufufuko', akiwa na mwili wa utukufu, ni namna ile ile ya kuzungumza kuhusu 'Wasafiri Kiwakati'--mtu kuweza kuonekana hapa wakati huu, na hapo hapo labda, kutokea kungine 'bila shida'--mambo ya 'Ufalme, Nguvu na Utukufu'...

Haya mambo ndiyo kwenye mapokeo ya Uislamu huja kwa khabari za 'Arshi' ama pia 'Dhikr'--Nidhamu ya Kukumbukia.

Kumbe basi, dawa ya 'kutoboa Matriksi' ni 'Kukumbukia' kwenye 'CHANZO' cha Uzima wa Milele... Hichi ndicho kile kile kwenye mapokeo ya Ukristo huitwa 'Mwangaza wa Milele' ama 'Nuru ya Watu', Nuru iliyoko ndani ya Kiumbe Chochote chenye Usentienti-Konsayansi-Nuru ya Ufahamu...

SASA, dini zote ni 'Mchezo wa Kufumba na Kuchezea Akili za Wanaojitafuta', kwenye lugha ya kileo ya Maarifa na Ujuzi ni sawa sawa na kusema 'Matriksi' ni mkusanyiko wa mpangilio wa maneno, seti za maelekezo-utekelezaji-kuitika vitendo, yanayoishi kwa pumzi za wakati na huku yakipata 'Nguvu' kutokana na 'Matriksi' nyingine yenye Uzima zaidi. Hili kwenye Mapokeo ya Ukristo, ile 'Matriksi ya Uzima zaidi' ndicho kile khasa hutajwa ni 'Roho Mtakatifu'...

Dini zote zinavishikizo ambavyo vinaweza kubayanika kwa mtu wa Hekima na Roho ya Utambuzi kwa ngazi/daraja la Ufunuo wa 'Roho Mtakatifu'...

Kiufundi, mambo yote ya Melkizedek, Khidr, Yesu, Eliya, Shiva, Khrishna, Babaji, n.k ni ILIMU ilivyo ni metafizikia ya Elimu... Sayansi 3.0 ya 'UWEPO' -- Kwenye habari za dini za Uyuda/Ukristo ni mambo ya SHEKINAHI--Uwepo katika 'Nguvu na Utukufu'...

Katika Uwepo, Maarifa na Maarifu ya UTU ni nyenzo ya moja kwa moja ya kutenda kwa hata namna zenye kupitiliza kawaida tuliyoizoea--kawaida ya 'Matriksi Dunia/Sayari/Falaki'; kwa shauri hili, tuanze kudhamiria ku-JUA -- kujua ilivyo bora ya kwamba 'Dhahiri yote ni Maneno/Mawazo yanayoishi'... Kufanyika Utu wa Nguvu ni mwanzo wa kuyamudu 'Maneno haya yanayoishi' kwa kurejea kwenye kitovu cha CHANZO--Chanzo ndiyo kile ambacho kwenye Dini moja ama ingine hu/kuzungumzwa ni 'Mungu'...

Basi ndiyo yawa; katika Kitovu cha Chanzo kuna nasibu ya kuyamudu yote ya miili, wakati na upahala--kiufundi na ukweli khasa wa mambo 'HAKUNA WAKATI'... Wakati ni vina vya tafsiri tu kulingana na Uakili jinetifu tulionao ili kuishi kwenye ulimwengu wa mapana-kimo-kina-kimo...

Kuna ambayo tutaanza kuelekezana na kufundishana kuhusiana na 'fumbo la wakati/nyakati'--kwenye mapokeo ya Dini, wakati ni kitu kinachohusishwa na 'Shetani/Ibilisi': kuwa kwamba asili ya Matriksi ni Shetani kama fanusi inayokinza UTU usirejee katika 'Mwangaza/Kumbukumbu ya Miongozo ya Uhai/Kristu'...

