Hukumu ya kesi ya vigogo wa TANESCO inachekesha

mwembemdogo

JF-Expert Member
Feb 28, 2016
2,282
1,252
Pamoja Na kutokuwa mwanasheria Kwa maana ya kujua Sheria hakika Hakimu aliyeisikiliza kesi hiyo Na hatimaye kutoa hukumu hiyo amenifanya niangue kicheko.Nakubaliana Na kauli ya mwanasheria wa Takukuru kuwa Rushes Mahakama ya kisutu imeshamiri.Mh.Rais kuendelea kuwa Na mahakimu wa aina ya huyu aliyeisikiliza kesi ya vigogo wa Tanesco juhudi za serikali yako zitakwama tunaomba hebu wahamishe weka mahakimu wenye uzalendo Na nchi hii.Tunaishauri Serikali yako ikate Rufaa.
 
Yaani ni mambo ya kustaajabisha sana mie nilidhani nipo peke yangu kuwa na shaka na maamuzi haya-kimsingi kulikuwa hakuna haja hata ya kuwafikisha mahakamani kama maamuzi ni haya
 
Mahakami kinachoangaliwa ni hoja sio story za nje kama takukuru wameshindwa kuwasilisha hoja wasilalamike
Kwa hali hii hakuna fisadi au mhujumu uchumi atatiwa hatiani hata akina mramba bila shaka kuna namna fulani ya siasa ndo maana wamepewa ka adhabu
 
Mkuu unashangaa nini? nchi hii makosa ya matumizi mabaya ya ofisi na kuisababishia hasara serikali adhabu yake ni ndogo sana, hata kama wangekutwa na hatia sana sana wangeambiwa wakafanye usafi ofisi za TANESCO
 
Mahakami kinachoangaliwa ni hoja sio story za nje kama takukuru wameshindwa kuwasilisha hoja wasilalamike

Ninadhani anashindwa kuelezea alichokisikia mahakamani yawezekana ni kituko kiasi kwamba kinakwamisha juhudi ya kupambana na watu wa namna ya mafisadi
 
Pamoja Na kutokuwa mwanasheria Kwa maana ya kujua Sheria hakika Hakimu aliyeisikiliza kesi hiyo Na hatimaye kutoa hukumu hiyo amenifanya niangue kicheko.Nakubaliana Na kauli ya mwanasheria wa Takukuru kuwa Rushes Mahakama ya kisutu imeshamiri.Mh.Rais kuendelea kuwa Na mahakimu wa aina ya huyu aliyeisikiliza kesi ya vigogo wa Tanesco juhudi za serikali yako zitakwama tunaomba hebu wahamishe weka mahakimu wenye uzalendo Na nchi hii.Tunaishauri Serikali yako ikate Rufaa.
Rais ndo huwa anahamisha Mahakimu? Kwa Ukilaza huu bado unaishangaa Mahakama,hujioni kuwa unaweza kuwa na tatizo kichwani?
Elimu,Elimu, Elimu! Rais haingiliani na Mahakama,sawa?
 
baadhi ya watu wachache wanaujumu nchi , ila kwa hii kesi serikali imeshindwa kuthibitisha mashitaka kuna kitu hapa ambacho kimejificha .
 
Mahakami kinachoangaliwa ni hoja sio story za nje kama takukuru wameshindwa kuwasilisha hoja wasilalamike
Ni kweli kabisa usemacho

Kama hao TAKUKURU wameshindwa Ku frame hiyo kesi vizuri sasa unataka hakimu afanyeje?

Pili kama hoja zenu hazina vidhibitisho unataka mahakama awasaidieje?
 
