mzaramo
JF-Expert Member
- Sep 4, 2006
- 6,371
- 5,183
Mwanzo nilikuwa mbishi mbishi kukubali kuwa ni ujinga kuanzisha mahusiano na mwanamke ambae ameshazalishwa na mwanaume mwingine(single mother) labda pengine huyo mwanaume wake awe ametangulia mbele za haki otherwise utawekwa mitala hivi hivi unajiona.
Nisiwachoshe wakuu maana habari yenyewe ni ndefu kidogo twende kwenye mada moja kwa moja ila naandika nikiwa na uchungu mno.
Mwaka jana mwezi wa 10 nilikutana na huyu Binti ni msichana mrembo kweli.Mweupe,mrefu kidogo na ana chura ya kutosha kabisa inayofaa kwa matumizi ya binadamu.
Nikamtokea akanikubali ila kila siku alikuwa ananiambia kuna kitu inabidi tuongee ila akawa anasita sita kusema nini kinamsibu.Mpaka tunaanza kufanya matusi hakuwahi kuniambia hicho kitu chenyewe maana msichana mwenyewe ana aibu aibu mno.
Baada ya kama mwezi hivi ya mahusiano katika kupekua pekua simu yake nikakuta picha za mtoto katika kumuuliza akaanza kulia pale na kuniambia mimi bhana nina mtoto ana miezi 10 ila baba ake hayupo amesafiri kwenda Angola maana huyo jamaa anapiga deal za madini ila kabla ya jamaa kuondoka walikuwa wameshaachana yaani hawakuwa kwenye relationship tena zaidi ya kumcheki mtoto wao.
Akaomba sana msamaha kwa kunificha alifanya vile kwa sababu ananipenda sana na alikuwa anaogopa kuniambia ukweli kwa sababu wanaume wengi wanawaogopa wanawake wenye watoto na sasa yeye aliogopa nisije kumuacha kama akiniambia.
Mapenzi yashanikolea na ukicheki nishamtambulisha kwa washkaji zangu nikaona poa amna noma tukaenda mpaka kwao kumuona mtoto na mapenzi yakaendelea.Hiyo ilikuwa mwezi wa 11 mwaka jana nikawa baba wa yule mtoto zingatia pampers,maziwa na vikorokoro vyote kama mtoto wangu kabisa na mwezi wa 12 yule msichana na mtoto wake wakaamia kwangu kabisa nikawa nahishi nao.
Mimi sina mtoto na yule bibie hakuwa anatumia vidonge wala vijiti kuzuia mimba kisa hataki kutoka kitambi mie nikawa nakata viuno kweli kweli ili nimtie mimba tuwe ngoma draw na yule mzazi mwenzie tukajikuta mwezi wa 1 yule bibie hazioni siku zake.nikamchukua kwenda nae hospital kupima ikawa kweli ana mimba ya mwezi mmoja basi nikazidisha mapenzi kwa mama na mtoto usiku silali mara niletee maji baridi niletee chungwa hapo yule mtoto wake kishafikisha mwaka mmoja hapo.
Maisha yakaendelea mimba ilipofikisha miezi 4 ndio mabalaa yakaanza.Nilikuta sms kutoka kwa aunt yake anamwambia itakuaje sasa maana mzazi mwezio karudi na wewe ushatiwa mimba na huyo mpenzi mpya.
Katika kuzidi kupekua hiyo simu yake nikafuma meseji kibao za mchizi kuwa yeye hataki chochote zaidi ya kumtaka warudi nyumbani akalee mtoto wake la sivyo atafanya maamuzi magumu mno maana hataki damu yake ilelewe na mwanaume mwingine.
Kumuuliza yule bibie wewe ulisema uliachana nae kabla ajaondoka sasa mbona anakupiga mikwara ya urudi kwake?!akanijibu na yeye amuelewi nikamwambia mwambie ukweli upo na mtu mwingine na una mimba yake bibie anaogopa kumwambia mimi nikajipa jukumu nikamchana yule jamaa ukweli kupitia simu huyu ni mpenzi wangu na hapa mimba yangu ina miezi so kaa nae mbali muone kama sukari ya magendo jamaa kwa kujiamini anajibu hayo ya mimba sijui hayo sio yangu na hayanihusu ninachotaka ni kukaa na mwanangu na mama wa mwanangu full stop likanishuka pale.
Bahati mbaya au nzuri mimi ni mpiga madili tu hapa mjini nikapata deal la maana mikoani huko ikabidi niende mara moja nilitegemea nitakaa kwa wiki 4 hivi kwa hiyo nikaona huyu ana mimba na ana mtoo atapata tabu kukaa peke yake nikamwambia ww rudi kwa shangazi yako nikirudi nitakufata akasema poa.
Hiyo mwezi wa 4 na mimba ina miezi 4.Nimekaa kule mwezi mzima na tunawasiliana kama kawa anytime mpaka nimerudi amna tatizo lolote lile.
Balaa likaja nimerudi sasa nije kukufata kwa aunt yako turudi home ananikwepa mara sipo kwa Aunt npo kwa Uncle mara mama kasema kama unanitaka uje ulipe mahari mara baba mtoto wangu ananitishia kuniua nikiwa na wewe yaani sababu elfu lela ulela nikaona huu uboya nikafanya uchunguzi wangu nikagundua yule bibie anakaa na yule mzazi mwenzie tena mbaya zaidi na mimba yangu yenye miezi 5 maana kila siku naona anatupia picha tu WhatsApp na tumbo lake.
Hapa kichwa changu cha moto sijui hata nifanye nini na sijui hata nilikosea wapi.
Nikawaza Ana mtoto na yule jamaa lakini ana mimba yangu pia.Mawazo yenu wakuu nimeshindwa kabisa kuji upgraded natanguliza shukran