Kwa hivyo maisha ni 'majaribu' pia kwa kumbukumbu za uongo na kweli kuhusu 'Utu Wetu'; ambavyo kuishi Duniani kuna mengi ya hadaa--hadaa iliyotengenezeka ili kuwanasa walimwengu waicheze 'Sikinde Ngoma ya Ukae'... Wapo viumbe watu wanaodukua 'Matriksi' na kuzijaza mabatili ili wale wote wenye Usentienti-Konsayansi-Nuru ya Ufahamu 'Wasitoboe'--wasishtukie Mchezo na 'Kuharibu Mambo'...

SASA, Matriksi huharibiwa kwa kuleta 'Mwangaza' kwenye mapana ya Ustawi wa wale wenye kuishi ndani yake... Hili ndilo hufanyika kwa 'UTU wa Nguvu' kuingia ndani ya Matriksi yenyewe na Kuuishi Utambuzi na Akili yenye Nguvu... Ndicho kisa na Mkasa cha akina Melkizedek, Khidr, Yesu, Eliya, Shiva, Khrishna, Babaji, n.k

Kuna mengi, sasa tunayaingia ili kuja kuyafahamu moja kwa moja....

Hmmm
++++


View: https://www.youtube.com/watch?v=SDkAGkd4NLc
 
Melikizedek kulingana na Biblia
Alikuwa Kuhani Na Mfalme Jerusalem wakati wa Ibrahim (Sifa za Kimasihi.

Alikuwa anaamini Mungu sawa na Ibrahim (Inaonesha Yawehism was always there)

Ni mtu pekee ambaye amewahi kuwa Kuhani na Mfalme, atakaye kuwa hivi ni Masihi ajeye kulingana na Imani za Kiyahudi

Kulingana na Waandishi wa agano LA kale wanamlinganisha Melkezedeki na Yesu
 

Tanzania – Ilivyo ni Taifa-Dola/Nchi-Dola, katika muktadha akilifu wa mapana ya Jamii ilivyo ni Uono na Ufikirifu Mifumo, tena kwa fremukazi ilivyo ni TRIZANIAMU, ni ‘Moyo’ wa mageuzi makuu ya kijamii na utamaduni kwa Bara la Afrika na hata Dunia Nzima; ambavyo hili linafanyika kwa Ufadhili wa utendaji wa Kimazingira na Mazingara ya Wadau wenye ‘Uweza-Utayari-Umahiri’ walio katika miili na wasio katika miili ya nyama.

Kwa mintarafu ya hivi, ‘Uweza-Utayari-Umahiri’ wa wanajamii wa Taifa la Tanzania unasimama katika mhimili wa ‘Mkuki wa Jaala’ ambavyo (x) Uakili-Jinetifu, unasaba wa uzazi na mazazi ya jamii na tena katika Upumzi wa Mazazi, hudhamirika kwa kuanza na (y) Mbegu za Utu bora kwa ‘Uhuru-Udugu-Haki-Amani’; Mbegu inayochanua na kustawi katika akili na mioyo ya wanajamii na hata kuja kukadirisha ‘Ndoto ya Ujamaa’ wa kweli : (z) ‘Sovereini Jumuifu’ ya Ujamii katika ‘Ufalme-Nguvu-Utukufu’.

Basi ndiyo yawa, (1) asili khasa ya ‘Ufalme’ ni nasibu ya Utashi Uliobora na Mamlaka ya Kujiamulia na Kutenda mambo kwa Maarifa na Maarifu yaliyobora, (2) asili khasa ya Nguvu ni Simetria na Koherensia ya Miundo na Vitendo, na (3) Utukufu ni mnunurisho wa Kimafikara yenye kubeba mbegu za Hekima-Nguvu-Uzuri.

Kiufundi, TRIZANIAMU ni mizania ya Utatu, Upembetatu, wa (1) UONO, (2) ONTOLOJIA YA TAASISI, na (3) SOVEREINI JUMUIFU; ambavyo (x) ‘Miundo na Matendo’ hufanya Swastika ya ‘kupanda na Kuvuna’ kiudhamirifu wa Utu, Maisha na Kujichagulia. (y) Uono Mifumo ni Umbonishaji Sahihi wa Dhamira na Matendo ya chochote chenye asili ya Usentienti, Konsayansi na Nuru ya Ufahamu; kwa kuwa (z) Sura na Mienendo ya Jamii ni ‘Sovereini Jumuifu’ pale ambapo kuna ‘Usahihi wa Kimfumo’ katika Miundo na Matendo ya Wanajamii.

