Mwalimu Makini
Member
- Dec 5, 2009
- 65
- 23
Huo ndio ufisadi wa kawaida wa CCM. Kama walikubali kujivua gamba inamaana wao ni yoka.
Hata kama Nyoka amejivua gamba, bado sumu yake ipo pale pale. Cha kufanya ni kuendelea kumtafuta huyu nyoka-CCM na tumponde kichwa chake kwa NYUNDO yao na kumkata kwa JEMBE lao !
chami ni nani?
Baada ya kusikika kelele kubwa dhidi ya serikali pale walipozuia magari ya Ndesamburo kupeleka wagonjwa kule Semunge kwa babu, mainzi wakali walijitoma kusaka chanzo cha timbwili hilo.
Ikumbukwe kuwa kule Bunda malori yalipitisha abiria wengi tu kupeleka Loliondo. Gari alilopeleka Ndesamburo ni gari linalotumika kusafirisha wazungu (watalii) kwenda mbugani. Gari hilo limelipiwa leseni ya kusafirisha abiria (PSV) na linatumiwa na kampuni ya utalii ya KEYS yenye makao yake mjini Moshi.
Habari za uhakika tulizozipata kutoka katika kikao cha siri kilichojumuisha mkuu wa mkoa wa Arusha, kaimu Mkuu wa mkoa Kilimanjaro, waziri wa Viwanda na Biashara Dr. Cyril Chami pamoja na watumishi wa serikali mkoa wa Kilimanjaro kilichokaa ofisini kwa RC Kilimanjaro kilipitisha uamuzi wa kuhakikisha kuwa Ndesamburo hapeleki tena wagonjwa Semunge kwani yeye anajiona Mungu wa Kilimanjaro.
Watumishi walitakiwa mmoja mmoja kutoa sababu za Ndesamburo kushinda uchaguzi mwaka 2005 na 2010. Kila mfanyakazi alijibu "SIJUI"
Baada ya Kalembo kuwalaani sana wafanyakazi hao kwa kushindwa kumdhibiti Ndesamburo ndipo Chami alitoa agizo kuwa serikali ifanye kila liwezekanalo kuhakikisha kuwa Ndesamburo hapeleki tena wagonjwa Loliondo kwani kwa kufanya hivyo wananchi wa majimbo yao wanawahoji kwa nini hawawapeleki Loliondo kama anavyofanya Ndesamburo? "Ndesamburo asitunyime usingizi" "sisi ndo tumnyime usingizi"
Viongozi wa Halmashauri ya Manispaa ya Moshi wameenda jijini Arusha kumwona RC kusikia kauli yake ili wajipange kuishambulia serikali baada ya kujiridhisha pasi shaka yoyote kuwa hatua ile ilichukuliwa kumhujumu Mbunge wao.
Nitaleta Updates zaidi
chami ni waziri wa viwanda na biashara, na pia ni mbunge wa moshi vijijini kama sikosei,im not sure, lakini ana jimbo mmoja mkoani kilimanjaro maeneo ya kibosho na kwingineko...sasa anamchukia sana ndesamburro, kutokana na suala kwamba ccm wamejiaribu kwa nguvu zao zote kumng'oa pale moshi mjini, na wameshindwa..
chami ni mbunge wa siha na si moshi vijijini