Hotuba ya rais Kikwete mwisho wa mwezi Machi

hivi rais mzima unaweza ukahiza wananchi kuchukua risiti?kamisha tra anafanya nini?afisa biashara kazi yao nini siku hizi?hajui kuwa uzembe,ukiritimba wa TRA ndio unawakatisha tamaa wananchi kulipa kodi wafanyakazi wa tra wana majibu ya mkato hovyo sana

Hiyo inaonesha ni vipi Rais anajali na anatazama kila "detail".
 
risiti zenyewe kwa bidha za china na kenya india kidogo!mkoa wa shinyanga pekee una ngombe wengi kuliko nchi ya botswana lakini botwana wanatuzidi kipato katika export ya bidhaa za ngozi pembe!kama rais wa nchi hayo ndio maswali ya kuwaelekeza wananchi wafanye nini kujikwamua kiuchumi!sasa mwananchi atakula risiti?
 
oya toeni mawazo kasema nini cha maana siyo mnaponda tu haiwezekani awe amezungumza hewa kwa dakika zote zile mkome na mkomaeeeee
 
Wakubwa hishima kwenu.
Style ya humu ndani inaonekana ukimponda Rais ndiyo unaonekana wa maana siyo?
 
Majimshindo changia hoja mkuu! Sio kujibu na kukosoa wenzio.
Acha ushabiki wewe! Mbona wewe hujatoa hoja hapa? Acha kuwa referee! Hao waliandika mara kapauka, mara hakuwa na confidence,, wewe umeona hoja hizo??
 
kaongea nini cha maana? maana ndo nimetoka bafuni kuoga naona wanapiga wimbo wa TAIFA tbc
Mkuu,
Mwanzo uliandika hutaki kusikiliza upupu, sasa mbona unauulizia tena? Upupu unautaka sasa? Ulisema bora ukacheze kamali, au umesahau?, Au umeshaliwa kekundu huko?? Wewe vipi ndugu? Akili yako iko sawasawa kweli? Stop contradicting yourself and confuse people in here.
 
oya toeni mawazo kasema nini cha maana siyo mnaponda tu haiwezekani awe amezungumza hewa kwa dakika zote zile mkome na mkomaeeeee
Very simple logic, I concur with you Sir! Mtu hawezi akaongea muda wooote huo eti vapour tupu? Basi kama ndivyo, most of us in here we are either dumb or pretending.
 
Hapo chini substance ni ndogo sana, less than 18%. Ukiondoa ukweli kwamba ni too repetitive na essentially haina ulazima kwani zaira za wizara zote zilikuwa covered na media, the whole thing has nothing new. This is not what a president would say about the "backbone" of the economy baada ya robo ya kwanza ya mwaka. No review, no strategies, no way foward nothing! Hali ni mbaya

Kilimo, Mifugo na Uvuvi

Ndugu Wananchi;
Nilipotembelea Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika na Wizara ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, nimepata faraja kuwa utekelezaji wa malengo yetu ya kuleta mageuzi ya kilimo, ufugaji na uvuvi yanakwenda vizuri. Nimefurahi kuona kwamba muelekeo wa miaka mitano ijayo ni mzuri. Nimeelezwa changamoto mbalimbali zinazozikabili sekta zetu hizi na nimefurahishwa na mikakati ya Wizara zetu mbili ya kukabiliana nazo. Nilifarijika sana kusikia kuwa mipango kabambe ya kuendeleza ufugaji na uvuvi imekamilika. Mimi nimewaahidi kuwasemea kwa wanaotoa mgao wa fedha ili wawezeshwe kutekeleza malengo yao.

Ndugu Wananchi;
Hizi ni sekta muhimu sana, hivyo kuendelezwa kwake kunawanufaisha Watanzania wengi. Ukizungumzia kupunguza na hatimaye kuondoa umaskini nchini huwezi kufanikiwa bila kuendeleza sekta za kilimo, ufugaji na uvuvi ambazo asilimia 80 ya Watanzania huzitegemea.

