Hotuba ya zitto kabwe leo kibaha

Hotuba ya zitto kabwe leo kibaha

kabanja

Senior Member
Joined
Apr 5, 2015
Posts
173
Reaction score
41
Zitto Kabwe
Kibaha 28.06.2015
Leo ACT Wazalendo inatimiza mwezi wa tatu tangu mkutano
mkuu wa kuchagua viongozi wake wa kitaifa ambapo baadhi
yetu tumechaguliwa kuongoza chama chetu. Katika kipindi
hicho tumeweza kutambulisha chama chetu katika makao
makuu ya mikoa 22 ya Tanzania bara. Mikoa ya Arusha na
Kilimanjaro tumefikia wilaya zake na mkoa wa Dar Es Salaam
tutaingia tarehe 4 Julai 2015. Baadaye tutakwenda kufanya
mikutano katika miji ya Arusha na Moshi. Mikutano yetu
imekuwa na mafanikio makubwa sana. Tunamshukuru mungu.
Leo tupo kibaha katika mkoa wa Pwani. Leo pia Mwenyekiti
wetu yupo Karatu katika mkoa wa Arusha. Katika awamu hii
ya ziara tumekuwa pia tukifafanua kuhusu Azimio la Tabora
linalohuisha Azimio la Arusha. Katika Azimio la Tabora
tumeamua kufanya kampeni kurejesha Miiko ya Viongozi. Sisi
tunaamini kuwa Miiko ya Viongozi ambayo inadhibiti viongozi
wa umma kujilimbikizia Mali ndio mwarobaini dhidi ya ufisadi
nchini mwetu.
Nilipokuwa Nachingwea juzi nilitoa mfano wa wanasiasa 4 wa
chama cha CCM ambao niliwataka kutoa ufafanuzi kuhusu
masuala yanayozungumzwa dhidi yao. Hii ilikuwa katika
kuonyesha umuhimu wa Miiko katika aina Mpya ya siasa
tunazotaka kuanzisha katika nchi yetu. Bado narudia kutoa
wito kwa wagombea wote wa Urais kutoka vyama vyote
kuacha porojo za kupambana na ufisadi na badala yake
waseme namna watakavyopambana. Sisi tunaamini kuwa njia
pekee ya uhakika ya kupambana na ufisadi ni kurejesha Miiko
ya Viongozi.
Nataka kuwahakikishia wataanzania kuwa chama chetu
kitaweka mgombea Urais mwaka huu na tutashinda. Mimi
siamini hata kidogo kuwa mabadiliko yataletwa kupitia CCM
na ndio maana siku zote nimekuwa nikiwasihi wanasiasa
wenzangu vijana wanaotaka kuongoza nchi yetu kama
January Makamba na Mwigulu Nchemba waondoke CCM waje
kwenye chama hiki ili kujenga Tanzania Mpya yenye misingi
imara.
Chama chetu kinataka kujenga siasa Mpya zenye lengo la
kurejesha nchi kwenye misingi. Kwa namna ambavyo ufisadi
umetamalaki nchini kwetu, kurejesha Miiko ya viongozi
hakuepukiki. Ninaamini wanasiasa vijana wana uwezo huo
kwani bado hawajaingia kwenye tabia hii mbaya ya
kujilimbikizia Mali.
Tunawataka Watanzania kuwashinikiza wanasiasa kutangaza
Mali na Madeni yao ikiwemo maslahi mbalimbali kabla ya
kushika nyadhifa za uongozi wa umma. Ninawataka vijana wa
Tanzania kuungana nasi katika kufanya mabadiliko makubwa
kwenye nchi yetu ili kujenga uchumi unaozalisha ajira na
kuondoa umasikini, kuboresha huduma za jamii kama Maji,
Afya na Elimu, kupambana na ufisadi na kuziba nyufa za udini
na ukabila kwa kurejesha ujamaa.
Wananchi wa Kibaha, mkoa wenu wa Pwani ni moja ya mikoa
masikini kabisa nchini mwetu. Ni mkoa ambao hata juhudi za
awali za kujenga viwanda ili kuukomboa zimezimwa kwa
kubinafsisha viwanda vilivyokuwa hapa Kibaha. ACT
Wazalendo inataka kushirikiana nanyi kujenga heshima ya
mkoa wa Pwani. Tutarejesha viwanda ili kutoa ajira kwa
vijana wetu. Pwani yaweza kutumika kupunguza msongamano
jijini Dar Es salaam kwa kujenga container depots kibaha na
chalinze na hivyo kuongeza ajira kwa vijana wetu.
Wananchi wa mkoa wa Pwani tumekuja kutambulisha chama
chetu kwenu. Tunaomba mtuunge Mkono. Nawashukuru sana
Zitto Kabwe
Kiongozi wa Chama cha ACT Wazalendo
 
Back
Top Bottom