Hotuba ya rais Kikwete mwisho wa mwezi Machi


Hata ufahamishwe vipi hutaelewa kwani usha "set mind" yako kuwa "biased". Kila atachosema au fanya Kikwete hata kiwe chema kipi, hutokiona. Umefunga.
 
Ah, huyu bwana huwa ana maneno na hotuba ndefu wakati utekelezaji nil, hana jipya!
 
Yaani rais anataka kutufanya watu wazima na akili zetu ni majuha ati anawapongeza TRA .... ..... ... hawa wezi wenzake ndio anawapongeza? Mbona anawakataza kuwashughulikia akina Sin Bin Clair kwenye Madini kila mwaka ati wanakula hasara, Mwizi mwenzake na swaiba wake mkuu RA pamoja na EL mbona makampuni yao hayaguswi na TRA? JK time is up soon rather than later cha mtema kuni kilichomtoa kanga manyoya utakiona. Hatuwezi kuwa na kina Chenge na rafiki zao ambao ni wakwepaji wakubwa wa kodi then mnakuja kusema tufunge mkanda hali ni mbaya, hii hali ni mbaya kwa wenzenu tu? Then unasema ati tutapata misaada! Nani anataka misaada ya kutudumaza, hatutaki misaada, Tanzania sio ya tima kutegemea misaada kutoa nchi za nje. Watoa misaada wote ni wezi na wanaendelea kutuibia kwa sababu tuna viongozi ambao wanawadharau wazawa na kuwakumbatia wezi wa urithi tulioachiwa.

Swala la umeme wewe kama rais na madaraka uliyopewa kwa nini kila mwaka unakubali TANESCO wakodishe umeme wakati nchi ina uwezo wa kununua majenerator yake? Hivi uliposoma Economics pale mlimani ulifaulu kweli au ulipendelewa? Unapanga mpango ati mwezi wa saba. Mbona magenerator yapo tu tena bei poa kwa nini tuendelee na kampuni za RA kwa ushirika na EL na JK wakati uwezo tunao. Mkuu naona u-rais umekushinda. Fedha za dhuluma kwa walipa kodi hazitapotea bure!
 
Hata ufahamishwe vipi hutaelewa kwani usha "set mind" yako kuwa "biased". Kila atachosema au fanya Kikwete hata kiwe chema kipi, hutokiona. Umefunga.

Hapana mkuu, katika hilo kundi simoio kabisa. Mine is a very professional advice without any malice whatsoever to my president. Kuna vitu viwili 1. Utaratibu wetu wa ndani ya nchi kuomba kukubaliwa kuwa urithi wa dunia 2. Sheria za UNESCO zinavyo tufunga baada ya kukubali ombi letu. One does not need a college degree to know that the problem starts at home. Je waziri ana mamlaka ya kutuma hayo maombi? Wanachi wanashirikishwaje? Je inatangazwa katika gvt gazette kabla ya maombi rasmi kutumwa? Is there an opportunity for an aggreaved party to appeal? Tayari tuna status ya UNESCO kwa Mji mkongwe, Serengeti, Ngorongoro, Rock paintings za Kondoa na Mlima Kilimanjaro. Je michakato ya hii iliendaje? Ku withdraw hili ombi moja kuta saidia nini au kuathiri vipi management ya hizo cite nyingine? AAnze na wizara kuwachorea ubaoni neno USHIRIKISHWAJI. Hawalijui kabisa. This is the most undemocratic ministry in the country!

AGAIN I have no any malice. Ni ushauri wa kweli kabisa and being true to my country mkuu!
 

Hapo penye rangi ndipo panapotutenganisha mimi na wewe. Na ndiyo maana nasema Rais na Serikali yake wanajua kilichofanyika na ndiyo akawa mwepesi kusema kwa "taratibu zilizopo", Sasa hapo mimi na wewe ambao hatujui tungetafuta kujua kwanza taratibu zinasemaje? au hiyo michakato mingine iliendaje ndipo tuweze kum criticize Rais. Kwa mfano nikuulize wewe, je unajua taratibu au sheria hiyo inasemaje ambayo ndiyo reference ya kulaumu? Status yetu na UNESCO ina boundaries gani au zipi? Je kila ombi ni lazima likubaliwe tu kwa sababu tulikubali mengine huko nyuma? otherwise una point nzuri ila unaonekana unakurupuka kutaka tu kumlaumu Rais.
 

Mkuu mimi naujua utaratibu mzima, trust me. Base yangu ya ku criticize haipo kwenye boundaries zetu na UNESCO au kukubaliwa/kukataliwa far from that. My concern is the impact of correcting a mistake by another (even bigger) mistake. Wizara haikufuata utaratibu kuomba UNESCO status...rais naye hafuati utaratibu anatoa amri ya kuwithdraw maombi yaliyokwisha tumwa. Honesty this is too low. Au ni wewe umemshauri nini mkuu maana hapo kwenye kijani umeonyesha mkanganyo wa hali ya juu. Sasa kama hata kukubaliwa hakuna guarantee why take trouble to send such an unfriendly gesture to a UN agency? What are the long term repurcusions?

Nawasilisha, mkuu!
 
Mwezi wa tatu ulikuwa mwezi wa ziara.
Mkuu karibia sehemu zote yeye anafarijika na kufurahi tu. Dah!
 


Haeliti matuini hata kidogo kwa mtanzania wa Kijijini.
 
Kama watanzani tunaoulazima wa kuisikiliza hotuba yake tena kwa umakini sana ili pale ambapo panahitaji kukoselewa pakoselewe,sasa kama wakati hotuba inaendelea na watanzania wanaangalia habari za babu wa Loliondo na kwengineko na tamthilia je atakosoa? na je wenye ufahamu mdogo nani atawaelimisha juu ya mapungufu haya ya hotuba za Rais wetu? Tuwe wazelendo wa kweli na nchi yetu na kumbukeni hakuna wakuja kuijenga Tanzania yetu isipokuwa sisi wenyewe.Enyi watanzani wenzangu kumbukeni kuwa kujenga ni kuumia.
 
Sidhani kama kuna mtanzania anajali haya maneno ya kikwete. Kazi ulipewa 2005, mpaka leo hujui unatakiwa ufanye nini. Alikushauri kufanya hizi hotuba za mwezi kwa mwezi amekudanganya, wananchi wanataka update ya ulichokifanya kwa manufaa yao sio uongo.
 

Nafikiri unafanya makosa kuzungumzia umuhimu wa kusikilia hotuba za Jk. Wewe umesikiliza hotuba ngapi mpaka sasa hivi? Bado unataka kusikiliza hotuba badala ya wewe kama mwananchi kupewa updates za Jk na serikali yake walichokifanya tangu 2005. Nani ambae atakikusikia tatizo la umeme linatatuliwa vipi, maji, elimu, uchumi, afya? Maybe wewe ni kada tu au hujui ulazimu wa ofisi ya raisi kuwa na ukweli na kuacha kuwadanganya watanzania. Maswala ya kurekebisha yapo kila kona na mengi huyo huyo Jk kayaleta TZ. Huwezi kuwafanya hotuba kutaka kuwabadilisha watanzania kwa uongo. The facts will always remain the truth - umaskini umeletwa na ccm

Legacy ya kikwete anaijenga yeye mwenyewe sio Dr Slaa
 
Wewe kweli hujui unachoongea bana. kwenye speech hii unataka upewe updates gani zaidi ya ulizoziona? Kuwa specific na siyo ku generalize vitu. Mpeni Rais pumzi afanye majukumu yake. Kila kitu kwenu kibaya tu. Hamna jema ninyi viumbe?
 
Anasisitiza kulipa kodi wakati wao ndio kwanza wana exemptions almost katika kila kodi!
 
