Huu mtiririko wa vyeo nchi hii masikini, Rais angalia uwezekano wa restructuring

MSEZA MKULU

JF-Expert Member
Jul 22, 2011
3,763
5,591
1: Afsa Mtendaji wa kijiji

2: Afsa mtendaji wa Kata

3: Afisa Tarafa

4: diwani

5:Meya/mwenyekiti wa almashauri

6:Mkurugenzi

7:Mwenyekiti wa kijiji

8:Mwenyekiti wa mtaa

9:Mwenyekiti wa kitongoji

10:Katibu tawala wa wilaya

11 Mkuu wa wilaya

12:Katibu tawala wa mkoa

13:Mkuu wa mkoa

Yawezekana wengine nimewasahau, Siku za hivi karibuni dunia inashuhudia mabadiliko makubwa na ya kasi yenye kuleta changamoto kwa wakaazi wake (agility).

Mifumo iliyokuwa inafanya kazi zamani leo haina nafasi na yawezekana ikawa chanzo cha matokeo hafifu kabisa na utendaji wa spidi ya kobe. Mtego mkubwa kwa taifa ni HOfu ya kutokukubali Mabadiliko haya. Wakati wake ni sasa.

Taasisi Moja Kubwa Duniani Baada ya kujitafakari waligundua chanzo cha kusuasua kwao ni kwa sababu ya uwepo wa REPORTING STRUCTURE Ndefu na Muningiliano wa majukumu, huku hii kitu ikiacha mianya mingi ya UZEMBE,MAJUNGU,UVIVU, KUKWEPA MAJUKUMU,.

WAlifupisha Kutoka stage nane hadi nne na ikaleta matokeo chanya ndani ya muda mfupi. Ila ilibidi NAFASI ZIUNGANISHWE, VYEO VIONDOLEWE, MAJUKUMU YATAWANYWE NA KUTAZAMWA UPYA.

Napendekeza taifa lipitie upya Mfumo wake wote uliowekwa Miaka zaidi ya 45 iliyopita. Yawezekana Ulifaa wakati huo ila Dunia ya sasa na Tanzania ya inahitaji Kitu Bora zaidi ya uoga wa mabadiliko. Na hii Inapenya ndani zaidi ya MABADILIKO YA KATIBA.

CHEO CHA KWANZA KUONDOLEWA NA MAJUKUMU YAKE KUTAWANYWA AU KUHAMISHA KWA WAHUSIKA TOFAUTI NAPENDEKEZA iwe ni MKUU WA WILAYA NA KATIBU TAWALA WAKE.

VILIO KAMA HIVI VILISIKIKA KATIKA ANGA LA TAIFA HILI TAJIRImasikini MIEZI MICHACHE ILIYOPITA

MABADILIKO = LOWASA,LOWASA =MABADILIKO V/S MAGUFULI FOR CHANGE (M4C)

KARIBU KWA LOLOTE JEMA,
 
Na hapo unakuta tatizo dogo hao wote wanashindwa kulitatua, tatizo ni elimu kwa hao waajiriwa
 
Back
Top Bottom