Nilipozitembelea Wizara hizo nilisisitiza mambo manne ambayo ningependa muyafahamu. Jambo la kwanza linahusu kuutazama upya mfumo wa vocha za pembejeo ili kuleta ufanisi zaidi. Serikali imeanzisha mpango wa kutoa ruzuku kwa pembejeo za kilimo kama vile mbegu, mbolea na dawa. Mpango huu una nia ya kuwaongezea wakulima uwezo wa kupata mavuno zaidi ili waongeze kipato chao na kuinua hali zao za maisha. Tulianzisha mfumo wa vocha ili kuhakikisha kuwa ruzuku hiyo inawafikia wahusika. Kuanzia miaka miwili iliyopita kumejitokeza vitendo viovu vinavyofanywa na wajanja wachache ambavyo ni kinyume na matazamio ya Serikali. Nilishaagiza vyombo vya dola kuwasaka wahusika na kuwafikisha mbele ya sheria. Kazi hiyo inaendelea ingawaje naomba kasi na nguvu iongezeke.

Pamoja na kufanya hayo, nimeagiza tuuangalie upya mfumo wetu wa ugawaji wa pembejeo za ruzuku. Kama kuna upungufu wowote tuurekebishe, tuzibe mianya inayotumiwa na wahalifu ili ufanisi zaidi upatikane. Nimefurahishwa na taarifa kuwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali ameanza kuufanyia ukaguzi mfumo wa ugawaji pembejeo ili atoe mapendekezo ya namna ya kuuboresha. Vile vile, nimefurahishwa na uamuzi wa Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika wa kupeleka watu Malawi ili wakajifunze kutokana na uzoefu wa wenzetu.

Jambo la pili, linahusu kuanzisha mfumo wa masoko ya mazao ili wakulima wawe na masoko ya uhakika na yanayotoa bei nzuri. *Ni jambo ambalo nimekuwa nalihimiza tangu niingie madarakani. Nilifurahi sana nilipoambiwa kuwa hivi sasa mchakato wa kuanzisha “Soko la Mazao ya Kilimo” yaani Commodity Exchange Market uko mbioni kuanza. Narudia kuwapongeza sana na kuwatakia mafanikio mema na ninawaahidi msaada wangu pale itakapostahili.

Jambo la tatu, ni kwamba nimezielekeza Wizara zinazohusika na kilimo na mifugo kushirikiana na TAMISEMI kuanza kupeleka wahitimu wa vyuo vikuu katika ngazi ya tarafa na kata ili wasaidie kuinua ubora wa kilimo na ufugaji miongoni mwa wananchi. Na, jambo la nne ninalopenda kulisemea, ni kutoa pongezi kwa Idara ya Uvuvi kwa kazi kubwa waifanyayo ya kupambana na uvuvi usiokuwa endelevu pamoja na uvuvi haramu. Narudia kuwahakikishia utayari wangu na wa Serikali kuwasaidia kuwajengea uwezo wa kutimiza wajibu wao ipasavyo.
 
Kweli ombwe... Vibwagizo vilevile ... anaomba, anakumbusha, halafu anaishia kwa kupongeza. Halafu ktk hizo ziara feki mbona hakutembelea mwinyi (wizara ya ulinzi)?
 
Hapa sawa japo tunataka kuona haki za binadamu zinazingatiwa 1987 na sasa tofauti kabisa mheshimiwa rais. Na pia sababu za kushindwa kwa idara ya wanyamapori haziko wazi, je hawana pesa? wako demotivated? Halafu kuwa na waziri mmoja tu asiye hata na naibu katika wizara nyeti kama hii kunatoa picha gani mheshimiwa? Au huyu ni "Yes men" wako? Please do first things first

Matukio ya Ujangili katika Hifadhi

Ndugu Wananchi;
Nilipotembelea Wizara ya Maliasili na Utalii, pamoja na mambo mengine, tulizungumzia tatizo la kuongezeka kwa vitendo vya ujangili katika mbuga za wanyama zinazoangaliwa na Serikali au mashirika yake. *Kuna kila dalili kwamba mamlaka za hifadhi zetu zinaelekea kuelemewa na majangili. Nimewaagiza waongeze juhudi na nimewaambia kuwa niko tayari kuagiza Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania kusaidia kupambana na majangili. *Nchi yetu inayo historia ya kufanya hivyo mwaka 1989 kwa mafanikio. *Niko tayari kufanya hivyo tena.
 
Bellow is the most unfortunate part of the speech mheshimiwa. We are a part of the international community. We can not act so arbitrarily when it comes to collective issues for the good of the future generation. What image will this have on Tanzania's commitment to conservation? What does the law says about applying for world heritage cite?

Jambo lingine ambalo nililizungumzia ni mchakato wa Wizara wa kutaka kuitangaza misitu ya milima ya Tao la Mashariki yaani milima ya Pare, Usambaa, Uluguru, Nguu hadi misitu ya Udzungwa kuwa urithi wa dunia (World Heritage Site). *Lengo linaweza kuwa zuri kwamba nchi yetu inaweza kupata misaada ya kuhifadhi misitu hiyo. *Lakini, uamuzi huo una maana kubwa kwa watu wa maeneo hayo, mamlaka za Serikali za Mitaa na hata nchi kwa jumla. *Kwa mujibu wa utaratibu uliopo, watu au hata mamlaka ya nchi haitaweza kuamua kufanya jambo lolote katika maeneo hayo bila ya kupata kibali cha UNESCO.
 
Mkuu analysis yako inaweza kuwa nzuri, lakini ukaingalia andiko lako penye wekundu na lile la Rais penye Blue, ni wazi kwamba wewe ndiye usiyejua sheria au kanuni zinasemaje kuhusu suala hilo. Rais yeye anaonekana anajua ndiyo maana amesema kwa mujibu wa taratibu( sheria na kanuni) zilizopo. Cha kufanya wewe ungejitahidi uzijue pia taratibu, sheria na kanuni hizo ndipo u challenge hii. Otherwise, Rais amesema vyema.
 
Mkuu inaonekana tunazungumzia vitu viwili tofauti. Mh rais hapo reference yake ni "utaratibu uliopo" BAADA YA KUJIUNGA akimaanisha sheria za UNESCO zinavyo zifunga nchi wanachama. Hapo yuko sahihi kwa sehemu. Swali langu je sheria zetu zinasemaje kwa taratibu ZA KUJIUNGA? Hapo ndipo tatizo lilipo na tulipaswa kurekebisha our own approach na siyo kupeleka aibu UNESCO wakati hata jeraha la CITES kutuzuia KWA AIBU kuuza meno ya tembo kule Qatar halijapona.
 
Kweli ombwe... Vibwagizo vilevile ... anaomba, anakumbusha, halafu anaishia kwa kupongeza. Halafu ktk hizo ziara feki mbona hakutembelea mwinyi (wizara ya ulinzi)?

Alikwambia kamaliza ziara zake?
 
risiti zenyewe kwa bidha za china na kenya india kidogo!mkoa wa shinyanga pekee una ngombe wengi kuliko nchi ya botswana lakini botwana wanatuzidi kipato katika export ya bidhaa za ngozi pembe!kama rais wa nchi hayo ndio maswali ya kuwaelekeza wananchi wafanye nini kujikwamua kiuchumi!sasa mwananchi atakula risiti?

Wewe alikukataza nani kuanza ku-export hizo ngozi? au unataka ufanyiwe kila kitu?

Tanzania biashara ziko wazi, asieweza kuzifanya au asiyejuwa pa kuanzia, aulize, hata hapa JF wengi huja na kuuliza, jamani nna million 8 au mwingine 60 au 100 nifanye biashara ipi, hupewa mawazo. Sasa wewe kama unataka kuuza ngozi, ni nani aliyekuzuia? kama hujui pa kuanzia uliza wenzio wanao export ngozi, walianzaje na jee kwa nini hawa export zoooote.

Nashangaa sana mTanzania anapiga kelele kutaka rais amuelekeze namna ya kufanya biashara, Rais anakwambia ukifanya biashara, pata risiti.
 
Back
Top Bottom