Hakimu ana angalia ushahidi uliotolewa na sio hisia au huruma japo wakati mingine hivi pamoja na rushwa vinabomoa haki - ndio maana kuna rufaa kama huridhiki na hukumu
 
Pamoja Na kutokuwa mwanasheria Kwa maana ya kujua Sheria hakika Hakimu aliyeisikiliza kesi hiyo Na hatimaye kutoa hukumu hiyo amenifanya niangue kicheko.Nakubaliana Na kauli ya mwanasheria wa Takukuru kuwa Rushes Mahakama ya kisutu imeshamiri.Mh.Rais kuendelea kuwa Na mahakimu wa aina ya huyu aliyeisikiliza kesi ya vigogo wa Tanesco juhudi za serikali yako zitakwama tunaomba hebu wahamishe weka mahakimu wenye uzalendo Na nchi hii.Tunaishauri Serikali yako ikate Rufaa.

hapo jipu ni maafisa TAKUKURU waliosimamia hiyo kesi wameshindwa kupeleka ushahidi unaowatia hatiani watuhumiwa. Unapomtuhumu mtu kampa tenda mkewe hata mm sio mwanasheria najua lazima kwanza uhakikishe je ni kweli hiyo kamapuni iliyopewa tenda ni ya mke wa mkurugenzi wa TANESCO?? Pili je hata kama ni ya mke wa mkurugenzi wa TANESCO, Je haina haki ya kuomba tenda hapo? tatu je taratibu zilifuatwa? Mfano kuondoa mgongano wa maslahi je mkurugenzi yeye kama yeye personel alishawishi na kushiriki vikao vilivyotoa maamuzi ya hiyo kampuni ya mkewe kupewa tenda? na hapa lazima udhibitishe kwa fact na vielelezo kama minutes za vikao, list ya waliohudhuria vikao etc, vilevile kama TAKUKURU walichunguza taarifa za kiuchunguzi walizopata waziweke mahakamani ili ziwape uzito wa hoja. Sasa kama wanaenda mahakamani na story za magazetini usitegemee hakimu awape ushindi sababu tu ni TAKUKURU.
 
hapo jipu ni maafisa takukuru waliosimamia hiyo kesi wameshindwa kupeleka ushahidi unaowatia hatiani watuhumiwa. Unapomtuhumu mtu kampa tenda mkewe hata mm sio mwanasheria najua lazima kwanza uhakikishe je ni kweli hiyo kamapuni iliyopewa tenda ni ya mke wa mkurugenzi wa tanesco?? Pili je hata kama ni ya mke wa mkurugenzi wa tanesco je haina haki ya kuomba tenda hapo? tatu je taratibu zilifuatwa? Mfano kuondoa mgongano wa maslahi je mkurugenzi yeye kama yeye personel alishawishi na kushiriki vikao vilivyotoa maamuzi ya hiyo kampuni ya mkewe kupewa tenda? na hapa lazima udhibitishe kwa fact na vielelezo kama minutes za vikao, list ya waliohudhuria vikao etc, vilevile kama takukuru walichunguza taarifa za kiuchunguzi walizopata waziweke mahakamani ili ziwape uzito wa hoja. Sasa kama wanaenda mahakamani na story za magazetini usitegemee hakimu awape ushindi sababu tu ni takukuru.

Umenena vyema mkuu...watz wengi ni wepesi wa kuzungumza bila kufahamu facts...jamaa kachiwa sababu TAKUKURU wameshindwa kuthibitisha hoja zao za matumizi mabaya ya madaraka...sasa wabongo wanatoka povu tu hata km mtu hana hatia...tuna shida bado
 
Hivi hakuna aliyefuatilia hili suala huko mahkamani ili atuandike kilicho tokea huko. Mshtakiwa alijitetea vipi na washtakiwa walikua na ushahidi gani ili tuache kuandika mamabo tusioyafahamu. Sisi wananchi tukijua hilo inakua rahisi kujuwek upande gani...
 
Pamoja Na kutokuwa mwanasheria Kwa maana ya kujua Sheria hakika Hakimu aliyeisikiliza kesi hiyo Na hatimaye kutoa hukumu hiyo amenifanya niangue kicheko.Nakubaliana Na kauli ya mwanasheria wa Takukuru kuwa Rushes Mahakama ya kisutu imeshamiri.Mh.Rais kuendelea kuwa Na mahakimu wa aina ya huyu aliyeisikiliza kesi ya vigogo wa Tanesco juhudi za serikali yako zitakwama tunaomba hebu wahamishe weka mahakimu wenye uzalendo Na nchi hii.Tunaishauri Serikali yako ikate Rufaa.
bora ukatoe ushahidi wewr
 
Back
Top Bottom