Pengine mada hii ilishaletwa hapa kivingine na kujadiliwa, ila muungwana unapoona juhudi chanya usisite kuipongeza hata kama utarudia rudia! Nimefuatilia clips kadhaa sasa (ila kwa bahati mbaya mie sio mtaalamu wa kuweza kuzitundika hapa), zinazoonesha michango mbali mbali ya Hussein Bashe bungeni.
Ananipa taswira chanya kwamba, kwanza anasoma makabrasha wanayopewa bungeni; pili, ana ufahamu mpana wa mambo kadhaa hasa kwenye maswala ya biashara, soko la hisa/mitaji, kodi nk; tatu, ana uwezo mzuri wa kujenga hoja za kushawishi kuungwa mkono; nne, ana ujasiri wa kusimamia hoja yake hata pale inapokuwa kinzani kwa maonjo ya watawala!
Simfahamu Bashe nje ya clip nilizozisikia hivyo sina maslahi binafsi naye! Kwenye jangwa la wabunge wa ndioooo, namwona kama mpapai unaochanua kwa matumaini!