Huruma iliyozidi kipimo

shikwashikwa

Senior Member
Joined
Jun 5, 2015
Posts
188
Reaction score
46
Wasalamu wana jamvi,

Ninae mpenzi ambaye miezi 3 mbele panapo majaliwa tutafunga ndoa, nashukuru MUNGU kwani ni mwema kwa kunipa mwenza panapo majaliwa. Huyu mke wangu mtarajiwa ni mpole na mwenye huruma sana anarafiki yake chakaramu kidogo kanizoea lakini hatuna utani nae, anampenda sana rafiki yake mke wangu mtarajiwa.

Kwani katika historia ya urafiki wao kasaidiwa mambo mengi sana sana moja la mfano ni kulipiwa Ada ya chuo mwaka mmoja baada ya ndugu zake kukwama kiuchumi hilo ni moja tu lakini yapo mengi mengi kwa mfano ameshaishi nae mwaka na nusu kwake kula, kulala na kila kitu juu ya rafiki yake. Sasa Jana nilipigiwa simu kuwa anaomba tukutane tuongee nikaona sio mbaya shemu wangu wa nguvu tena nikamuelekeza sehemu huwa pana michemsho mbali mbali, punde akawa amefika.

Baada ya salamu na maongezi ya hapa na pale akasema tafadhali shemu naomba usimsaliti mke wangu mtarajiwa ataumia sana hata kama unafikiria kuwa na mchepuko ni bora hata ukaniambia mimi kuliko kutoka na wanawake wa huko.

Nikamuuliza kwani vipi? Akaniambia eti kuna mtu anapeleka habari kwa wife to be kuwa mimi natoka na wafanyakazi wenzangu na huyo jamaa aliwahi kumtaka akamtolea nje.

Nikakataa na kumuuliza kwani nikitoka na wewe nitakuwa sijamsariti? Akanijibu bora mimi sitakuwa na wivu na nitakuwa na heshima.

Nimefikiria nikaona sababu mbili
1~Nategwa

2~Huyu anahuruma kwa shosti wake lakini hajui kama ndio anamfanyia ukatili.
Nimepanga leo nikutane na mke wangu na nimueleze yote haya, sijui nitakuwa nimekosea?

Naombeni mnishauri kistaarabu

Asante
 
Tumia akili kabla hujamueleza hayo yote. Maana hujui yeye na huyo rafiki yake walipanga nini au wameongea nini.
 
Usimweleze acha ujinga wewe.... Wanaume mmepewa kifua mkanyimwa manyonyo unafikiria ni kwa nini? Be a man maneno mengi .. Kama huna nia ya kumsaliti tulia wewe

Sawa,wasi wasi wangu kama ni mtego na nikiuchuna inaweza kumpa picha mbaya mke wangu mtarajiwa kuwa inaweza kuwa mtego wao umenasa kimya kimya
 
Sawa,wasi wasi wangu kama ni mtego na nikiuchuna inaweza kumpa picha mbaya mke wangu mtarajiwa kuwa inaweza kuwa mtego wao umenasa kimya kimya
kama kakutega kiivyo hana adabu.. wewe usimweleze malizana na huyo shemeji kuwa huna mpangao wa kuchet na hujachit
 
Sasa shikwashikwa si usubiri uone lengo la huyo shemeji ....utamwaambia huyo mpenzi wako nin sasa kwamba umetongozwa ama? Subiri kwanza shikwashikwa na wewe endelea kumtega hadi uone mwisho wake...
halafu kingine anaenda kumweleza mpenzi wake kwa kuwa tu ni shemeji kamwambia .,.. hao mademu wengine wa kitaa atakuwa anapeleka taarifa
 
halafu kingine anaenda kumweleza mpenzi wake kwa kuwa tu ni shemeji kamwambia .,.. hao mademu wengine wa kitaa atakuwa anapeleka taarifa
Kwani yupo na mademu wengine tena? No sidhani jamaa anaonekana mtu safi....:frown:
 
kama kakutega kiivyo hana adabu.. wewe usimweleze malizana na huyo shemeji kuwa huna mpangao wa kuchet na hujachit

Hilo nililiwaza lakini kwa uchakalamu wa huyo shemeji yangu nikimpayukia nahisi anaweza kuungana na jamaa anaemfukuzia mke wangu mtarajiwa japo hiyo stori ya kuwepo kwa mtu huyo kaileta yeye mimi sijathibitisha..labda nianze tabia za kumkwepa bila sababu
 
halafu mkuu unawahi kuoa ila akili yako bado hajpevuka utateseka sana........... HIVI WANAUME WA SIKU HIZI UWANAUME WENU MMEUACHA WAPI?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…