Kwa mintarafu ya hivi, Maisha na Kujichagulia ni fanusi ya (1) Kujua / Ku-Jua ama pia (2) Kutojua Kabisa/Ujinga; katika Usentienti (Kujisikia) kwa Wanajamii; ambavyo kutopatia Shauri-mbegu kwa ‘Dhamma ya Sovereini Jumuifu’ ilivyo ni ‘Uhuru-Udugu-Haki-Amani’ huleta Sura na Mwenendo wa Jamii wenye ‘Historia yenye Kujirudia’ : Karma. Hili lafanya msingi wa Elimu 1.0, kwa sehemu kubwa, imejikita kwenye visomo empirikali vyenye asili ya Ukweli unaotegemea Matokeo ya Kimarudio ya Kimazingira, kiakili na Utambuzi; kama ‘Sayansi’ ya kubayanisha ‘Uhakika’ wa ‘Mipangilio ya vitendo na Matokeo yake kwa Uono Rahisi wa Kawaida na tena ‘wa Juu Juu’ wa mambo.

Basi ndiyo yawa, Ujuu Ujuu wa mambo ni Mashauri yenye Konstrakti za kadiri ya Duara, Mraba na Pembetatu ambavyo marefu, mapana na kina chake hukadirisha pumzi ya Utufe, Mraba na Piramidi; ambavyo (1) Utufe Hushikilia yote ya Nguvu na Utukufu, (2) Mraba Hujishikiza kwenye Nguvu na Utukufu na basi kufanya nasibu ya Pumzi na Kugawanyika kwa ‘Hekima-Nguvu-Uzuri’ na (3) Piramidi hutia ‘Chachu na Moto’ wa Uhai wa ‘Hekima-Nguvu-Uzuri’ kwa asili isiyokoma ya ‘Uzima wa Mambo’.

Uhusiano wa Uduara, Mraba na Pembetatu ndiyo fanusi ya Eneagramu ya UTU ilivyo ni UUNGU – Tisa (9) iliyo ni Tatu(3) mara Tatu(3) katika Uduara; ambavyo Hekima-Nguvu-Uzuri hutunisha KUBU ya Matriksi mara 24 – pande miraba sita (6) zenye ‘Vitendo Miundo’ vipatavyo vinne(4) katika kila kingo. KUBU huwa na nasibu ya kugawanyika kwa fanusi ya ‘Msalaba’ ambavyo Kuna idadi ya Misalaba mitatu (3) tu inayogawa KUBU yote katika vipande sawa Vinane (8). ‘Unane’ uliyo ndiyo asili ya Oktavi ya Mipangilio ya Kipumzi, Utetema – ‘toni sauti’ na ‘rangi za kimwangaza : Mwanga Mweupe kuwa Uhamonifu wa Rangi Saba za Upinde’.

Kiufundi, Mageuzi ni fanusi ya KUBU na Oktavi za Mipangilio ya Kipumzi ilivyo ni Utetema; ambavyo utetema ndiyo hata asili ya Ulimwengu wote kuwa ni wenye ‘Kuzima na Kuwaka’ kwa kasi ya hali ya juu mno – na huku Usentienti kuwa ni ‘mazazi ya Pumzi’ ya ‘kumbukumbu Uzoefu’ ilivyo ni ‘Mafikara Yanayoishi’. Hili lafanya ‘Mbawa Mbili’ za ‘Shika Neno, Tenda Neno’ kuwa ni asili pacha ya ‘DNA’ : Gundi Nne(4) za kiprotini katika Ujinetifu/Unasaba ni kadiri empirikali ya ‘Ushawishi’ na ‘Miundo’ kwa kujisuka na kujifuma kimuundo wa ‘Seli Hai’ za namna ya ‘Miili yenye Uzima’.

