Hotuba ya mwisho ya gadafo

Hotuba ya mwisho ya gadafo

The Grandson

Member
Joined
Nov 15, 2014
Posts
13
Reaction score
5
HOTUBA YA MWISHO YA GADDAFI
QADAFFI ANAANZA HIVI:
"Kwa jina la Mwenyezi Mungu (Allah), Mungu mpaji,
na mwenye rehema....
Kwa miaka takribani 40 ama ilikuwa zaidi sikumbuki.
Nachokumbuka ni kuwa nilifanya kila nilichoweza
kuwapa watu wangu nyumba, hospitali na shule. Na
kila walipohisi njaa niliwapa chakula. Niliifanya
Benghazi kutoka jangwa kuwa ardhi nzuri ya kilimo.
Nilisimama imara dhidi ya Ronald Regan (Rais wa
zamani wa Marekani), alipomuua binti yangu
niliyemuasili. Alikua anajaribu kuniua mimi lakini
akamuua yule binti yatima masikini. Niliwasaidia kaka
na dada zangu waafrika fedha kupitia AU.
Nilifanya kila nililoweza kuwafanya watu wangu
waelewe maana halisi ya demokrasia; ambapo watu
wa tabaka la chini niliwapa madaraka.
Lakini hawakuridhika. Hata aliyekuwa na nyumba ya
vyumba kumi, nguo mpya, na fanicha nzuri,
hakuridhika. Alihitaji zaidi.
Kwa jinsi walivyokuwa wabinafsi walihitaji zaidi.
Hivyo wakawaambia Marekani kuwa wanataka
"demokrasia" na "uhuru". Hawakujua kuwa
"demokrasia" waliyoitaka ilikua ni mfumo wa
unyonyaji ambapo mbwa mwenye nguvu zaidi huwala
mbwa wadogo.
Walikua hawasikii wala hawaoni. Walitaka
"demokrasia". Wakasahau kuwa hata Marekani
hakukuwa na huduma za afya za bure, dawa bure,
elimu bure na chakula cha bure. (Huduma hizi za
bure zilipatikana Libya tu).
Nchini Marekani mtu masikini/fukara hana cha bure.
Labda awe ombaomba au avuje jasho kuhemea.
Haikujalisha nilifanya kwa kiasi gani bado
hawakuridhika. Lakini wapo waliojua mimi ni mtoto
wa Gamal Abdel Nasser, mwarabu pekee halisi na
kiongozi wa kiislamu tuliyewahi kuwa nae tangu enzi
za Salah-al-Deen.
Wakati Nasser anapigania mfereji wa Suez kwa watu
wake nami nilikua naipigania Libya kwa watu wangu.
Nilikua najaribu kufuata nyayo zake ili kuwaweka
watu wangu huru kutoka kwenye makucha ya
wakoloni wanaotuibia.
Lakini kwa sasa niko mateka katikati ya majeshi
makubwa ya dunia katika historia. Mwanangu
mpendwa mwenye asili ya Afrika, Obama anataka
kuniua.
Ili achukue uhuru wetu, achukue haki yetu ya huduma
za bure za afya, huduma za bure za elimu, na
chakula chetu; na kutuletea mfumo mpya wa
kimarekani wa kuiba uitwao "Ubepari"
Lakini wote katika dunia ya tatu tunajua maana yake.
Maana yake ni kuwa "washirika" wanatawala
mataifa, wanatawala dunia, na watu wanaishia
kuteseka.
Kwa hiyo hakuna mbadala kwangu. Lazima niwe na
msimamo. Na kama Mungu atapenda nitakufa kwa
mapenzi yake.
Mapenzi yake yaliyofanya nchi yetu kuwa na ardhi
yenye rutuba, chakula bora, na huduma bora za afya.
Mapenzi ya Allah yaliyowezesha tukawasaidia kaka
na dada zetu waafrika na waarabu waliokuwa na
shida.
Sipendi kufa; lakini kama nitakufa ili kuiokoa ardhi hii,
kuokoa watu wangu, na wengine ambao ni kama
wanangu; acha nife.!
Acha sauti hii iwe agano langu kwa dunia kuwa
nilisimama kupinga uvamizi wa NATO. Nilisimama
kishujaa kupinga usaliti wa nchi za magharibi na nia
mbaya za kikoloni. Na hapa nimesimama na ndugu
zangu waafrika, kaka na dada zangu waislamu kama
ngao yangu ya matumaini.
Wakati wengine walipokuwa wanajenga majumba ya
kifahari, mimi niliishi kwenye nyumba ya kawaida na
kwenye mahema. Siwezi kusahau maisha yangu ya
utoto kule Sirte.
Sikutapanya rasilimali za nchi yangu kipumbavu. Na
kama alivyokua Salah-al-Deen, kiongozi wetu katika
uislamu, nilichukua kidogo sana kwa ajili yangu, na
sehemu kubwa niliwapa wananchi.
Watu wa magharibi wameniita "kichaa",
"mwendawazimu" lakini wanajua ukweli kuwa mimi
si kichaa wala mwendawazimu; ila waache
waendelee kudanganya. Wanajua hii ardhi ni huru na
haipo kwenye himaya ya kikoloni. Huu ndio msimamo
wangu na dira yangu na imekuwa wazi kwa watu
wangu.
Nitapambana hadi pumzi yangu ya mwisho ili watu
wangu wawe huru. Mwenyezi Mungu atusaidie tubaki
waaminifu na tuwe huru.
-- Mu'uammar Qaddafi.
 
Atakumbukwa daima kwa mazuri aliyowafanyia wananchi wake...inshallah mwenyezi mungu ampe punziko lililo jema...
 
Tatxo Gadafi alizani marekani wanatania!!

Alikua anasema anawasubilia panya wa mwitini wasogee awacharange na nuclear zake!!

Kumbe hakua hata na nusu debe la nuclear!
 
Tatxo Gadafi alizani marekani wanatania!!

Alikua anasema anawasubilia panya wa mwitini wasogee awacharange na nuclear zake!!

Kumbe hakua hata na nusu debe la nuclear!

We mnyalugusu alizani ndio nini na anawasubilia ndio nini? Na mwitini ndio nini?..
 
Back
Top Bottom