Samson Ernest
JF-Expert Member
- Aug 28, 2014
- 1,118
- 1,565
Eze 15:7 SUV
[7] Nami nitaukaza uso wangu juu yao; nao watatoka motoni, lakini moto utawateketeza; nanyi mtajua ya kuwa mimi ndimi BWANA, nitakapoukaza uso wangu juu yao.
Watu wa Israeli walikabiliwa na ghadhabu ya Mungu kwa ukaidi wao, hapa inaonyesha wazi kuwa hata kama wangeepuka moto wa kwanza, wangekabiliwa na hukumu ya Mungu tu.
Lengo la hukumu hii kwa Waisraeli lilikuwa kutambulishwa ukuu wa Mungu ulivyo, wangemtambua Yeye ni nani katika maisha yao.
Vile ambavyo tumeona ujumbe wa kinabii kupitia kwa Ezekieli, akiwaeleza wazi watu wake kile kinawajia mbele yao, "watajua ya kuwa mimi ndimi BWANA". Ndivyo Paulo anaeleza wazi kuwa ghadhabu ya Mungu inafunua uadilifu wake.
Rum 1:18 SUV
[18] Kwa maana ghadhabu ya Mungu imedhihirishwa kutoka mbinguni juu ya uasi wote na uovu wa wanadamu waipingao kweli kwa uovu.
Tunajua hukumu au ghadhabu ni kitu cha kutisha na hakuna anayekubali kukutwa nacho, lakini hapa hukumu ya Mungu inakuwa ushuhuda wa utakatifu wake.
Tunapata somo kuwa Mungu si wa kubezwa, wale wanaobeza na kudharau neema ya Kristo wawe na uhakika watakabiliwa na moto wa kiroho.
Hukumu na wokovu ni utambulisho wa Mungu wa kumfanya mtu au watu watambue Mungu ni BWANA wa maisha yao, na ndiye muumba wa mbingu na nchi, na vyote vinavyoonekana na visivyoonekana.
Soma neno ukue kiroho
Liwe jua iwe mvua soma biblia na kutafakari
Mungu akubariki sana