Hujafa hii dunia hujaumbika jaman

Hujafa hii dunia hujaumbika jaman

Joined
Jan 9, 2013
Posts
39
Reaction score
30
Wanajamvini msinishangae mie kila siku wa kuomba ushauri .

Nina rafiki yangu mmoja kweli anatia huruma, kaolewa mwaka wa tano hapati mtoto katembea sana mahospitalini ila nashukuru Mungu sasa kapata dokta mzuri anaendelea nae kimatibabu.

Binasfi hajawahi shika mimba tangu azaliwe na wala hajui inaingiaje ila ameambiwa ana ovary cyst na fibroid sasa anatakiwa kufanyiwa operation. Je inawezekana baada ya haya akapata mimba? maana dokta alimuweka kwenye dawa maalumu za zoladex zimtoa uvimbe ila bado upo ndo kaamua amtoe tu hayo mauvimbe .

Sasa najiuliza, je baada ya hapo chance yake ya kuzaa inakuwa kiasi gani? Anatamani mtoto mpaka namuonea huruma.

Msaidieni mawazo pia muombeeni jamani nadhani kila mwanamke anajua kukosa mtoto kunauma kiasi gani.
 
Ipelekwe JF Doctor, hapa panahitaji ushauri wa kitaalam zaidi.
 
Aende Sure Herbalist Clinic tatizo lake litapatiwa ufumbuzi. Maelezo zaidi aangalie channel 10 jumapili mchana..
 
tatizo wamezidi kutoa mimba na midawa ya izazi wa mpango bila kusahau kondomu hazina usalama kwa kuwa yale mafuta hubaki ndani ya nyeti zao
 
tatizo wamezidi kutoa mimba na midawa ya izazi wa mpango bila kusahau kondomu hazina usalama kwa kuwa yale mafuta hubaki ndani ya nyeti zao

Mkuu kwa mujibu wa mtoa mada huyo haijui mimba! by the way si kila anaeshindwa kupata ujauzito alitoa mimba,!! wapo waliotoa mimba na bado wana watoto!!
 
tatizo wamezidi kutoa mimba na midawa ya izazi wa mpango bila kusahau kondomu hazina usalama kwa kuwa yale mafuta hubaki ndani ya nyeti zao
Taratibu mkuu punguza jazba, ushauri kwanza mengine yatafuata.
 
aende foreplan clinic zipo dawa za kuyeyusha uvimbe bila kufanyiwa operation nina ushahidi
 
tatizo wamezidi kutoa mimba na midawa ya izazi wa mpango bila kusahau kondomu hazina usalama kwa kuwa yale mafuta hubaki ndani ya nyeti zao

nawe ushaambiwa hajawahi beba mimba tangu azaliwe,katoa lin ss?
 
mmmh jaman inaumiza sana mungu amjalie walau mtoto mmoja mweeeee kweli hujaumbika
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom