Huyu binti ni mrembo kwa kweli, ila hapa tu ndo anaponikoseshaga raha

Mwanabalagha

Senior Member
Nov 11, 2015
196
235
Habari za jioni wakuu?

Kwa uwezo wa MUNGU natumain nyote mu wazima. Mi ni mgeni humu kwa kuleta post ila ni mwenyeji sana wakusoma post za watu mbalimbali humu tangu enzi za mwalimu.

Sasa picha linakuja hivi mimi ni kijana wa kiume, naishi kwangu yaan nimejitegemea tayari.

Katika kupitishapitisha macho sehemu mbalimbali, siku moja jicho langu likagota kwa msichana mrembo japo sio sana, ila anafaa kwa matumizi ya nyumbani.

Nilimfata nikachonga nae kidogo tukabadilishana namba na mambo mengine yakaendelea kama mnavyojua kifuatacho i.t.v ni.

Sasa tatizo alilonalo huyu mrembo ni mdomo, yaani mdomo unanuka sio kidogo, ukilala nae huwezi kuvumilia msogeleane hata pumzi anazotoa ni vivyohivyo, sasa hapa kinachonipa mawazo ni namna ya kumuambia.

Yaani sijui nianzeje ili asione labda namkashifu, manake anapenda sana romas, sasa akinisogezea tu uso wake huwa natamani kuzimia.

Naomba ushauri wakuu nifanye nini ili niepukane na hii dhahama? Manake inavyoonekana yeye mwenyewe hata hajijui kama ana tatizo hilo.

Naomba kuwasilisha.
 
watu wakiambiwa wacheni umbea na majungu hawataki...matokeo yake ndiyo kama haya midomo kunuka...huwa ananuka mdomo wakati wa kulala tu ama hata mchana?

Ni muda wote mkuu....saa nyingine huwa natamani niwe nae ila nikikumbuka tu hiyo hali yake, hamu yote inaisha.
 
Duuh pole i real understand you niliwahi kuwa na boyfriend very very smart and handsome lakini hana harufu nzuri ya mdomoni,kusema ukweli nilikosa courage ya kumuambia kwa hyo nikampotezea tu.natamani niweze kumwambia kwa sababu bado ni marafiki
 
Kabla ya tukio kuanza nenda kaswaki wewe kwanza then kaoge na ukimaliza mwambie dawa na mswaki hii hapa na maji ya kuoga nishakutengea bafuni. Mdogo mdogo atakuelewa tu
 
Kaka Mimi sio daktari ila nimewahi kusoma mahali kuwa harufu ya mdomo inasababishwa na bacteria kinywani wanaotokana na usafi hafifu wa kinywa kwa miaka mingi. Mpeleke kwa Dr wa meno/dentist
 
Mtoa mada nimekuelewa vizuri kwani mimi pia nimeshapata tatizo kama lako kbs kwa 100%mdomoni na akipumua anatoa harufu mbaya na kali.

Sababu inaweza kuwa mojawapo ya vifuatavyo:-

-vidonda vilivyopo mdomoni au kwny fizi,na vinasababishwa na Bacteria.

-Kutopiga mswaki japo mara mbili kwa siku...asbh na jioni

-kujaa gesi tumboni mara kwa mara.

-kutojisaidia hajakubwa kwa muda mrefu baada ya kula

-Kutopenda kunywa maji mara kwa mara tena anapaswa kuchangana na limao.

-Kutoongea kwa muda mrefu.

SULUISHO:

-Atumie dawa kali ya meno yenye nguvu,napendekeza zlya Aloe vera original (ya forever living) au Colgate LAKINI PIA na mouthwash (Napendekeza Listerine mint) mara 2 au 3 kwa siku.

-Karafuu na Limao pia zinasaidia sana.

Kama imekuwa chronic nenda hospital kwa dentist yeyote akusaidie.
 
Ushauri mzr na wenye kusaidia bigup mkuu,nami naongezea kidogo,andaa mazingira sahihi,wakati sahii na tumia maneno stahiki kumweleze tatizo alilonalo na muanze tiba.
 
Mtoa mada nimekuelewa vizuri kwani mimi pia nimeshapata tatizo kama lako kbs kwa 100%mdomoni na akipumua anatoa harufu mbaya na kali.

Sababu inaweza kuwa mojawapo ya vifuatavyo:-

-vidonda vilivyopo mdomoni au kwny fizi,na vinasababishwa na Bacteria.

-Kutopiga mswaki japo mara mbili kwa siku...asbh na jioni

-kujaa gesi tumboni mara kwa mara.

-kutojisaidia hajakubwa kwa muda mrefu baada ya kula

-Kutopenda kunywa maji mara kwa mara tena anapaswa kuchangana na limao.

-Kutoongea kwa muda mrefu.

SULUISHO:

-Atumie dawa kali ya meno yenye nguvu,napendekeza zlya Aloe vera original (ya forever living) au Colgate LAKINI PIA na mouthwash (Napendekeza Listerine mint) mara 2 au 3 kwa siku.

-Karafuu na Limao pia zinasaidia sana.

Kama imekuwa chronic nenda hospital kwa dentist yeyote akusaidie.

Asante sana mkuu, shukrani kwa msaada wako ngoja nianze kulifanyia kazi.
 
  • Thanks
Reactions: Art
ni just simple before hamjalala mwambie tuswaki halafu msisitize aswaki ulimi,asubuhi mkiamka swakini pamoja halafu msisistize aswaki ulimi.basi inakuwa umesolve tatizo kwa namna hiyo maana huko kunuka mdomo ni vile haswaki ulimi
 
Kamnunulie mouth wash, wengine wanasema tatizo linaweza kuwa limeanzia tumboni. Tafuta ushauri wa daktari
 
Back
Top Bottom