Nadhani wote mpo sahihi ila ingekuwa vyema mtoa huduma kwa wateja angekuuliza vitu ambavyo anaona ni vya muhimu ulivyo tumia kuisajili sim yako.mfano jina lako,tarehe ya kuzaliwa,aina ya kitambulisho ulichotumia kujisajili na mwisho namba ya kitambulisho, baada ya hapo angegundua kuwa wewe ni mmiliki wa hiyo sim au laa.kwa upande mwingine usimlaumu kwani watu wengine wanatumia mwanya wa kuonge na wahudumu wa huduma kwa wateja kublock sim za watu wengine pasipokuwa na sababu.kuhusu kulipia sh.100 kwa dakika ni sawa kwani watafidia wapi sh.i kwa dakika siku nzima?ukumbuke kuwa si kila kitu ukisikiavyo ndivyo kilivyo vingine kuna vitu vingine vimejificha ambavyo havisikiki na vimo ndani yake.