Technology
JF-Expert Member
- Oct 19, 2010
- 769
- 284
5. Mr. President, Could you please include very carefully and seriously the curent electricity status in the country... all those below you have proved failure to tell the truth. I am confident linakusumbua saaana wewe binafsi pia
What is posho? Nina hakika Rais hawezi kubabaika na hoja ya kijinga ya posho hivi mleta mada hajui kama posho no vijisenti? Kama kweli hao chadema wana uchungu na sie kwanini wasipinge pesa za kiinua mgongo wakimaliza term ya miaka mitano? Kuna wastaafu hawajapata haki zao baada ya kutumikia serikali miaka 40 na zaidi lakini wao wanachokipata ni mara tano ya wanaotumiukia miaka 40. Ila kwa kuwa kiinua mgongo wanajua ni donge nono hawatathubutu kiguswe watabakia kujitoa kimasomaso na pesa mbuzi za vikao.
Acha ujuha wewe huyo mwalimu akistaafu baada ya kula vumbi la chaki analipwa kiinua mgongo shilingi ngapi? Na mbunge akimaliza miaka mitano analipwa ngapi? Kwanini kina zitto wasipokee sawa na waalimu au robo ya waalimu maana wanatumikia miaka mitano mitano na kila kipindi kikiisha wanakula pesa ndefu na wakichaguliwa wanapewa pesa za kununua mashangingi? Wakati mwalimu wako uliemsema hata baskeli hana!c"Ila kwa kuwa kiinua mgongo wanajua ni donge nono hawatathubutu kiguswe watabakia kujitoa kimasomaso na pesa mbuzi za vikao. " Sokomoko.Sasa utataka wadai na mishahara ipigwe marufuku. Posho za ma.ta.ko iwe ni pesa mbuzi au pesa ng'ombe ni wizi wa mchana kweupe! Hiyo ndio hoja! Je mwalimu anapewa hiyo pesa mbuzi kwa kuingia darasani au kukaa katika staff-room? Kama ni 'pesa mbuzi' mbona wamagamba pamoja na ufisadi wao bado wamezing'ang'ania!!! Hiyo 'pesa mbuzi' inaweza kumtoa mtoto wa shule ya msingi kuandikia sakafuni, akaandikia dawatini.View attachment 32772