Huumizwi bali wewe mwenyewe unachagua kuumizwa

Galacha Maestro

JF-Expert Member
Sep 29, 2011
1,353
2,220
HUUMIZWI BALI WEWE MWENYEWE UNACHAGUA KUUMIZWA

Tunapokuwa na mipango na watu wengine, na watu hawa wakawa na eneo lao ambalo wanatakiwa walitekeleze ili na sisi tuweze kutekeleza eneo letu, tunaweka mategemeo yetu makubwa kwa watu hao.

Na inapotokea kwamba watu hawa wakashindwa kutekeleza lile eneo lao, na hivyo sisi tukashindwa kutekeleza eneo letu pia, tunaumia na tunasema watu hawa wametuumiza.Lakini je ni kweli kwamba watu hawa wanatuumiza? Ni kweli kamba mtu anaweza kukuumiza?

Jibu ni hapana, hakuna mtu anayeweza kukuumiza wewe, hasa kihisia. Bali wewe mwenyewe ndio unajiumiza, wewe mwenyewe ndio unachagua kuumia. Na unaumia kweli kwa sababu unajipa mwenyewe maumivu.

Kwa mfano kwa mtu huyu ambaye alitakiwa kutekeleza eneo lake ili na wewe utekeleze lako, vipi kama usingeweka mategemeo yako yote kwa mtu huyu? Vipi kama ungeangalia njia nyingine mbadala ya kuhakikisha unaweza kutekeleza eneo lako hata kama mtu huyu atashindwa kutekeleza eneo lake? Je bado ungeumizwa kwa yeye kutokutekeleza eneo lake?

Hapa huwezi kuumia kwasababu unakazana kuendelea kufanyia kazi eneo lako. Na ndio maana nakuambia ya kwamba kuumia au kuumizwa kihisia ni wewe mwenyewe unayefanya, na sio mtu mwingine anafanya hivyo.

Labda tuangalie ni vitu gani vinakuwa vinakuumiza katika hali kama hizi;

1. HASIRA.
Je kuna mtu anakuja na hasira na kuziingiza kwenye mawazo yako? Jibu ni hapana, unatengeneza hasira mwenyewe.

2. HOFU.
Je kuna mtu anachukua hofu na kuijaza ndani yako? Jibu ni hapana, hofu unatengeneza mwenyewe kwenye mawazo yako.

3. CHUKI.
Nani amewahi kupewa chuki na mtu mwingine? Hakuna, hii inaanzia ndani yako.

Hivyo kabla hujatuambia kwamba umeumizwa, hakikisha una ushahidi kwamba mtu alikuja na hasira na akazipandikiza kwenye mawazo yako na pia hakikisha ulijipanga vizuri kwa kila changamoto. Lakini ukweli ni kwamba hakuna anayekuumiza, unajiumiza mwenyewe.
 
Maumivu ya moyo yasikie tu kwa wenzako
Binadamu by nature tuna expectations kutoka kwa wengine and it's right to expect, utakuwa hujithamini km huna viwango vya kutaka kuwa treated the way unawatreat wenzio,refer to the Golden Rule
Hatujiumizi all the tym tunaumizwa pia
 
Asante kwa maoni.
 
Hiyo imekaa vizuri mkuu kuna ukweli ndani yake , unaumia sababu uliweka matumaini mengi sana kwake
 
Yes! nakubaliana na mtoa mada,maumivu ni choice,kuna kitu kinaitwa "psychological Identity",ni ile hali ya kujimilikisha uhusika,it means unamtegemea binadamu au kitu,mfano umeshajijenga kisaikolojia na kimazoea dhidi ya kitu flani,mfano umeajiriwa unafanya kazi mahali umeizoea hiyo kampuni mpaka umejipa ownership kwenye hiyo kampuni,siku ikitokea umefukuzwa kazi utaumia sana,au una mpenzi(boyfriend/girlfriend) na umejiwekea na umezoea wewe ni yeye na yeye ni wewe,siku ikitokea amekuacha unaumia sana coz ulishakuwa na psychological identity dhidi yake na subconscious mind yako ilishaamini hivyo,hiyo ni mifano tu ya mazoea tuliyonayo wanadamu bila kuwa na mbadala hivyo ikitokea kinyume tunaumia sana,so sometimes pain is a choice,ndio maana walio na imani wanasema its better uwe na "psychological Identity with God",maana yeye mungu hafi...nina mambo mengi ningeweza ku share hapa lakini kwanza niishie hapa!
 
Asante kwa maoni yako.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom