Himidini
JF-Expert Member
- May 8, 2013
- 5,534
- 4,190
^^
Umekosea kuoa?
Hilo ni swali nilomuuliza rafiki yangu kipenzi sana. Alinifuata kwa maongezi ya kawaida. Maongezi yenye upendo,furaha, amani na urafiki. Wepesi wangu wa kumjua rafiki yangu ndio ulizua mengi. Hakuwa na furaha! Ni kana kwamba alijilazimisha kusema! Hata hivyo hakuwa msemaji sana bali, aliishia kutamka tu 'nimekosea kuoa!'
....
Ni vigumu kukataa ukweli uliondani ya usemi wa rafiki yangu. Maana ktk mahusiano hufika mahali kila mwanaume huwaza kuwa 'amekosea kuoa' na hata huthibitisha mawazo yake kupitia majirani ambao huwatathimini uhusiano wao kwa namna ya nje kuliko ndani zaidi. Na ni kweli pia yapo mahusiano yasiyobebeka hata uwe na kichwa chuma, yatakuyeyusha tu mpaka uyaache. Lakini yapo ambayo yanaweza kudhibitiwa yasife mbali kiasi cha kutengana.
...
Rafiki yangu anadai mkewe hashauriki, haambiliki, wakipanga hivi yeye hufanya vile, nyumba inaonekana ina wanaume tu na anadai mkewe hawezi kubadilika kamwe! Ni katika mwaka wa tatu na wana mtoto mmoja. Sasa anasema 'amekosea kuoa' anakumbuka X wake alivyomuasa kuhusu mpenzi wake, ambae sasa ni mkewe! Anasisitiza amekosea kuoa
...
Jawabu langu lilikuwa rahisi, 'Umekosea namna ya kufikiri'. Nadhani hili linawagusa wengi walio katika uchumba au ndoa, wanaodhani wamekosea kuwa na wenzi wao! Lakini ukidadisi vizuri wamekosea namna ya kufikiri. Mahusiano ya aina hii nayaona katika namna ifuatayo
I:
MAHUSIANO YANAHITAJI KIASI FULANI CHA HEKIMA
Unapokuwa na mwenza wa uchumba au ndoa, ni vema kukubali kuwa huna mtu mkamilifu. Anayo madhaifu ya kimwili, kiuamuzi au kiushawishi. Hekima ni namna gani unaondoa kwa uangalifu milango aliyoziba mwenzio katika kupata muafaka.
II:
HATA MPYA ANAYO YASIYOPENDEZA
Kumuacha uliyetoka nae mbali kwa tofauti za mawazo,mitazamo au tabia zinazoweza kujadiliwa na kumpata mpya, haina maana kuwa kule utapata asiye na kasoro. Jambo baya ni kusahau mambo mazuri makusudi kama heshima yake, mchango wake wa kukutunzia watoto, umakini wake katika kuhudumia familia, kukupa mavazi yanayokufanya usifiwe ofisini n.k Mahusiano ni zawadi inayohitaji kupakwa rangi.
..
UMEKOSEA KUFIKIRI
Asili ya maamuzi yote ni matunda ya kufikiri. Ukifikiri vibaya utavuna tunda la uchungu upweke au kujihukumu. Ukifikiri vema na kupembua mambo utapata tunda la kuchukuliana, kuvumiliana na kupalilia mti wa penzi upya.
Kagua namna yako ya kufikiri.