Huu ndiyo mfumo tunaotaka ufumuliwe.

Allen Kilewella

JF-Expert Member
Sep 30, 2011
20,411
38,703
Kumekuwa na mjadala wa muda mrefu sana humu JF kuhusu kama tatizo la mkwamo wa kisiasa nchini mwetu ni la kimfumo au ni la watu waliomo kwenye mfumo. CCM wanasema tatizo ni watu na wala si mfumo wakati wapinzani wao wanadai tatizo ni mfumo. Hivi mfumo unaobishaniwa ni upi huo?

Kwa kuwa tumerithi mfumo wa kiutawala wa Kiingereza basi na tafsiri yake kuhusu mfumo huo ni lazima itokane na waingereza hata kama mbele ya safari dhana kuhusu Mfumo itatofautiana nao.

Govern = to legally control a country or its people and be responsible for introducing new laws, organizing public services.

Tafsiri ni ya kwangu: Kutawala ni kuidhibiti nchi au watu wake kihalali na kuwa na wajibu wa kutunga sheria mpya, na kutoa huduma za Jamii.

Government = the group of people who are responsible for controlling a country or a state.

Tafsiri ni ya kwangu: Serikali ni kundi la watu wenye wajibu wa kuidhibiti nchi.

= The activity or the manner of controlling a country

Tafsiri ni ya kwangu: Serikali ni Shughuli au mwenendo wa kuidhibiti nchi.

= A particular system or method of controlling a country.

Tafsiri ni ya kwangu: Serikali ni mfumo au mbinu maalum ya kuidhibiti nchi.

Control = the power to make decisions about how a country is run

Tafsiri ni ya kwangu: Udhibiti ni mamlaka ya kufanya maamuzi jinsi gani nchi inaendeshwa.

The system = The rules or people that control a country or an organization.

Tafsiri ni ya kwangu: Mfumo ni kanuni au watu wanaodhibiti nchi au taasisi


Kwa tafsiri hizo hapo juu ni kwamba Serikali ni kundi la watu lenye wajibu wa kufanya maamuzi jinsi gani nchi iendeshwe kwa kutumia mbinu na kanuni maalumu ili kuidhibiti nchi. Kundi hilo la watu pia limepewa jukumu la kutunga sheria na kutoa huduma za jamii.

Hapo hapo tunaposema mfumo tunamaanisha vitengo vya dola ambavyo vina kazi ya kusaidia hilo kundi la watu katika kuidhibiti nchi, Kwa ivo kumbe ni lazima kuwepo na kanuni fulani ambazo zinatumika ili kuidhibiti nchi. nchi haiwezekani ikadhibitiwa kiholela.

Katiba ya Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Ibara ya 8 Kifungu kidogo (a) kinasema wananchi ndiyo msingi wa mamlaka yote, na serikali itapata madaraka na mamlaka yake yote kutoka kwa wananchi kwa mujibu wa Katiba hii. kwa maana nyingine hicho kikundi cha watu hayo mamlaka ya kuidhibiti nchi ni lazima yatoke kwa wananchi na wala chenyewe kisijipe mamlaka ya kuidhibiti nchi kitakavyo.

Tunaotaka mfumo ubadilishwe hoja yetu inatokana na Katiba ya sasa. Ukiisoma Katiba yetu kwa makini pamoja na sheria zilizotungwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano na zile sheria tulizoziasili (adapting) toka wa wakoloni, utaona nafasi ya Kikundi hicho cha watu kujitwalia madaraka bila ya kuyapata toka kwa wananchi ni kubwa mno.

Tunataka mfumo wa kutunga sheria, kusimamia sheria, kutawala, unaohusu mahusiano kati ya kikundi hicho cha watu na wananchi, uwe bora zaidi kuliko ulivyo sasa. Tunataka siyo tu kwa nadharia bali kiahalisia wananchi ndiyo wawe wanatoa mamlaka kwa kikundi hicho cha watu nini kifanyike kwa manufaa ya wananchi na nchi kwa jumla.

Tunataka kabla ya kufanya maamuzi kwa niaba yetu ni lazima watu hao washirikishe wenye mamlaka kwao ambao ni wananchi. Kuna watu watauliza watashirikishwaje zaidi ya hivi wanavyoshirikishwa sasa? Kikuhalisia tunataka mamlaka za kukaguana (Checks and Balance) ziwekewe mipaka iliyo wazi kabisa ili kuzuia mhimili mmoja kuingilia mhimili mwingine. Tunataka wanaotunga sheria (Bunge) wasiingilie wanaotafsiri sheria (Mahakama) wakati huo huo tunataka wanaotekeleza sheria (tawi la Utendaji) nao pia wasiingilie mamlaka za wenzao.

Tunaposema tunataka mfumo ufumuliwe tunamaanisha Katiba iliyopo na sheria zake zinazowapa kundi hili la watu mamlaka ya kufanya maamuzi kwa niaba ya wananchi ziandikwe upya ili ile dhana kwamba Wananchi ndiyo msingi wa mamlaka yote iwe halisia na itekelezwe.

Maaelezo ya Kiingereza nimeyatoa kwenye Kamusi ya Kiingereza ya "Oxford ADAVANCED LEARNER'S Dictionary, International Student's Edition. 7[SUP]th[/SUP] edition".
 
Umeyaformalaiz mawazo yangu. Asante
Bado tuna safari ndefu sana kwenye kujenga tafakuri ya jamii yetu ili iweze kushughulika na vyanzo vya matatizo badala ya matokeo yake. Hayo yanayoitwa majipu kama tungekuwa na mfumo usiosubiri mtu kwa utashi wake binafsi ndiyo aje kutumbua majipu, hii nchi ingekuwa mbali sana.

 
Ninauwakika kushindwa kwa magufuli itakuwa ndyo mwanzo wakurudi nyuma nakutambua chanzo cha matito yetu. Then baada ya hapo tutaanza kwenda sawa
 
Back
Top Bottom