JK: kwa jumla ziara zangu zilikuwa nzuri na malengo niliyojiwekea yametimia. Nimefarijika sana kuona na kusikia mafanikio makubwa yaliyopatikana katika utekelezaji wa majukumu ya Wizara, Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya 2005 – 2010 na maagizo niliyoyatoa miaka mitano iliyopita. Aidha, nimeridhishwa na jinsi Wizara na Taasisi zao zilivyojipanga kutekeleza majukumu yao na Ilani ya Uchaguzi ya 2010 – 2015.

Mimi: Wanaotakiwa kuona mafanikio sio watendaji ni watendewa, iweje mwanafunzi ajisahihishie mtihani?

​JK: Juhudi za kuongeza mapato ya Serikali zitakuwa na maana iwapo kutakuwa na matumizi mazuri ya fedha za Serikali. *Jambo hili nimekuwa nalisisitiza mara kwa mara na nililirudia tena nilipozungumza na viongozi na wafanyakazi wa Wizara ya Fedha na Wizara ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

Mimi: mbona mashangingi bado yapo, tena latest V8?

JK: Vile vile, nimewakumbusha umuhimu wa kuhakikisha kwamba watumishi wapya wanaoajiriwa wanalipwa mishahara na stahili zao mara wanapowasili katika vituo vyao na kuanza kazi. Watumishi kukaa miezi kadhaa bila ya kulipwa mishahara na stahili nyingine ni jambo linalosikitisha, halikubaliki na kwamba wakati umefika lisiendelee kutokea.

Mimi: Samahani mzee, wale wazee wetu wa East African Communication..... sorry Community unawakumbuka? si ungemalizana nao kwanza au unaonaje.

JK: Kwa upande wa Wizara ya Uchukuzi, nimerudia maelekezo yangu ya kawahimiza kuharakisha mchakato wa Shirika letu la reli kuachana na RITES na mchakato wa kuboresha reli ya Kati na TAZARA. Nimefurahi kusikia kwamba mchakato wa kununua meli mpya katika Maziwa ya Victoria, Tanganyika na Nyasa upo katika hatua mbalimbali za utekelezaji. Niliarifiwa kuwa tayari wataalam washauri kutoka Denmark wamekwishaanza kufanya upembuzi yakinifu juu ya aina ya meli itakayofaa katika Ziwa Victoria. Nimewaagiza, waharakishe kukamilisha mchakato huo ili waendelee na zoezi kama hilo katika Maziwa Nyasa na Tanganyika na hatimaye ununuzi wa Meli ufanyike.

Mimi: Mmhh, Ok.... Ndio Mzee.

JK: Kama nilivyokwishaeleza, hivi sasa TANESCO wanaendelea na mchakato wa ukodishaji wa mitambo ya dharura ya kufua umeme wa megawati 260. Tayari zabuni imekwishatangazwa ili kumpata mkandarasi atakayekidhi viwango na mwenye gharama nafuu. TANESCO wameahidi kuwa ifikapo mwezi Julai uzalishaji wa umeme huo wa dharura utakuwa umeanza. Nimewaagiza TANESCO na Wizara ya Nishati na Madini kuhakikisha kuwa mpango huo unatekelezwa kama ilivyopangwa. Aidha, nimewataka waongeze kasi ya kutekeleza mipango mingine ya kulipatia taifa umeme wa uhakika na endelevu katika kipindi kifupi kijacho.


Mimi: Sorry mzee, I dont mean to annoy you, lakini ni kama nakumbuka zamani ulisemaga kuwa mgao wa umeme utakuwa historia, kwani what happened? Sorry lakini!!:rockon:
 
Neno dowans hapendi hata kulisikia au kuliongelea, hivi tz utaongelea tatizo la umeme kwa kwa sasa bila kugusa dowans!

Mengine ya mvua na kadhalika ni kumsumbua mungu, kama mikataba ya tanesco, ingekuwa inasainiwa kwa maslahi ya watanzania tungekuwa tunakuwa na umeme through out the year!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…