Kwa mintarafu ya hivi, katika ‘Ontolojia ya Taasisi’ ni ‘Tunda la Maarifa na Maarifu ambalo ni Tunda Uzima’ ndilo huja kufanya ‘Mbegu ya Uzima’ilivyo ni mbegu ya ‘U-JUA-ji’ kwa ‘Maumbile Hai’ ilivyo ni pumzi iliyoganda na kushikilia ‘Matendo ya Uhai’ – Uhai wa Kimazingira na Mazingara wa Kiumbe chochote chenye Usentienti, Konsayansi na Nuru ya Ufahamu/Kujifahamu; ambavyo kukua na kuongezeka ni usikronifu (Pumzi za Marefu ya Muda, katika muenendano/mlandano wa Wakati/Majira) wa matendo ya pumzi kugawanya miundo hai katika mafungu ya 1→2→4→8→7→5→1—skeli dayatonishi katika Eneagramu.

Basi ndiyo yawa, ‘namba 13’ ni namba tukufu ya Mageuzi kwa kuwa KUBU ya uasili wa ‘Uhai wa Hekima-Nguvu-Utukufu’ kukadirika kwa (x) Akitipu ‘Umbawa Shika-Neno-Tenda-Neno’, na (y) Akitipu ‘Kumbukumbu Uzoefu’; Tunda la Maarifa na Maarifu kwa Oktavi za Mipangilio ya Kipumzi ina Maduara 13, na pia vivyo hivyo ‘Utukufu wa Hekima-Nguvu-Utukufu’ una Maduara 13.

Hili la ‘namba 13’ kuwa na ‘Utukufu’ ndilo, >katika mapokeo ya Ukristo -- kwa mujibu wa rejea ya Shauri katika khabari za Mathayo 13<, lafanya ‘Ufahamu Kristu’ kuwa ni ‘Metafo ya Ufalme wa Mbingu’ ijayo kwa akitipu (Nasibu konstrakti kwa fahamu na mafahamu Kiakili na Utambuzi kwa ajili ya Usentienti Jinetifu) ya yote matatu katika vielezi vya:- (1) Upanzi wa Mbegu, (2) Utunzaji wa Shamba, na (3) Malaika wa Mavuno/Uvunaji; ama pia Mshika Nyengo ya Mauti’ katika ‘vielezi Mafunuo’ kwenye khabari za ‘Kitabu cha Ufunuo wa Yohana’.

Tena basi, asili khasa ya Ukuhani wa Milele hata Milele, Melkizedeki – Mtu/UTU katika 13 ya Shauri, ni ‘Tunda la Maarifa na Maarifu’ kushughulika ‘Ontolojia ya Taasisi’ kwa Mazazi ya Jamii zenye Utu – Duniani na Kote Ulimwenguni.

Katika mapokeo ya Ukristo, Huduma ya Yesu ilikuwa na Dhamira ya Miundo na Matendo ya Yesu (1) na Wateule 12 kufanya ‘Tunda la Maarifa na Maarifu’ ya Ujamii katika ‘Usahihi wa Kimifumo’. Hili ndilo lafanya Shauri la kuwa ‘Hekima-Nguvu-Utukufu’ ni jambo la wanajamii, wanajamii katika nchi/Dunia/Sayari, kufanyika sifa na sura ya kimatendo na utukufu kama ilivyo katika fahari ya ‘Mbingu’; ambavyo (x) ‘Nchi’ na miili ya Nyama ni ‘Horizoni ya Wakati’ kwa ajili ya (y) Maajilio/heraldri ya ‘Hekima-Nguvu-Utukufu’: kwa Sifa, Sura na Hadhi ambayo Mtume Paulo aliitaja kama ‘Umoja katika Mwili wa Kristu’ , ilivyo pia ni Roho ya Utendaji kwa kadiri ya ‘Imani-Tumaini-Upendo’-- 1 Wakorinto 13.

