Kuna Watanzania ni laana kwa nchi hii. Wengine ni kutokana na ujinga na uwezo duni wa kuona mbali. Wengine ni mawakala wa maadui wa Taifa letu. Wengine ni sababu ya ubinafsi na tamaa.
Ulimwengu huu tangu uumbwe, vita vilivyopiganwa mara nyingi zaidi, ni vya kugombania maeneo/ardhi. Urusi inapigana na Ukraine kwa nia ya kuyachukua maeneo yote ya mashariki mwa Ukraine. Ukraine nayo inapambana kurudisha maeneo yaliyoporwa. Waisrael na wapalestina wanapigana kugombania maeneo. Kadhalika Spain na Morocco, Tanzania na Uganda, n.k.
Hivyo mtu yeyote mwenye kichwa kinachofanya kazi, anakuwa makini sana kwenye suala la wageni kuwapa rasilimali msingi ambazo siku moja zinaweza kumpa mgeni nafasi rahisi ya ushindi.
WAARABU
Mfalme wa Oman, miaka ya karibuni ametamka kwa uwazi kuwa lazima siku moja makao makuu ya sultani wa Oman yarudi Zanzibar.
Makamu wa kwanza wa Rais wa Zanzibar amewahi kutamka kuwa maeneo yote ya pwani ya bahari kutoka pwani ya bahari kuingia bara kilometa 20, ukanda wote toka Pangani mpaka Mtwara, ni maeneo ya Zanzibar kwa sababu maeneo hayo yalikuwa chini ya utawala wa sultani.
IGA inasema DP wanatakiwa kumilikishwa ardhi ya maeneo yote watakayowekeza. IGA ni mkataba mama, na haujabadilishwa hata nukta moja hata leo. IGA, kila mmoja mwenye uelewa aliiona, lakini HGA iliyosainiwa hakuna aliyeiona, na wanayoyanena hawa watu wasioaminika, hakuna mwenye uhakika kama yapo kwenye mkataba huo wa bandari ya Dar au ni mwendelezo ule ule wa uwongo na ulaghai wa watawala. Lakini hata kama maneno wanayoyasema ni kweli, bila mabadiliko ya IGA, siku yoyote DP wanaweza kuibuka na kudai kilichopo kwenye IGA.
LENGO LA MUDA MREFU
DP watachukua maeneo ya bandari, na maeneo mengine ya pwani ya bahari watayanunua toka kwa wananchi, ambao wengi wao ni maskini, na hawatakuwa na uwezo wa kukataa donge nono la mnunuzi mwarabu. Baada ya miaka mingi mbeleni, pwani yote ya bahari, toka Pangani mpaka Mtwara, itakaliwa na kumilikiwa na waarabu. Na kutokana na nguvu ya pesa, watajiunga CCM, (na kwa CCM ukiwa na pesa utapewa cheo chochote utakachotaka) na hivyo kuwafanya wageni hawa wawe na nguvu za kisiasa na uchumi.
Yumkini, huko mbeleni pwani yote ya bahari ya hindi itachukuliwa na waarabu, na kisha kuifanya ni sehemu ya Zanzibar. Hilo likitokea, Tanganyika itakuwa landlocked, ikibakiwa na vibandari vya kwenye maziwa, na hivyo kuzitegemea bandari za mataifa mengine. Ukamilifu wa haya unaweza usitokee miaka ya karibuni, lakini ni mpango wa muda mrefu. Baada ya migogoro mingi, Zanzibar itajitenga, na kuridhia kuwa sehemu ya Oman, na hapo ndipo makao makuu ya sultani yatahamia mji mkongwe.
Umeandika fikirisho tosha kabisa, kuna watakao kebei kwakuwa yawezekana wao watakuwa wakisha kufa, na kuna ambao pesa za wakati huo zitakuwa tamu na kusukuma siku za kuishi, hawa ndio hao wasiojali nchi yao bali ccm itawale, hao ndio wale wafia madarakani, hao ndio wale wanaojioma nchi hii ni yao peke yao na familia zao, hao ndio wale wajiitao machawa ili mradj wakati wote wako karibu na viomgozi
Hii ndio Tanzania ya kinafiki wenye busara ni wachache na wengine walikwisha tangulia mbele za haki
Watanzania wanaojitolea kuipigania nchi hii wanafanywa. Maadui wa taifa, masikini wasiojielewa na wao wanaingia kwenye mkumbo wasio uelewa
Kuna neno ni baya lakini ni jema, unaweza kuwa na mzazi saababu ni baba yako ukadhan ni mtu wa busara sababu kakuzaa wewe
Lakini akawa mi mtu wa ovyo dhidi ya matendo yako yasiyo na busara
Kumbe nk mbakaji, kumbe ni jambazi, kumbe ni muuaji
Lakini kwako ni baba bora
Ccm. Si kila kitu katika maisha yetu
Ccm ni kama vyama vingine tu na sio sababu imeleta uhuru basi ni chama chema
Ni chama kilichokwisha poteza wisdom yake ni chama kilichokwisha vunja misingi yake
Ni chama kilichobakiza rangi tu pamoja na picha ya nyundo na jembe
Yani ni chama kilichopitwa na wakati , wao bado anawaza jembe mlaka sasa wakati hivi sasa kuna teknoloji mpya za maendeleo
Sio kila kitu mfundishwe
Nina mengi ila cha muhimu wcha nirudi kwenye point
Parestna inasemekana ilichukuliwa kwa mfano wa andiko hili, mamaanisha post hii tunayoichangia
Wakati wa Israel
wanarudi walirudi kwa kununua maeneo yao makubwa ikiwa ni mkakati wa kurudi katika ardhi yao
Ma mpaka kufikia kujikusnya na kuwa na nguvu na kurudisha taifa lao
Hawa ni waraabu hawashindwi kufikia maamuzi kama ya ndugu zao
Tuunganeni kuikomboa nchi yetu sote
Tuwe Islamic, au Kristian au Pagani
Hii nchi ni ya vizazk vijavyo tuache ubinafsi
Samahanini kwa error zozote zilizojitokeza, nina matatizo kidogo ya macho