
NDIO MFALME SASA
Kaumu vumilieni ndivyo hivyo ishakua
Yeye kashiika mpini kiongozi bwana juha
Haya mwingi akilini hata ma
mbo ya murua
Sasa ni Maliki wetu Muhimu kumuelewa
Muhimu kumuelewa qatu hatokusumbua
Fanya anavyo elewa baa lita kukimbia
Huwa kama amelewa mambo anavyo fatua
Sasa ni Maliki wetu Muhimu kumuelewa
Ahwali huzi finyanga na ufuko kumzidi
Amali kwake ujinga baraka ya ukaidi
Fata anavyo ya panga yeye kwake maridadi
Sasa ni Maliki wetu Muhimu kumuelewa
Mbishi haaambiliki atakavyo itakua
Kaidi hasemezeki ukisema kakungoa
Jadidi Wa hikinahiki hizo khabari za juha
Sasa ni Maliki wetu Muhimu kumuelewa
Naomba mufahamu mfalme wetu juha
Hijutia usanamu mambo ya
Kimsumbua
Msemeni kwa nidhamu ujumbe na wapatia
Sasa ni Maliki wetu Muhimu kumuelewa