Kwa maoni yangu Dar sio safe kama ilivyo Nairobi na hata J'burg. Tofauti ni kuwa habari nyingi zinazotekea Dar haziripotiwi, tofauti na hizi sehemu nyingine. Kingine pia na taaluma wanayoitumia wahalifu wa Dar iko chini kulinganisha na hii miji mingine. Kibaya zaidi Dar kupata msaada wa polisi ni taabu, wakati J'burg msaada wa polisi upo karibu. Ila mara nyingi wakisha kuwahi kule wanapotea kama upepo, wakati hapa Dar wahalifu wanaweza kuamua kufunga mtaa na kuanza kupora duka moja hadi jingine mpaka watakaporidhika.
Dar sio safe, ukiamua kuja jitahidi ujiweke kawaida kwa kadri utakavyoweza ili usiwashawishi kuwa wanaweza kuvuna kwako.