Humphrey Polepole ni nani?

Huyu Prof. Assad subiri siasa imuingie mtaniuliza mwakani report yake itakuwaje.
 
Hii ni CV au kitabu
 
Duuhh hii ni CV au gazeti
 

Dah, natamani nimkate kichwa nikiweke kwangu aisee.

Maasha-Allah.
 
Polepole ana stashada ya juu ya maendeleo ya jamii kutoka chuo cha ustawi wa jamii Tengeru. CV yake nyingine ni kwamba ana bahati ya kupata vyeo kama bashite​
 
Wanajf, yeyote mwenye CV ya ndugu Humphrey polepole aliyekuwa mjumbe wa tume iliyoundwa kwa ajili ya katiba mpya na sasa katibu mwenezi na itikadi ccm aiweke hapa...

Ni baada ya huyu slowslow kuupata ukatibu mwenezi wa ccm ndiyo mauaji, kuteswa kwa wakosoaji wa Serikali, kununuliwa kwa viongozi wa upinzani, watu kuwekwa ndani kwa muda mrefu bila kufuata sheria n.k. ndipo yalipoanza
 
Amechambua au kaleta mipasho tu ya Uswahilini? Hoja za CAG haziwezi ziko nje ya uwezo wake.
Kachambua kwa kufuata taratibu zote za "kimataifa". Bado Da Ummy yeye nae atachambua kwa kutumia vigezo vya WHO. So far tupo kwenye light track
 
Nadhani kwa heshima ya Aina hii kufanya Kazi iliyotukuka ni sawa na kufanya Kazi ya Mungu. Pesa za walipakodi inafaa kuokoa Maisha ya walalahoi wengi mahospitalini na sehemu zingine za huduma ya Umma.



Kumwondoa kazini Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu Sheria ya 1984 Na.15 ib.43 Sheria ya 1995 Na.12 ib.19

144.-(1) Bila ya kuathiri masharti mengine yaliyomo katika ibara hii, Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu wa Jamhuri ya Muungano atalazimika kuacha kazi yake atakapotimiza umri wa miaka sitini au umri mwingine wowote utakaotajwa na Sheria iliyotungwa na Bunge.

(2) Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu aweza tu kuondolewa katika madaraka ya kazi yake kwa sababu ya kushindwa kutekeleza kazi zake (ama kutokana na maradhi au sababu nyingine yoyote) au kwa sababu ya tabia mbaya, au kwa kuvunja masharti ya sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma na hataweza kuondolewa kazini ila kwa mujibu wa masharti ya ibara ndogo ya (4) ya ibara hii.

(3) Iwapo Rais anaona kwamba suala la kumwondoa kazini Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu kwa mujibu wa masharti ya ibara hii lahitaji kuchunguzwa, basi katika hali hiyo mambo yatakuwa ifuatavyo:
(a) Rais atateua Tume Maalum ambayo itakuwa na Mwenyekiti na Wajumbe wengine wasiopungua wawili. Huyo Mwenyekiti na angalau nusu ya wajumbe wengine wa Tume hiyo itabidi wawe watu ambao ni Majaji au watu waliopata kuwa Majaji wa Mahakama Kuu au Mahakama ya Rufani katika nchi yoyote iliyomo kwenye Jumuiya ya Madola; (b) Tume hiyo itachunguza shauri lote halafu itatoa taarifa kwa Rais kuhusu maelezo ya shauri lote na itamshauri Rais kama huyo Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu aondolewe kazini kwa mujibu wa masharti ya ibara hii kwa sababu ya kushindwa
kufanya kazi kutokana na maradhi au sababu nyingine yoyote au kwa sababu ya tabia mbaya.

(4) Ikiwa Tume iliyoteuliwa kwa mujibu wa masharti ya ibara ndogo ya (3) itamshauri Rais kwamba huyo Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu aondolewe kazini kwa sababu ya kushindwa kufanya kazi kutokana na maradhi au sababu nyingine yoyote au kwa sababu ya tabia mbaya, basi Rais atamwondoa kazini.

(5) Ikiwa suala la kumwondoa kazini Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu limepelekwa kwenye Tume kwa ajili ya uchunguzi kwa mujibu wa masharti ya ibara hii, Rais aweza kumsimamisha kazi huyo Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu, na Rais aweza wakati wowote kufuta uamuzi huo wa kumsimamisha kazi, na kwa hali yoyote uamuzi huo utabatilika ikiwa Tume itamshauri Rais kwamba huyo Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu asiondolewe kazini.

(6) Mtu ambaye ni Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu au aliyepata kuwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu hawezi kuteuliwa kushika au kushikilia madaraka ya kazi nyingine yoyote katika utumishi wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…