Kiufundi, Utamaduni kwa Bara la Afrika na hata Dunia Nzima ni mapana ya Kijamii yenye Nasibu ya ‘Dhamma’ ya ‘Liberiti Afrika’; ambavyo ‘Hekima-Umoja-Amani’ ni jambo lile la ‘Hekima-Nguvu-Utukufu’ kwa kuwa ‘Umoja ni Nguvu’ na tena ‘Utukufu ni Nuru ya Uzuri’. Hili lafanya ‘Amani’ katika jamii ni Zao la ‘Utulivu’ ; na kumbe utulivu huja kulingana na (1) Utangamano wa Kijamii ama (2) Mapoooza/Unyonge wa Kijamii.

Kwa mintarafu ya hivi, simetria, koherensia na mipangilio ya elementi za jambo ama jamii ni epistimolojia ya ‘Uzuri’ na ‘Hekima’ ya mambo; ambavyo ‘Uzuri ni Shani ya Mvuto’ kwa Akili na Utambuzi wa mambo kufanya ‘Ukukufu’ ni ‘Nuru ya Watu’.

Basi ndiyo yawa, Dhamma ni Uadilifu wa Mema yenye kukadirisha Shani Bora ya Utu Jumuishi kama fanusi ya ‘Nyota ya Rehema’. Hili lafanya ‘Liberiti Afrika’ ni Shauri la kudhamiria kuifanya Afrika ni Nchi yenye Wanajamii walio na Mwangaza kwa ajili ya Kujikomboa kutoka kwenye Unyonge utokanao na kunyonywa/kunyonyana kwa namna yeyote ile na tena ili kudumisha ‘Heshima ya UTU’ kwa gharama ya mageuzi yeyote yale ya kijamii na Uzima wake.

‘Utangamano wa Kijamii’ ndiyo ufunguo wa ‘Nuru ya Watu’, watu/wanajamii wenye ‘Utukufu iliyo ni Nuru ya Uzuri’ kwa UTU wao Bora. Hili lafanya ‘Usahihi wa Kimifumo’ ndiyo khasa kiini cha utangamano wa fanusi za kiutendaji za jamii kwa ajili ya NENO/Shauri la ‘Ufalme-Nguvu-Utukufu’ : Mambo ya ‘UFAHAMU KRISTU’ ilivyo ni Sura yake MUNGU –kwenye mapokeo ya Kikristo.

Utu katika mapokeo ya UKristo hufaragua ‘Mtu Yesu’ kama ‘Kiini cha Chachu ya Nia ya Utu Bora’ japo kiukweli khasa wa mambo Mwanajamii yeyote yule mwenye Usentienti-Konsayansi-Nuru ya Ufahamu anaweza kuwa ‘Sura ya Mungu : Fanusi ya Utendaji iliyo ni UFAHAMU KRISTU’.

Kila mwenye kuiishi ‘Sala na Kazi’ ni ‘Mwana wa Mungu’ kwa kuwa ‘Kristu huwa ndani yake’ na yeye kuwa ndani ya Kristu; Mtu/Mwanajamii awaye katika Sifa, Hadhi na Daraja la Nuru ya UFAHAMU KRISTU huwa ni ‘Muungwana’; Uungwana ni vitendo ambavyo atendaye katika Ufahamu wa Kristu, yeye kama mtu si mtendaji khasa—ni ‘Kristu ndani yake ndiye hutenda’.

Mapoooza/Unyonge wa Kijamii ndiyo kibano cha ‘Giza’ la Kuukosa Mwangaza wa ‘Nyota ya Rehema’ katika mapana ya ustawi wa Jamii; ambavyo ‘Kristu’ ni mwangaza kwa ajili ya Rehema na tena fadhili kwa ‘UTU BORA’ na tena ‘Nuru ya Uzima’ kwa ‘Dhamma’. Katika ‘Neema ya Sala’ na tena kule Kuazimia ‘Afrika Mpya’ : kuimba juu ya ‘Sote kufurahi kwa Ukombozi Wetu’ ni Mbegu ya u-JUA-ji kwa ‘Nyota ya Rehema’ – Nuru ya Ufahamu kwa kusudi la ‘Uhuru na Umoja’ ili kuifanya Afrika ‘Mti wa Uzima’.​

....
++++

View: https://www.youtube.com/watch?v=AMm-akgqdpE
 
Bwana akubariki ndugu.
 
