Huu Utapeli Hauzeeki tu?

Alola

JF-Expert Member
Joined
Nov 14, 2013
Posts
476
Reaction score
300
Habari, naitwa Mr. Raymond from EUROCARTA LTD Dar, tupo kikaoni tunapitia CV tuchague candidates wa kuinterview for I.T. OFFICER POST, salary ni 1,200,000/=. CV yako ni nzuri nataka kukusaidia upate hii kazi, kwa terms zifuatazo, ukishaanza kazi utanipa laki 3, na kabla ya saa 9 mchana uwe umetuma sh. elfu 40 by tigopesa to 0713-765442 ili nimpe mtu wa interview amesema anataka hiyo hela leoleo ili atoe maswal ntakutumia kwenye e-mail for now siwezi ongea mpaka badae nikitoka kikaoni na ndio muda huo utapigiwa simu lini uje for interview, jitahidi utume mapema.
 
Message za aina hiyo hata mimi kuna mmoja alinitumia,wala sikuhangaika naye,utapeli huo Tigo wanaweza kuukomesha mimi nataka niwaeleze tigo inaharibu company image kama watu wanaweza kutumia network yako kutapeli watu.Sidhani kama kuna mtu anatumiwa na hao matapeli wanakwambia uwatumie kwa Mpesa,voda wako smart hawaruhusu vitu vidogo vidogo kama hivi kuwaharibia heshima.Tigo amkeni mrudishe heshima ya network yenu hiyo namba iko kwenye system account mnaweza kuifunga au kumzuia asizitoe.
Hawa jamaa kwanini wanajiamini aidha wanajua network zinavyofanya kazi au hawajui,tena inawezekana hata majina walisajiri feki,kwani makampuni ya simu sometimes yako interested kupata wateja bila kuhakiki details.Sikumoja kampuni moja walikuwa wanauza line,nikawambia mimi sijatembea na kitambulisho changu cha mpiga kura,unaweza amini jamaa waliniambia kama nazikumbuka namba niwatajie tumalize business.Hapo sinaweza jitengenezea namba za uongo.
Utapeli huo hata polisi hawaitajiki only tigo can solve it sema sasa customer care yao mmhh.
Lakini tujiulize namba zetu wanapata wapi? Kwani kampuni wanayokutajia kwa mfano mimi sikuwahi kuomba kazi huko.
 
Wanatangaza kazi, watu wanatuma CV then wanapata info
 
Yaani mtu anajitambulisha kwangu halafu anasema anaitwa Mr. Raymond. Hilo tu tayari ni kosa, huwezi kuji address mwenyewe Mr. Ukiona hivyo ujue utapeli unakunyemelea.

Tiba
 
You are very smart Tiba
 
Ishskua cliché watafute kingine cha kudanganyia basi yaani hats ubunifu hawana
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…