Huwa hakuna msamaha wa kodi bali huhamishiwa kwingine

MamaSamia2025

JF-Expert Member
Mar 29, 2012
10,221
22,295
Nawasalimu kwa jina la CCM

Kama kichwa cha habari kinavyojieleza ni kwamba nasisitiza hakuna hoja inayotamkwa bungeni kwa bahati mbaya. Mbunge akisimama na kuanza kuzungumza tukubali kwamba tayari ilishapangwa na kufikiriwa. Hakuna bahati mbaya wala nini. Tusikimbilie kumbeza mbunge na kumwita kilaza au ana roho mbaya.

Majuzi hapa alisimama mbunge Zungu na kutaka tukatwe tsh 50 kila siku kwenye simu zetu ili kulipa kodi ya uzalendo. Siku kadhaa baadae tumeona Waziri wa fedha akija na kodi za kwenye miamala ya fedha na muda wa maongezi kwamba ni kodi za uzalendo. Kumbe Zungu alikuwa anatuandaa tu kisaikolojia kwa kile kilichokuwa kinaenda kutokea. Hii kodi ya uzalendo ni kodi ya kichwa iliyoboreshwa. Na ni zaidi ya kodi ya kichwa kwasababu hii watalipa hata watoto wadogo tofauti na ile ya kichwa.

Nyakati fulani katika haya maisha ya dhambi aliwahi kuniambia kitu msichana mmoja kwamba kamwe serikali haijawahi kusamehe wala kufuta kodi yoyote. Kinachofanyika ni kodi hii kuhamishwa hapa na kupelekwa pale. Hii serikali yetu imefanya ubunifu wa kuondoa TASKFORCE kwenye kukusanya kodi lakini ni kwamba watu wote tupende tusipende lazima tulipe kodi. Hii haina kukwepa. Utaamua umeze au uteme.

Binafsi najua kuna kibano kikali kinakuja kwasababu ya hii miradi mikubwa kama SGR, bwawa la umeme nk. Pia waziri kasema barabara zitazidi kujengwa kwa kupitia "kodi ya uzalendo".... naisihi sana serikali ya CCM itumie vizuri hela zitakazopatikana kufanya mambo waliyotuahidi yatafanyika kupitia hii kodi ya uzalendo. Yale mambo ya kusikia maafisa flani wamefakamia bilioni kadhaa kifisadi hayatavumilika.

KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI
 
Hela ikishaingia serikalini huwa hairudi hapo mmachofanya ni set off ya madai unahamishia kwingine Ila cash huwa hapewi mtu utadai mpaka ufe.
 
Back
Top Bottom