figganigga
JF-Expert Member
- Oct 17, 2010
- 25,658
- 55,487
Heshima kwenu wakuu,
Hii kesi ya Richmond siielewi, yaani sijui Sheria inafanyaje kazi kwenye hii kesi. Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Aprili 21, 2017 itatoa hukumu katika kesi ya Richmond inayomkabili mshtakiwa Naeem Gire, hukumu itakayotelewa na Hakimu Mkazi Mkuu Mfawidhi, Cyprian Mkeha.
Gire ambaye alikuwa wakala wa kampuni inayodaiwa kuwa ni kampuni hewa ya kufua umeme wa dharura, Richmond Development LLC, anakabiliwa na mashtaka ya kughushi nyaraka, kutoa taarifa za uwongo na kuwasilisha nyaraka za kughushi serikalini.
Huyu Gare alishawahi kuachiwa huru kuhusu hii kesi kwamba ushahidi hautoshi. Ilikuwa july 28 mwaka 2010.
Baada ya Miaka miwili, kesi ikafufuliwa tena, Gire akaitwa tena mahakamani Juni 6 2012. Soma=>Kesi ya Richmond kufufuliwa
Kesi ikaendelea hadi 21 machi 2017 ndo hukumu itatoka. Kwanini hii kesi inakuwa na danadana sana? Kuna jipya tutegemee?
Haya mambo Sheria yana wigo mpana

Soma=>Mahakama yamwachia huru Naeem Gire wa Richmond.Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu mjini Dar es Salaam, imemwachia huru Naeem Gire aliyekuwa akikabiliwa na kesi ya kughushi na kuwadanganya serikali kuwa mitambo ya Richmond ina uwezo wa kufua megawati 100 za umeme.
Gire ametoka kizimbani akichekelea baada ya hakimu wa mahakama hiyo, Waliarwande Lema , kutamka kuwa anamuona hana kesi ya kujibu kutokana na ushahidi uliofikishwa mahakamani na serikali kushindwa kumridhisha ili amuone kuwa na kesi ya kujibu.
Baada ya Miaka miwili, kesi ikafufuliwa tena, Gire akaitwa tena mahakamani Juni 6 2012. Soma=>Kesi ya Richmond kufufuliwa
Kesi ikaendelea hadi 21 machi 2017 ndo hukumu itatoka. Kwanini hii kesi inakuwa na danadana sana? Kuna jipya tutegemee?
Gire wa Richmond kurejeshwa kizimbani
THURSDAY, MAY 16, 2013
Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Dar es Salaam, imeamuru aliyekuwa mshtakiwa katika kesi ya Richmond, Naeem Gire, arejee kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, ili ajitetee dhidi ya mshtaka yanayomkabili.
Gire anakabiliwa na mashtaka ya kughushi nyaraka, kutoa na kuwasilisha taarifa za uwongo kuwa mitambo ya kufulia umeme ya ‘Richmond’, ina uwezo wa kufua megawati 100.
Inadaiwa kuwa taarifa hizo aliziwasilisha katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.
Julai 28 mwaka 2011, Gire aliachiwa huru na Hakimu Mkazi wa Waliarwande Lema wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, kwa maelezo kuwa hakuwa na kesi ya kujibu.
Ikiwa zaidi miaka miwili sasa tangu aachiwe huru, Mahakama Kuu imeamuru arejeshwe kizimbani na kujitetetea, baada ya kuridhika kuwa ana kesi ya kujibu.
Amri hiyo ilitolewa hivi karibuni na Jaji Lawrance Kaduri baada ya Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) kukata rufaa, akipinga uamuzi wa Mahakama ya Kisutu wa kumwachia huru mshtakiwa huyo.
Jaji Kaduri alisema ushahidi uliotolewa na mashahidi wa upande wa mashtaka unamtaka mshtakiwa kutoa utetezi wake .
Katika hukumu yake, Jaji Kaduri aliamuru kesi hiyo iendelee kusikilizwa kuanzia pale ilipoishia.
Alisema mshtakiwa anapaswa kujitetea mbele ya hakimu mwingine na si hakimu Lema.
Kesi hiyo, imepangwa kuendelea kusikilizwa Juni 6 mwaka huu mbele ya Hakimu mkazi, Emilius Mchauru.
Akimwachia huru Gire wakati huo, Hakimu Lema alisema baada ya kupitia ushahidi ameona kuwa hakuna ushahidi wa kutosha kuthibitisha kuwa mshtakiwa ana kesi ya kujibu.
Katika kesi hiyo, inadaiwa kuwa Machi 13 mwaka 2006, Gire akiwa na dhamira ya kutenda kosa, alighushi hati ya nguvu ya kisheria inayoonyesha kuwa imetolewa na Hamed Gile,
ambaye ni Mwenyekiti wa Kampuni ya Richmond LLC ya Texas, Marekani, kwamba amemruhusu kufanya shughuli za kampuni hiyo hapa nchini.
Haya mambo Sheria yana wigo mpana