Tafsiri zote ulizozitoa Kuhusu Melkizedek ni self implication hakuna Mahali maandiko yamemtaja wala Kumvisualise kama Ni Yesu..
Na Ukiangalia Sifa za Melkizedek Yesu hafit hata Moja
 
Tafsiri zote ulizozitoa Kuhusu Melkizedek ni self implication hakuna Mahali maandiko yamemtaja wala Kumvisualise kama Ni Yesu..
Na Ukiangalia Sifa za Melkizedek Yesu hafit hata Moja
Ebr 7:15-17 SUV
[15] Tena hayo tusemayo ni dhahiri sana zaidi, ikiwa ametokea kuhani mwingine mithili ya Melkizedeki; [16] asiyekuwa kuhani kwa sheria ya amri iliyo ya jinsi ya mwili, bali kwa nguvu za uzima usio na ukomo; [17] maana ameshuhudiwa kwamba, Wewe u kuhani milele Kwa mfano wa Melkizedeki.

Zab 110:4 SUV
[4] BWANA ameapa, Wala hataghairi, Ndiwe kuhani hata milele, Kwa mfano wa Melkizedeki.


Melkizedeki na Yesu wote walifanyika makuhani bila kujali sheria "Sheria inasema Kuhani anatoka kabila moja tu la Walawi"
 
Sasa Huwezi kulinganisha Kumbuka Melkizedeki hana Baba wala mama wala hana mwanzo wala Mwisho
 
Kumbuka Hapa katika hii siri ndipo palipoleta mgawanyiko na mkanganyiko mkubwa kati ya Ukristo na Imani nyingine kama vile uislamu, Na hapa hapa ndipo palipoleta migawanyiko mingine mikubwa katikati ya wakristo wenyewe.
Matriksi : Mchanganyiko wa Ukweli na Uongo kwa mapenzi ya 'Asili zetu ya Dhamiri zetu zilizoanguka'...

Siyo kila king'aacho ni dhahabu...

Sasa, Aprili/Mei 2025, tupo kwenye kipindi cha 'KUJIMULIKA'; na tena kuiishi hii nasibu ya kuikata minyororo yenye 'Kufyatua Ridhaa ya Kutawalika': Iwe kidini, taasisi vimvuli vya dini kwa ajili ya UTU-MAISHA-UISHO, sayansi/tekinolojia n.k

Mavuno kwa Ulimwengu: Utenganisho wa Pumba na Uwele wa Maisha na Kujichagulia...

Aprili/Mei 2025 sasa 'Hukumu' imeanza rasmi--Kila mwenye Usentienti, Konsayansi na Nuru ya Ufahamu atafute kujua ilivyobora na aichunge dhamiri yake--Je, kuchagua mabatili ya ubabiloni ama kuutafuta 'Usahihi wa Kimfumo'?

... Kifungo cha Kufikirika ilivyo ndiyo Matriksi ama KUTOKA?

Mwanajamii -- Simama Uhesabiwe WEWE ULIYE, SIMAMA NA UISHI !

Hmmm
====

View: https://www.youtube.com/watch?v=A-hB3vIR3ug
 

Attachments

Sikufichi mkuu, hizi story za akina Allah na Jehovah, huku zishapitwa na wakati hakuna mtu anaweza kupoteza mda wake kusoma huu upuuzi uliouandika hapo, duniani watu wapo busy kuweka history,wapo busy kuenjoy maisha wewe Baki na ujinga wako kwamba mungu alikuwa, mara alifanya,mara aliweza,mara alijaribu. Ujinga na upuuzi huu mnarithisha Hadi watoto wenu,
 
Mkuu hiyo ID yako inamuongelea nani?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…