Huu ndio ukweli kuhusu mkataba wa DP world na serikali unaofichwa na viongozi wengi. Tumekukosea nini Mungu sisi watanzania?

Huo uchambuzi ulioambatanisha ulifanywa na nani? Kwa nini unasema ulifichwa? Mbona mkataba huu umechambuliwa na watu wengi tangia utoke, wakiwemo magwiji wa sheria kama Prof Shivji? Nini kipya kwenye hiyo document uliyo attach?
Huo ndio uchambuzi wangu, naamini unaweza kuona kama ni porojo au uzembe wa serikali. Acha majungu
 
Wazalendo Mungu awabariki sana
 
Nimekuwa nikijuuluza mara nyingi sana.
Tanganyika (Tanzania) ndiyo yenye rasilimali. Lakini koote huko imelazimika kufuata draft za so called wawekezaji. Why ?!. Tuna tatizo gani ?!. Upungufu wa akili na kujiamini au ni umasikini naturally.

Kwenye migodi, hivyo hivyo. Kwenye Gas na mafuta, mbuga zetu za wanyama ni hivyo hivyo. Tuna nini , umasikini wa mawazo au tunatetemekea weupe ?!.
 
Jungukuu halikosi ukoko jamani, kunyoa panki huyeyusha ubongo mtupu, kipofu huwa haoni hata kwenye mwanga wa jangwani. Kiziwi huwa hasikii hata kwenye moto wa jaaanam.Hoja hujibiwa kwa hoja na sio matapishi. Ambaye hajaona pdf anijulishe, vilevile naiweka tena 🙃
 

Attachments

  • Analysis-DP world contract.pdf
    8.4 MB · Views: 3
Hili ni swali ambalo viongozi wa nchi hii wana wajibu wa kulijibu. Siyo swali dogo hata kidogo, ni swali la msingi kabisa.

Mtu yeyote akiwa na uhitaji, huenda sokoni kununua mahitaji yake, soko/duka haliendi kwa mnunusi.

Hawa viongozi kila siku wanatuimbia "kuvutia/kujiuza"...., kuweka mazingira rahisi, n.k.,. Na kwamba tumo kwenye ushindani wa "kujiuza"; kwa hiyo tujiuze kwa masharti hata yasiyokuwa na manufaa kwetu. Huu ni ukichaa!
 
Huo ndio uchambuzi wangu, naamini unaweza kuona kama ni porojo au uzembe wa serikali. Acha majungu
Mbona umeshachelewa. Hitimisho la huu mjadala ni kesho kutwa, tarehe 10 August 2023 huko Mahakama Kuu ya Mbeya. Kiakacho amriwa huko itakuwa ndiyo.
 
Nimeweza kuusoma,umejadili kwa urahisi na lugha inayoeleweka.
Kazi nzuri!
 
Haionyeshi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…